Quran si Mashairi kama wanavyodai makafiri
(i)Dai kuwa Qur-an ni Mashairi aliyotunga Muhammad (s.
(i)Dai kuwa Qur-an ni Mashairi aliyotunga Muhammad (s.a.w):
Dai hili lilitolewa na Makuraishi katika enzi hizo za kushuka kwa Qur-an pia linaendelea kutolewa na makafiri wa karne hizi. Kwa mfano Stober, baada ya kusoma tafsiri ya Qur-an alidai kuwa itakuwa imeandikwa na Mwarabu ambaye ni mweledi wa historia ya Mayahudi na mila za nchi yake ambaye pia ni mshairi mzuri.
Udhaifu:
Wasomaji wa mashairi ya Kiarabu wanafahamu kuwa mashairi hayo yana mizani,beti na vina na yanaimbika kwa kiasi kwamba wakati mwingine inabidi hata maana au sarufi viwekwe pembeni alimradi tu shairi liimbike. Hivi sivyo kabisa ulivyo mfumo wa Qur-an. Qur-an si mashairi bali ni ujumbe wenye maana kamili ulioandikwa katika fasihi ya hali ya juu kwa kuzingatia sarufi na miiko yote ya lugha hai
.
Historia imeshuhudia kuwa Qur-an si mashairi. Ilikuwa kawaida ya washairi wakati ule wa Mtume (s.a.w) kubandika mashairi yao kwenye mlango wa Ka'aba kama changa-moto kwa washairi wengine. Ilitokea siku moja mshairi mashuhuri wa wakati huo, Labbiib ibn Rabiah, akabandika shairi lake kwenye mlango wa Ka'aba ili kutoa changamoto kwa washairi wengine. Shairi lake lilikuwa limetungwa kwa utaalamu mkubwa sana na lilikuwa zuri mno kiasi cha kutothubutu mtu yeyote kupambanisha shairi lake na hilo. Lakini baada ya kubandikwa kipande cha Sura ya Qur-an karibu na shairi lake, Labbiid mwenyewe (ambaye alikuwa Mshirikina) baada ya kusoma mistari michache ya sura hiyo alinaswa na mvuto wake na kuiamini dini iliyofunuliwa kutoka kwa Allah (s.w) na kubandua shairi lake
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 web hosting 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Sababu za kshuka surat al Asr
Sura hii ni katika sura za kitawhidi sana. Maulamaa wanasema inatosha sura hii kuwa ni mawaidha. Imamu sharifu anasema kuwa sura hii inatosha kuwa muongozo…
Soma Zaidi...Sababu za kushuka kwa Surat al-Kawthar na fadhila zake
SURATUL-KAUTHAR Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail.
Soma Zaidi...Fadhila za kusoma surat al Baqarah
Surat al Baqarah ni katika sura ambazo tunapaswa tuwe tunasoma mara kwa mara. Post hii itakufundisha kuhusu fadhila za sura hii.
Soma Zaidi...yaliyomo: HUKUMU YA MIM SAKINA, NUN SAKINA, MADA, WAQFU, QALAQALA, TAFKHIM NA TARQIQ, USOMAJI WA QURAN
DARSA ZA TAJWID YALIYOMOSURA YA 01 .
Soma Zaidi...