Mie ni kijana wa kiume umri 33, nna tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nna minyoo lakini hata nikinywa dawa sioni afadhali, niliona labda ni pombe nikapumzika kunywa tatizo lipo pale pale japo nisipokunywa haliwi kwa ukubwa ule ila lipo. Dawa za minyoo nilizokunywa ni vumtreNamba ya swali 020

Pole sanaNamba ya swali 020

Endelea kupunguza unywaji wa pombe, ila tafuta hospitali yenye vipimo zaidi upate kuimaNamba ya swali 020

Tatizo la kujaa kwa mate kwenye mdomo kitaalamu hufahamika kama hypersalvation au sialorhea au ptyalism. Kikawaida huu si ugonjwa ila ni dalili ya magonjwa kama:-

1. uJauzito

2. maambukizi kwenye koo

3. vidonda ama uvimbe kwenye mdomo

4. usafi wa Mdomo kuwa mdogo

5. maambukizi ya maradhi kama kifua kikuu

6. mipasuko kwenye taya

7. maumbile ya ulimiNamba ya swali 020

Sawa nitajitahidi kwenda kupimaNamba ya swali 020