PHP LEVEL 11 SOMO LA KUMI NA MOJA (11)


image


Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form.


SOMO LA 11


HTML FORM
Ili uweze kujaza madodoso kwa kutumia fomu ya HTML utahitaji sehemu ya kwenda hayo madodoso baada ya kujazwa. Kwa kutumia HTML utaweza kutuma na kupokea taarifa zilizokazwa kutoka katika fomu ya html.

Angalia fomu hiyo hapo chini.


 

<html>
<form method="post" action="">
<label>first name</label>:<br>
<input type="text" name="firstname">
<br>
<label>last name</label><br>
<input type="text" name="lastname">
<input type="submit" name="">
</form>
</html>


 

Ukiingalia vyema fomu hii utagunduwa ipo katika namna hii:-
1.Kuna tag ya fomu <form kuonyesha kuwa hapa ndipo fomu inaanzia.
2.Katika tag ya form kuna attribute ambayo ni method <form method attribute hii kazi yake ni kueleza kuwa hizi taarifa za humu kwenye hii fomu baada ya kujazwa zitatumwa kwa njia ipi.
3.Katika attribute method value yake ni post. Hii ina maana njia itakayotumika kutuma taarifa hizi ni njia ya post.
4.Kisha kuna attribute nyingine ndani ta tag ya <form ambayo ni action, hii kazi yake ni kueleza je action zote katika fomu hii zitachakatwa katika faili lipi. Mfano kama utahitaji michakato ifanyikie kwingine kwa sababu za kiulinzi basi utaweka faili unalotaka kwenye value ya attribute action. Katika mfano wetu hapo juu ipengele hili kimeachwa wazi.inamaana action zote zitafanyika hapahapa.
5.Kuna lebo ya firstname na ya last name
6.Kisha kuna input type. Input type hapa ni taarifa ambazo unahitaji huyo mjazaji wa dodoso aweke. Kama unataka aweke email, hpo utaweka email. Katika mfano wetu huu input type ni text, yaani anachotakiwa ajaze mtu ni text ambazo ni herufi, namba na symbils.
7.Mwisho kuna batani ya kusabmit. Hii ndio batani ya kutumia dodoso. Yaani ukiibofya batani hii dodoso litakuwa limetumwa.batani hii yenyewe input type yake ni submit.


 

FORM METHODS
Kama nilivyogusia hapo juu ni kuwa method zipo mbili katika kutuma na kupokea madodoso kutoka kwenye html form moja ni POST na nyingine ni GET. Tunatumia post tunapotuma taarifa za siri, na tunatumia GET tunapotuma ama kupokea taarifa zisizo za usiri. Tutajifunza mengi zaidi kwenye mafunzo ya mbele. Na vinapotumika kwenye file huwa katika sura hii $_POST[''] au $_GET[''] ndani ya hayo mabano utaweka variable zako mfano $_POST['firstname'].


 

UKUSANYAJI WA DODOSO:
1.Kwanza lazima uandae fomu ya kuingiza hizo taarifa mfano tunahitaji kukusanya jina la kwanza na la pili. Hivyo fomu yetu itakuwa na input mbili.
Mfano:

<form method="post" action="#">
First name:<br>
<input type="text" name="firstname">
<br>
Last name:<br>
<input type="text" name="lastname">
<input type="submit" name="">
</form>


 

2.Kisha hatuwa inayofata ni kukusanya hizo taarifa yaani kuzipokea. Hapa tutahitaji kutengeneza variable ambazo zitapokea taarifa kutoka katika fomu. Variable hizi zinatakiwa zifanane na value ya name kwenye input type kwenye html form. Mfano kkwenye input type pale kwenye name ni firstname basi na variable yetu inatakiwa iwe hivyo hivyo firstname.
3.Kisha utaweka output kama itahitajika. Je unataka baada ya taarifa kukusanywa zifanye nini. Mfano tunataka zionyeshwe hivyo tutaunga jina la kwanz ana pili kupata jina zima.
4.Haya yote hufanyakika kwenye lile faili ulilolitaja kwenye action. Kama hukutaja faili basi code zeote za kufanya haya zifanyike kwenye faili moja na hiyo html form.

Cheki mfano wa code nzima hapo chini


 

<html>
<form method="post" action="#">
First name:<br>
<input type="text" name="firstname">
<br>
Last name:<br>
<input type="text" name="lastname">
<input type="submit" name="">
</form></html>
<?php

$firstname=$_POST['firstname'];
$lastname=$_POST['lastname'];
$fullname = "$firstname, $lastname"
echo $fullname;
?>


 

Kwa mfano huu mty ataingiza jina la kwanza kisha la pili, kisha variable ya full name itachanganya firstname na lastname ili kupata fullname. Baada ya hapo echo itadisplay full name.

Vyema kufanyia mazoezi tofautitofauti mifano hii. Katika muendelezo wa masomo haya tutakuja jifunza kwa mfano kama huu kuhifadhi taarifa hizi kwenye database.

Huu ndio mwisho wa masomo haya ya PHP level hii ya kwanza. Tutamalizia project kwenye kipindi cha 12 kisha tutafunga course. Course itakayofata itaingia ndani zaidi katika mafunzo haya. Hivyo nakusihi endelea kuwa nami hadi mwisho.

Mafunzo haya yanakujia kwa ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email:mafunzo@bongoclass.com
Phone: 0774069753 unaweza kunicheki wasap kwa link hii https://wa.me/message/7CTQP5BSWBR5I1

 

 



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mafunzo ya php level 1 somo la pili (2)
hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php. Soma Zaidi...

image Mafunzo ya php level 1 somo la tatu (3)
hili ni somo la tatu katika masomo ya php level 1. Hapa utajifunza zaidi kuhusu variable na namna ya kuitengeneza. Soma Zaidi...

image Mafunzo ya php level 1 somo la kwanza (1)
Karibu kwenye mafunzo ya PHP level 1 na hili ni somo la kwanza. Hapa utajifunza maana ya php, inavyofanya kazi pamoja na historia yake kwa ufupi Soma Zaidi...

image Mafunzo ya php level 1 somo la nne (4)
somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la tano (5)
Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions. Soma Zaidi...

image PHP level 11 somo la kumi na moja (11)
Katika somo hilivutajifunza namna ya kutumia HTML form. Namna ya kuookea taarifa kutoka kwenye madodoso ya html form. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la tisa (9).
Somo la nane mafunzo ya php, katika somo hili utajifunza kuhusu array na jinsi ya kutengeneza array. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la sita (6)
Katika somo hili la php level 1 somo la 6 utajifunza namna ya kutumia tarehe yaani function date() kwenye PHP Soma Zaidi...

image Php level 1 somo la saba (7)
Hili ni somo la saba, mafunzo ya php level 1. Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika function yako mwenyewe. Soma Zaidi...

image PHP level 1 somo la kumi na mbili (12) final
Mafunzo ya php level 1 somo ka 12 mwisho wa mafunzo. Hapa utaona project ambazo unaweza kufanya kutokana na mafunzo haya. Soma Zaidi...