Mimi nilifanya ngono isiyo salama Tar 14/07 mwaka huu, nilikutana tu na mwanamke ambae sikuwa hata na background yake yoyote hivyo baada ya siku tatu nilijikuta nina maambukizi ya zinaha (maumivu wakati wa kukojoa na usaha), hivyo nilienda hospital na kupatiwa matibabu...
Baada ya kuanza dawa kwa muda kama wa wiki moja nilianza kupata maumivu ya kifua na kurudi hoapitali siku ya 12 baada ya tendo, nilipimwa vipimo vyote ikiwepo HIV na sikukutwa na chochote mpaka kufika siku ya 18 nikapata mafua ambayo yameambatana na homa kali na sijakutwa pia na malaria baada ya kwenda hospital, pia nina mamivu ya tumbo hasa sehemu ya chini na kitovu na kifua sehemu za manyonyo
Kwa muda huo wote toka pale nimekuwa natumia dawa tofauti za kifua, gesi tumboni, na mafua lakini mwili kwa sasa una maumivu makali mgongo, mikono na tumbo.
HIV haiwezi kuonekana kabla ya miezi mitatu
Dalili zake huanza kuja baada ya muda gani? Mheshimiwa pia kuhusu hizi changamoto zinaweza kuwa dalili za HIV? Leo ni siku ya 22 baada ya kitendo
Dalili zake zinanzia wiki ya kwanza mpaka miezi mitatu kisha zinapotea kabisa.
Dalili zake ni pamoja na mfua na homa Dokta?
Yes hizo ni dalili, ila zinawwza kuanbatana na mashambukizi mengi. Hivyo uhakika ni kupima baada ya miezi 3. Vipi ulipatabkuvimba mitoki, kwebye mapaja, shingo ama kwapa?
Hapana hiyo sijapata
mitoki ndio matezi?
Yes mitoki ni tezi
Zenyewe zinakuwaje, au ni uvimbe unatokea?
Hizi huwa ni katika viashiria vya mwanzoni sana, hata na huwapata watu wengi, sana
Hiyo sijawahi kupata kabisa, na mbaya zaidi nina hofu ambayo naona mpaka kufikia miezi mitatu itakuwa i,enipeleka pabaya zaidi, kwahiyo kwa kipindi cha miezi mitatu hii homa hazitakwisha?
HIV haipo hivyo kaka, yenyewe ipo siri sana. Inavijidaliki vichache sana, ambavyo sio rahisi kuviona kabisa. Homa kali, iloambatana na maumivu ya kifua, na mafua, huenda ni sababu nyingine kabisa. Ok, ulisema ulitokwa na usaha, bipo ulipopima walikueleza unanshida gani?
Walisema tu kwamba ni shida ya magonjwa ya zinaa ila sikuambiwa ni nini hasa hiyvo nilipatiwa dawa ambazo baada ya kutumia nimekuwa sawa kabisa na nilirudi kwaajili ya vipimo siku tatu baadae baada ya kumaliza dozi na sikukutwa na zile homa tena.
Yes huwenda ilokuwa ni kisonono.
Sawa dokta, naomba niwe naendelea kukujulisha hali yangu, lakini pia nipo Dar es Salaam kama naweza kuja kuonana kwa ushauri zaidi?
Ok