Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Mu’uminuun (23:1-11)

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Mu'uminuun (23:1-11)

3. Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Mu'uminuun (23:1-11)



Pia sifa za Waumini zinabainishwa katika Suratul-Muuminuun katika aya zifuatazo:


Hakika wamefuzu waumini ambao katika swala zao huwa wanyenyekevu. (23:1-2)


Na ambao hujiepusha na Lagh-wi (mambo ya upuuzi). Na ambao (nguzo ya) Zaka wanaitekeleza. (23:3-4)



Na ambao tupu zao wanazihifadhi isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyomiliki mikono yao ya kuume. Basi hao ndio wasiolaumiwa. (23:5-6)


Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. Na ambao amana zao na ahadi zao wanaziangalia. (23: 7-8).


Na ambao swala zao wanazihifadhi. Hao ndio warithi. (23:9-10)


Ambao watarithi Firdaus (Pepo ya daraja ya juu wakae humo milele. (23:11)



Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa, waumini wa kweli waliofuzu na watakaostahiki kupata Pepo ya Firdaus, (ya daraja ya juu kabisa) ni wale wanaojipamba na sifa zifuatazo:



(i)Wenye Khushui katika Swala
Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala. Yaani huswali kwa kutulizana kimwili, kimoyo na kifikra, huku wakizingatia yale wayasemayo mbele ya Mola wao wakiwa na yakini kuwa anawaona na anawasikia.



(ii)Wenye Kuhifadhi Swala
Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu sharti zote za swala, nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume (s.a.w) na hudumu na swala katika maisha yao yote. (Qur-an 70:23)



Zingatio:
Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote.


(iii) Wenye kuepuka Lagh-wi
Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi. Laghwi ni mambo ya upuuzi yanayomsahaulisha mtu kumkumbuka Mola wake, yanayosababisha ugomvi au bughudha baina ya watu na yanayomsahaulisha mtu kuswali (Qur-an 5:91). Mahala ambapo Allah (s.w) hakumbukwi, shetani huchukua nafasi. michezo yote ni lagh-wi isipokuwa ile tu inayochezwa kwa kuchunga mipaka yote ya Allah (s.w) kwa lengo la kukuza ukakamavu na siha ili kuwa imara katika kusimamisha Uislamu katika jamii.



(iv)Hutoa Zakat na Sadakat
Waumini wa kweli waliofuzu hutoa Zakati wakiwa na mali na hutoa misaada na huduma waziwezazo kwa wanaadamu wenziwe kwa kadiri ya haja ilivyojitokeza. Asiyejali binaadamu wenzake, huku ana uwezo si Muumini. Rejea Qur-an (107:1-3).



(v)Wenye kujiepusha na Zinaa na Tabia za Kizinifu.
Waumini wa kweli waliofuzu hujihifadhi na zinaa au hujiepusha kufanya jimai nje ya mipaka aliyoiweka Allah (s.w). Hatua ya kwanza ya kujilinda na zinaa ni kujiepusha na vishawishi vyote vinavyokurubisha watu kwenye zinaa. Muumini wa kweli hutekeleza pasina kusita ile amri ya Allah (s.w) ya katazo kuwa:


Wala usiikaribie zinaa; kwa hakika huo ni uchafu na ni njia mbaya kabisa. (17:32)



(vi)Huwa Muaminifu
Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana. Hutunza amana aliyopewa na kuirejesha au kuitumia kwa mujibu wa maelekezo ya mwenyewe. Amana kuu aliyopewa mwanaadamu na Mola wake ni kule kufadhilishwa kwake kuliko viumbe vingine vyote (Qur-an (17:70),(95:4) ili asimamishe Ukhalifa (utawala wa Allah) katika ardhi kama tunavyokumbushwa katika Qur-an:


"Kwa yakini Sisi tulidhihirisha amana kwa mbingu, ardhi na milima, vikakataa kuichukua na vikaiogopa, lakini mwanaadamu aliichukua. Bila shaka yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana." (33:72)



(vii)Wenye Kutekeleza Ahadi
Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.w). Ahadi kubwa wanayotoa Waislamu mbele ya Allah (s.w) ni Shahada; pale wanapoahidi kuwa hawatamshirikisha Allah (s.w) na chochote na kwamba wataishi maisha yao yote kwa kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mtume wake, Muhammad (s.a.w).




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 130

Post zifazofanana:-

CHUKUWA TAHADHARI HIZI KWENYE MAZINGIRA ILI KULINDA AFYA YAKO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

quran na sayansi
Soma Zaidi...

Faida za kula uyoga
Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya Soma Zaidi...

NAMNA MTUME(S.A.W) ALIVYOSIMAMISHA DOLA YA KIISLAMU MADINAH
Safari ya Mtume(s. Soma Zaidi...

Promo
Kama wewe ni Muandishi mzuri za hadithi au makala za kutoa elimu kwa watu na unataka kazi yako iwafikie watu wengi, au unataka kazi yako iweze kukuingizia kipato, Bongoclass ndio mtatuzi wako sasa. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MVUVI NA JINI
Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat As-Sajida
Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya? Soma Zaidi...

ZIJUWE NYANJA KUU 6 ZA AFYA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

vocabulary test 002
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula magimbi
Soma Zaidi...

Rangi za matunda
Fida za matunda huanzia kwenye rangi zake, je unajuwa kama rangi ya matunda inaeleza jambo? Soma Zaidi...

Kamaralzaman akiwa katika ndoto ya kweli
NDOTO AMA KWELI? Soma Zaidi...