Naomba kujuwa dua ya kuomba jambo ufanikiweNamba ya swali 067

Ili kuomba dua itakayokubaliwa unatakiwa uzingatie adabu za dua, nyakati za kuomba dua pia ujuwe hali zinazozunguruka dua yako. Hapa nitakueleza baadhi ya taratibu za kuomba dua itakayokubaliwa

Zingatia adabu na taratibu za dua kama ifuatavyo:- 1. Omba dua ukiwa twahara
2. Elekea kibla
3. kuwa twahara katika mavazi na mwili
4. Anza na kumsifu Allah (Tahmid, kwa kusema Alhamduliilahi rabbil-'alamiina)
5. Mswalie mtume (Swala ya mtume)
6. waombee dua waislamu wote
7.Taka istighfar kwa kusema Astaghfirullah (mara kadhaa)
8. sasa omba dua yako

Zingatia nyakati za kuomba dua. Nyakati zifatazo dua hukubaliwa rahisi:-
1. siku ya ujumaa
2. usiku wa manane
3. Baada ya Swala
4. Baada ya adhana
5. Wakati ukiwa umefunga
6. Wakati unapofanya jambo jema la kumfurahisha Allah

Pia omba Dua yako katika hali hizi:-
1. ukiwa umefunga
2. baada ya kusoma quran
3. Toa sadaka kisha muombe Allah dua yako
4. Mfanyie wema mtu aliye mbali akikuombea dua yake itakubaliwa.Namba ya swali 067

AhsanteNamba ya swali 067