Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat

"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi.

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat

1. Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat (49:15)


"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi." Ambao husimamisha swala na wanatoa katika yale tuliyowapa. Hao ndio wanaoamini kweli kweli, wao wana vyeo (vikubwa) kwa Mola wao, na msamaha na riziki bora kabisa". (8:2-4)


"Wenye kuamini kweli kweli ni wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kisha wakawa si wenye shaka na wanaopigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao. Hao ndio wenye kuamini kweli kweli." (49:15)



Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa waumini wa kweli ni wale wenye sifa zifuatazo:
(i)Wana yakini kuwa Allah (s.w) yupo
Waumini wa kweli huwa na yakini nyoyoni mwao juu ya kuwepo Allah (s.w) na Mtume wake. Yaani wanashuhudia kwa dhati nyoyoni mwao kuwa Allah (s.w) ni Mola wao pekee na Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake wa mwisho na katika matendo yao yote huishi kwa kufuata mwongozo wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na daima hukumbuka msisitizo wa aya ifuatayo:



β€œHaiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri wawe na hiari katika shauri lao. na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa)." (33:3 6)



(ii)Humcha Allah (s.w) kwa kutekeleza amri zake
Anapotajwa Mwenyezi Mungu au wanapokumbushwa juu ya maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hunyenyekea na kufuata kama walivyokumbushwa. Hufanya hivyo kwa kukhofu ghadhabu za Mwenyezi Mungu na kutarajia radhi zake.



(iii)Huongezeka Imani yao kwa Kusoma na kufuata Qur-an
Wanaposoma aya za Mwenyezi Mungu huwazidishia imani kwa maana nyingine, waumini wa kweli hufuata mwongozo wa Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao ya kila siku. Hawako tayari kufanya jambo lolote kinyume na mwongozo wa Allah (s.w). Imani huongezeka kwa kutenda inavyostahiki kwa mujibu wa maelekezo ya Allah (s.w).



(iv)Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Wanamsimamo thabiti na hawayumbishwi na yeyote katika kutekeleza wajibu wao kwa Mola wao. Wanayakini kuwa aliyenusuriwa na Allah (s.w) hakuna wa kumdhuru na aliyeandikiwa kupata dhara na Allah (s.w) hakuna wa kumnusuru.


(v)Husimamisha Swala
Husimamisha swala katika maisha yao yote. Huswali swala zote za faradhi na swala za Sunnah kwa kadiri ya uwezo wao kwa khushui (unyenyekevu) huku wakizingatia masharti na nguzo za swala. Na kwahiyo hufikia lengo la swala kwa kutojihusisha kabisa na mambo machafu na maovu. Pia husimama kidete kuondoa maovu na machafu yaliyopo katika jamii.



(vi)Husaidia wenye matatizo katika jamii
Huwa wepesi wa kutoa msaada wa hali na mali kwa wanaadamu wenzao wanaohitajia msaada. Pia hutoa mali zao na nguvu zao kwa ajili ya kuendeleza Uislamu na kuusimamisha katika jam ii.



(vii)Hupigania Dini ya Allah (s.w)
Wanafanya jitihada za makusudi kwa kutumia mali zao na kujitoa muhanga nafsi zao ili kuhakikisha kuwa dini ya Allah inasimama katika jamii. Yaani wanajitahidi kwa jitihada zao zote ili kuzitafanya sharia za Allah (s.w) ziwe ndizo zinazotawala harakati zote za maisha ya jamii. Lengo lao kuu la maisha ni kuutawalisha Uislamu katika jamii.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 994

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰2 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰4 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Sifa za wuamini zilizotajwa katika surat Al-ma'aarij

Kwa hakika binaadamu ameumbwa, hali ya kuwa mwenye pap atiko.

Soma Zaidi...
Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu

Nguzo za imani (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu

Soma Zaidi...
Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake

Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu.

Soma Zaidi...
Mwanadamu hawezi kuishi bila dini kutokana na vipawa alivyooewa na Allah

Je ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya kuwa na dini?. Vipawa alivyopewa na Allahni jibu tosha juu ya swali jilo

Soma Zaidi...
Maana ya kuamini malaika katika maisha ya kila siku

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Nafsi ya mwanadamu inavyothinitisha uwepo wa Allah

Mwanadamu ukifikiria vyema. Kuhusu nafsi yako, hakika utapatabfikra yabuwepp wa Mwenyezi Mungu

Soma Zaidi...