Samahani doctar mimi kila nikiamka asubuhi huwa nakojoa mkojo mchafu sana halafu najiskia vibaya Sana na mwili wote unaniuma je tatizo litakua ni nini
Je unepima UTI?
bado
Pamoja na hilo doctor Mimi huwa Nina presha napatwa na hofu Sana muda mwingine mpaka mshtuko wa moyo na vitu kunitembea mwilini vipi hapo waweza kunisaidia samahani lakini kwa usumbufu doctar
Pole sana. Hofu hiyo kitaalamu hutambulika kama anxiety. Husababishwa na hiyo hali uliyo nayo. Ijapokuwa zipo dawa kwa ajili yankuiondoa ama kuituliza ila ji vyema kufanya yafuatayo:- 1. Pata ushauri kwa washauri wa kidini ama watoaji ushauri nasaha, kuhusu kuondoa hofu. Kamabutaweza fanya mazoezi mara kwa mara mara. Ukipata tatizo halikisha unakabiliana nalo. Jitahidi kuwa mwenye furaha ukiwa nyumbani ama kazini
Hofu ulio nayo inawapata watu wengi, yenyewe si ugonjwa bali inaweza kupewa dawa ama kuondoka yenyewe
Nashukuru Sana ndugu yangu kitu kinachonitia hofu ni vitu kunitembea mwilini
Ni maeneo gani ya mwili?
Kwenye magoti mpaka mabegani
Je unapata maumivu kayika maeneo hayo??
Maumivu sipati ilatu vinatembea kwenye mishipa
Kwenye mishipa, hutokea kwa sababu ya never zenyewe, hii sio tatizo saana. Zipo sababu nyingine ila kama hupati maumivu yeyote, sio shida sana kiafya.
Nashukuru Sana kwa maelezo yako ndugu japo sikufahamu mungu akutie nguvu
Wengine wanasema litakua jini mahaba ndio wananitia hofu sana
Hapana, hali hiyo huwapata hata watu wenye UTI, KISUKARI NA WENYE MATATIZO YA TEZI YA THYROID NA NEVA. Pia huweza kuwapata watu wakati wakiwa na wa hofu. Ila hata hivyo jini mahaba, sijajuwa habari zake zaidi lakini sijapataponkusikia kuwa anaweza kusababisha hali hiyo. Ila ok wanasema dalili za majini huwa vitu hivi vinatokea. kitu cha msingi ni kuwa makini.