Dawa ya fangasi ukeni

Usisumbuliwe tene na fangasi ukeni, zijuwe hapa dalili za fangasi ukeni, tiba yake na njia za kukabiliana na fangasi ukeni

Dawa ya fangasi ukeni

DAWA YA FANGASI UKENI
Fangasi ukeni wanaweza kuwa ni tatizo kubwa na wakati mwengine wanaweza kuleta aina, madhara na kupoteza ladha ya mapenzi. Fangasi ukeni ni rahisi kutibika kama mwanamke atatumia dawa kwa uangalifu. Unaweza kutibu fangasi ukeni kwa kutumia dawa za kupata kutoka katika maduka ya dawa. Kama hali haina nafuu muonedaktari anaweza kukuandikia dawa za kumeza ama sindano ikibidi. Kunawada nyingine si za kupaka ila ni vidonge, hivi mwanamke ataweza ukeni na kitamumunyika chenyewe.



Makala hii inakwenda kukuletea tiba na dawa za fangasi ukeni, sababu zake, namna ya kupambana na fangasi hawa na dalili za fangasi ukeni. Pia tutaona madhara ya fangasi ukeni endapo watachelewa kutibiwa. Soma mkala hii hadi mwisho huwenda ikakusaidia sana.



1.Dawa ya fangasi ukeni ya kupaka
A.Clotrimazole
B.Miconazole
C.Tioconazole
D.Terconazole
E.Butoconazole



Ni vyema kumuona daktari kwanza kabla hujatumia dawa hizi. Kwa mfano terconazole na butoconazole zinahitaji maelezo kutoka kwa daktari kwa usalama zaidi wa afya yako.



2.Dawa ya fangasi ukeni ya kumeza
Endapo dawa za kupaka hazikuonyesha ahueni, mgonjwa atabadilishiwa dawa na kupewa za kumeza ama sindano.fluconazoe (diflucan) hii ni nzuri sana kwa wenye fangasi silizoshindikana kwa dawa za kupaka. Pata kwa nza maelezo ya daktari kabla ya kutumia. Dawa hii haitumiwi na wajawazito. Ukitumia dawa hii unaweza kuona mabadiliko kama maumivu ya tumbo au tumbo kuvurugika na maumivu ya kichwa.



3.Dawa ya fangasi ukeni walio sugu (azole resistant therapy).
Dawa hii sio ya kumeza, maana ni hatari sana. Napi asio ya kupaka. Dawa hii hutumika endapo ddawa za hapo juu zimeshindikana. Kwanamke atapewa dawa hii aiingize kwenye uke wake.



Nini kinasababisha fangasi ukeni?
Fangasi ukeni husababishwa na ina ya fangasi wanaoitwa candida albican. Kikawaida ukeni kuna bakteria na fangasi aina ya candida kwa kiwango maalumu. Pia kuna aina ya fangasi waitwao lactobacillus hawa huzuia ongezeko la fangasi candida wasiwe wengi kupitiliza. Sasa endapo fangasi candida wakizaliana kwa wingi na kupitiliza kiwango ndipo madhara yanaanza kuonekana. Swali la kijuliza hapa inakuwaje fangasi hawa wanazaliana zaidi?



Sababu za kuzaliana fangasi ukeni kwa wingi:
A.Kama mwanamke anatumia dawa za antibiotics
B.Kama mwanamke ana mimba
C.Kisukari kilichoshindwa kudhibitiwa
D.Mfumo wa kinga kudhoofu
E.Kutumia dawa za kudhibiti uzazi wa mpango dawa za kumeza.



Namna ya kujilinda na fangasi wa ukeni
1.Jiepushe kuvaa nguo za ndani zilizobana sana
2.Jizuie kusafisha uke kwa kemikali
3.Jiepushe na baadhi ya vifaa vya wanawake vilivyowekewa manukato kama pedi zenye manukato, badhi ya sabuni zenye manukato za kusafishia uke n.k
4.Kama huna ulazima wa kutumia antibiotics wacha kutumia
5.Usivae nguo zenye majimaji, hakikisha nguo zako ni kavu, ni vuema zile za ndani zikawa ni za pamba.




Dalili za fangasi ukeni
1.Miwasho ukeni
2.Maumivu wakati wa kukojo ana wakati wa kushiriki tendo landoa. Maumivu haya yanaweza kuwa kama unaunguwa ivi
3.Kuvimba kwa papa na kuwa nyekundu
4.Uke kuuma
5.Uke kuota upele ama ukurutu
6.Kutokwa na uchafu ukeni
7.Uke kutoa majimaji memngi



ATHARI ZA KUTOTIBU FANGASI
A.Kuendelea kupata maumivu
B.Kutoa harufu
C.Kuchubuka na hatimaye vidonda
D.Kujikuna muda wote
E.Kutokuwa na raha
F.Maumivu wakti wakukohoa na kushiriki tendo la ndoa
G.Kukosa hamu ya kushiriki tendo ka ndoa.





                   





Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1764


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-