Kutopupia dunia
"Ewe mwanangu!
(e) Kutopupia dunia
"Ewe mwanangu! Kwa hakika jambo lolote lijapokuwa na uzito wa chembe ya hardali, likawa ndani ya jabali au mbinguni au katika ardhi, Mwenyezi Mungu Atalileta (amlipe aliyefanya); bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo yaliyofichikana, (na) Mjuzi wa mambo yaliyo dhahiri"(31:16).
Aya hii inatuhakikishia kuwa kila mtu amekadiriwa jambo lake na hapana yeyote na hila yoyote itakayomzuia mtu asipate kile alichokadiriwa kukipata au kumuwezesha mtu kupata kile ambacho hakukadiriwa. Pia aya ifuatayo inatuweka wazi zaidi:
โNa hakuna mnyama yoyote (kiumbe chochote) katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Mwenyezi Munguโฆ.. " (11:6)
Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa lengo la maisha yetu si kutafuta rizki na maslahi ya dunia bali vitu hivi ni vitendea kazi tu vyakutuwezesha kulifikia lengo kuu. Lengo letu kuu ni kuusimamisha Uislamu katika jamii ili tuweze kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo katika kila kipengele cha maisha yetu ya kibinafsi na ya kijamii ambalo ndilo lengo la kuumbwa kwetu.
Hivyo katika mchakato wa kuliendea lengo hili la kusimamisha Uislamu katika jamii, tusimchelee yeyote wala
tusichelee kupoteza chochote kwani hamna mwenye uwezo wa kutupokonya au kutuzidishia chochote kile kinyume na alivyotukadiria Allah (s.w). Katika hili ni vyema tukazingatia pia aya ifuatayo:
Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwishaandikwa katika Kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kabla Hatujaumba. Kwa yakini hili ni sahali kwa Mwenyezi Mungu." (57:22).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina ๐2 web hosting ๐3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) ๐4 Dua za Mitume na Manabii ๐5 Bongolite - Game zone - Play free game ๐6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika Surat ahzab
Na waliposema wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, "Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu.
Soma Zaidi...Jifunze ni kwa namna gani Malaika waliweza kuwasiliana ana manabii Malimbali
Wakatibmeingibe Allah anapotaka kuwasiliana na wanadamu hutuma Malaika wake.
Soma Zaidi...Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu.
Soma Zaidi...