picha

Uthibitisho kuwa quran ni maneno ya Allah kutokana na Historia (Hadith)

Uthibitisho kuwa quran ni maneno ya Allah kutokana na Historia (Hadith)

(b)Uthibitisho kutokana na Historia (Hadith)



Historia ya kushuka Qur-an na namna Mtume (s.a.w) alivyoipokea ni ushahidi mwingine unaotuthibitishia kuwa Qur-an si kitabu alichokitunga Muhammad (s.a.w). Kuna maelezo kadhaa ya kihistoria tunayojifunza katika Hadith juu ya namna Mtume (s.a.w) alivyoipokea Qur-an. Hebu turejee hadithi zifuatazo:



(1)Hadithi ya bibi Aysha (r.a) iliyopokelewa na Imamu Bukhari inatufahamisha namna Mtume (s.a.w) alivyopokea wahyi wa kwanza wa Qur-an alipokuwa katika pango la Jabal Hira. Kama tulivyojifunza katika hadithi hiyo Mtume (s.a.w) alistushwa sana na tukio lile la kujiwa na Malaika Jibril (a.s) na kumuamrisha kusoma kinyume na uwezo wake. Tukio lile lilimhofisha sana Mtume (s.a.w) na kumfanya arejee nyumbani kwake akiwa anatetemeka. Tukio la Jabal Hira ni ushahidi mwingine tosha kuwa Qur-an si maneno ya Muhammad (s.a.w) bali ni ujumbe kutoka kwa Allah (s.w) uliofikishwa kwake kwa njia ya wahyi kupitia kwa Malaika Jibril.



(2)Mtume (s.a.w) alikuwa akibadilika haiba yake na kutokwa na jasho wakati wa kupokea wahyi kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
Bibi aysha (r.a) amesimulia: Kwa hakika nimemuona Mtume akiteremshiwa wahyi siku ya baridi kali na baada ya kumaliza kile kipindi cha kuteremshiwa wahyi alimininikwa na jasho jingi kichwani mwake." (Malik)



Amesimulia Aysha (r.a), "Al-Harith bin Hisham (r.a) alimuuliza Mtume wa Allah, 'Ee mtume wa Allah! Ni vipi wahyi unakuja?' Mtume wa Allah alijibu, "Wakati mwingine ulifunuliwa kwangu kwa sauti mithili ya mlio wa kengele, wahyi ulioletwa kwa namna hii ulikuwa mgumu sana kuliko aina nyingine zote (za wahyi), kisha hali hii ilikwisha baada ya kukidhibiti kile kilichofunuliwa. Wakati mwingine Malaika


(Jibril) alikuja katika umbile la binaadamu na kuzungumza nami, ambapo nilikidhibiti (nilikichukua) chochote kile alichosema." Aysha (r.a) aliendelea kusema: Hakika nilimuona Mtume (s.a.w) wakati anateremshiwa wahyi siku ya baridi kali na kuona jasho likitiririka usoni mwake." (Bukhari)
Hadithi hizi nazo zinatuthibitishia kuwa Qur-an si utunzi wa Muhammad (s.a.w) kabisa,bali ni ujumbe wa Allah (s.w) uliopitia kwake kwa njia ya wahy.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 2711

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 web hosting    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

HUKUMU ZA IDGHAM

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
KISA CHA TEMBO KATIKA QURAN, KUHUSU ABRAHA KUTAKA KUVUNJA AL-KABA NYUMBBA YA aLLAH

KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBOTukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji.

Soma Zaidi...
Hukumu za waqfu na Ibtida

waqfu ni misimamo ambapo msomaji wa Quran anaruhusiwa kusimama, kuhema au kumeza mate. Na ibtidai ni kuanza baada ya kutoka kwenye waqf

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa Surat al-Kawthar na fadhila zake

SURATUL-KAUTHAR Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail.

Soma Zaidi...
Hukumu ya Ikhfau katika tajwid

Ikh-fau ni moja ya hukumu za nun sakina na tanwin kwenye hukumu za Quran tajwid

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka Surat al Kafirun

Sura hii imekuja kukata rai ya Makafiri wa Makka kuhusu ibada ya ushirika. Hivi leo tungesema kuhusu dini mseto.

Soma Zaidi...
hukumu za kujifunza tajwid

Kujifunza tajwid ni katika mambo muhimu wakati wa kusoma Quran

Soma Zaidi...