Naomba Tafsir ya suratul quraysh na mafuzoyakeNamba ya swali 000

Suratul-Quraysh (106)

Kwa jina la Allah,mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu.
1.Ili kuwafanya Makurayshi waendelee.


2.Waendelee na Safari zao za wakati wa kusi (kwenda Yemen) na wakati wa kaskazi (kwenda Shamu).


3.Basi nawamuabudu Bwana wa nyumba hii (Al-Kaaba).


4.Ambaye anawalisha (wakati Waarabu wenzao wamo) katika njaa, na anawapa amani (wakati wenzao wamo) katika khofu.Namba ya swali 000

Mafunzo yake je?Namba ya swali 000

Mafunzo kwa MuhtasariKutokana na sura hii kwa muhtasari tunajifunza yafuatayo:
(1 )Neema zote zilizotuzunguka zinatoka kwa Allah (s.w).(2)Amani, usalama na ustawi wa kweli hupatikana kwa kumtii Allah (s.w) ipasavyo. Kwa mfano amani na ustawi wa Makka ulipatikana kutokana na dua ya Nabii Ibrahim (a.s) ambaye kwa kumtii Mola wake aliacha familia yake mahali pakavu na papweke pasipo na msaada wowote wa kibinaadamu. Wakati anatekeleza amri ya Allah (s.w) ya kuiacha familia yake pale, Nabii Ibrahim (a.s) aliomba:"Mola wetu! Hakika mimi nimewaweka baadhi ya kizazi changu (mwanangu Ismail na mama yake, Hajar) katika bonde (hili la Makka) lisilokuwa na mimea yoyote katika nyumba yako takatifu. Mola wetu! Wajaalie (wawe) wasimamishaji swala. Na ujaalie nyoyo za watu zielekee kwao na uwaruzuku matunda ili wapate kushukuru" (14:37)3)Mahusiano, maingiliano na mawasiliano baina ya mataifa katika nyanja mbalimbali za kijamii ni katika neema za Allah (s.w)Namba ya swali 000

Shukraa, Allah akuzidishie ElimuNamba ya swali 000

Aaamin Nawe pia ndugu yangu, Allah akupe Neema nyingiNamba ya swali 000