Njia za kupunguza ugonjwa wa zinaa

Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika Ili kuweza kupunguza kuwepo kwa magonjwa ya zinaa

Njia za kupunguza ugonjwa wa zinaa.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kuwa ugonjwa wa zinaa uleta matatizo mengi kwenye jamii kwa hiyo tunapaswa kutumia njia mbalimbali Ili kuweza kupunguza ugonjwa huu, kwa hiyo zifuatazo ni mbinu za kupunguza ugonjwa wa zinaa.

 

2 . kutumia kinga wakati wa kujamiiana na kuwa na mpenzi mmoja.

Kwa kutumia kinga kwa mtu ambaye haumfahamu kama ana maambukizi ni jambo zuri na la busara kwa sababu katika kufanya hivyo maambukizi hayawezi kuwepo, pia kuwa na desturi ya kuwa na mpenzi mmoja na kupima mara kwa mara Ili kuangalia kama Kuna maambukizi yoyote walau kila mwezi kama inawezekana.na pia ikitokea kuna maambukizi ni vizuri kupima nyote na kuhaidi kuwa waaminifu katika mahusiano.

 

3. Kuachana na Mila na desturi zinazochangia

 kuwepo na kuenea kwa magonjwa ya zinaa.

Jamii inapaswa kuachana kabisa na Mila na desturi za zamani ambazo usababisha kuenea kwa magonjwa ya zinaa, kwa mfano kukeketa wasichana kwa kutumia wembe mmoja na pia kitendo cha kurithisha wanawake au wanaume ikitokea mmoja amefariki, kwa hiyo hali hii inapaswa kukoma kabisa na jamii za hivi zipatiwe elimu Ili kuweza kuokoa maisha ya watu na kupunguza madhara yatokanayo na magonjwa haya kama vile ugumba na vifo vya watoto wachanga wanaozaliwa na kaswende.

 

4. Kutoa elimu kwa wakimbizi na vijana walio kwenye umri wa kubarehe.

Kwa kawaida katika makazi ya wakimbizi Kuna hattari kubwa ya kuwepo kwa magonjwa ya zinaa kwa sababu ya kuwepo kwa watu mbalimbali na waliokusanyika kwa pamoja kwa hiyo wanapaswa kupewa elimu kuhusu madhara ya magonjwa ya zinaa na njia za kuepuka Nazo ambazo ni kuwa na mpenzi mmoja pamoja na kutumia kondom.

 

5. Vile vina na vijana wanapaswa kuwa na mipaka na kuepukana na matendo ya zinaa katika umri mdogo kwa hiyo wanapaswa kusubiri au hali ikiwa vibaya watumie kinga Ili kuepuka na kuwepo kwa magonjwa ya zinaa.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/11/Wednesday - 10:40:05 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 816


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-