Muhtasari wa sifa za waumini

Lengo tarajiwa la Muhtasari huu ni kutuwezesha kuzibaini fika sifa za Waumini zilizoainishwa katika Qur'an, kisha kujipamba nazo ili tuwe waja wema watakaorehemewa na kuridhiwa na Allah (s.

Muhtasari wa sifa za waumini

Muhtasari wa sifa za waumini



Lengo tarajiwa la Muhtasari huu ni kutuwezesha kuzibaini fika sifa za Waumini zilizoainishwa katika Qur'an, kisha kujipamba nazo ili tuwe waja wema watakaorehemewa na kuridhiwa na Allah (s.w).



1. Al-Anfal (8:2-4).
(i) Anapotajwa Allah (s.w) nyoyo zao hujawa na khofu
(ii)Wanaposomewa aya za Allah (s.w) huwazidishia Imani.
(iii)Wanamtegemea Mola wao tu basi katika kila jambo lao.
(iv)Wanasimamisha swala.
(v)Wanatoa katika yale walioruzukiwa na Mola wao ikiwa ni pamoja na Zakat, Sadaqaat, n.k. kwa ajili ya Allah (s.w).


2. Ar-Raad (13:19-24)
(i)Huamini na kuyafuata yaliyotoka kwa Allah (mafundisho ya Qur'an na Sunnah).
(ii)Hutimiza Ahadi ya Allah (s.w) (6:162:163), (7:172-173), (33:72-73).
(iii)Hawavunji ahadi za wanadamu wenzao kwa hali yoyote ile.
(iv)Huyaunga aliyoamuru Allah (s.w) yaungwe .
(v)Humuogopa Mola wao kwa kuzingatia uwezo wake, nguvu zake, na mamlaka yake yasiyo na kikomo.
(vi)Huiogopa siku ngumu ya Hesabu na Hesabu mbaya ikawa sababu ya kuyakimbia maovu na kuyaendea mema na mazuri.
(vii)Ambao pia huwa na subira na uvumilivu katika mazito yanayowakabili katika maisha.
(viii)Husimamisha swala.
(ix) Hutoa katika vile walivyoruzukiwa na Allah (s.w) kwa siri na dhahiri.



3. Al-Mu'uminuuna (23:1-11).
(i)Huwa wanyenyekevu katika swala zao.
(ii)Hujiepusha na mambo ya upuuzi (laghwi) - Upuuzi ni jambo lolote ambalo humtoa mtu katika lengo la kumuabudu Allah (s.w) na kusimamisha Ukhalifa katika jamii.
(iii)Hutoa katika yale waliyoruzukiwa na Allah (s.w).
(iv)Huhifadhi tupu zao kwa kusitiri uchi na kujiepusha na zinaa.
(v)Huchunga amana zao.
(vi)Hutekeleza ahadi zao.
(vii)Huhifadhi swala zao.


4. Al-Furqaan (25:63-77).
(i)Huwa ni wanyenyekevu (walioepukana na kibri, majivuno,(n.k.) na wenye nidhamu katika kuendesha maisha yao ya kila siku.



(ii)Watu wajinga (wasio na nidhamu wala ustaarabu katika maisha yao) wakiwakorofisha huwasiliana nao kwa njia ya amani (husema nao maneno ya salama).



(iii)Hupitisha baadhi ya saa zao za usiku kwa ajili ya Mola wao kwa kusujudu na kusimama (kuswali Tahajjud/Qiyaamullayl).



(iv)Humuomba Mola wao awaepushe na adhabu ya Jahannam kwa kujua kwamba ni pahala pabaya pa kukaa Mja.



(v)Wanapotumia hawafanyi Israaf (kutumia kwa fujo) wala hawatumii kwa ubakhili bali hutumia kwa kadiri ( kati kwakati).



(vi)Hawamuombi mungu mwingine pamoja na Allah(s.w) na hawamshirikishi Allah (s.w) katika aina zote za shiriki. (vii)Hawaui nafsi iliyoharamishwa kuuawa ila kwa haki. (viii)Hawakaribii zinaa wala kuzini.



(ix)Huwa na tabia ya kuleta toba ya kweli kila wanapokosea kosa dogo au kubwa kwa kufuata masharti yake ambayo ni (1) Kumuamini Allah (s.w) ipasavyo, (2) Kudumu katika kutenda vitendo vizuri, (3) Kujutia dhambi waliyofanya, (4) Kuchukuwa ahadi na azma ya kutorejea tena dhambi hiyo (5) Kurejesha haki kwa wenyewe (6) Kisha kumuelekea Mola na kumuomba msamaha kwa khushui.



(x)Hawashuhudii shahada za uongo (hawatoi ushuhuda wa uongo) hata kama ni juu ya nafsi zao au watu wao wa karibu. (xi)Wanapopita penye upuuzi, hupita kwa heshima zao.


(xii)Wanapokumbushwa Aya za Mola wao hawaziangukii kwa uziwi na upofu (huziingiza katika utendaji).



(xiii)Humuomba Mola wao awape wake wema na watoto we ma.



(xiv)Humuomba Allah (s.w) awajaalie kuwa viongozi wa wamchao yeye (Allah) ambao ni wapesi kuelekea katika njia iliyonyooka.


5.As-Sajdah (32:12-20).
(i) Wanapokumbushwa Aya za Mwenyezi Mungu huzitii na kuzitekeleza ipasavyo
(ii)Humtukuza Mola wao kwa sifa zake tukufu (huleta mara kwa mara tasbihi, tahmid, tahlili, takbir, n.k.)
(iii)Hawafanyi kiburi katika ardhi (Hawatakabari).
(iv)Huinua mbavu zao usiku kutoka vitandani mwao kwa ajili ya kuswali Tahajjud, kwa kuogopa Moto na kutaraji Pepo. (v) Hutoa katika vile walivyoruzukiwa na Mola wao.
6.Al-Ahzaab (33:35-36)
(i)Husimamisha nguzo za Uislamu ipasavyo.
(ii)Huamini nguzo zote za Imani ipasavyo kimatendo.
(iii)Ni watiifu kwa Allah (s.w) ipasavyo katika kuendesha maisha yao ya kila siku.
(iv)Husema kweli na kusimamia ukweli.
(v)Huwa na subira.
(vi)Ni wanyenyekevu kwa Allah (s.w) katika kuendesha maisha yao.
(vii)Hutoa vile walivyoruzukiwa na Allah (s.w) kuwapa wanaostahiki.
(viii)Hufunga swaumu ya mwezi wa Ramadhani na funga za Sunnah.
(ix)Huhifadhi tupu zao na hujiepusha na zinaa.
(x)Humkumbuka Allah (s.w) kwa wingi na kumtaja kwa wingi. (xi)Hawawi na khiyari katika mashauri ambayo Allah (s.w) na Mtume wake wameshapitisha hukukumu juu yake (yaani hutii bila ubishi au bila kuhoji).

7.Ash-Shu'ura (42:30-43).
(i)Wanamuamini Allah (s.w) na Mtume wake na nguzo zote za Imani.
(ii)Humtegemea Mola wao katika kila jambo lao
(iii) Wanajiepusha na Madhambi makubwa na hujiepusha na mambo mabaya.
(iv)Wanapokasirika husamehe.
(v)Huitikia amri za Mola wao kila wanapoamrishwa.
(vi)Husimamisha swala.
(vii)Hushauriana katika mambo yao.
(viii)Hutoa katika vile walivyoruzukiwa na Mola wao. (ix)Jeuri inapowafikia huzitetea nafsi zao.
(x) Husuluhisha ugomvi baina yao.
(xi)Hulipiza kisasi baada ya kudhulumiwa.
(xii)Huwa na Subira.



8.Al-Maarij (70:19-35).
(i) Husimamisha swala.
(ii)Hudumisha sala zao.
(iii)Katika Mali zao iko sehemu maalumu ya kuwapa
wanaostahiki.
(iv)Husadiki siku ya Malipo.
(v)Huogopa adhabu itokayo kwa Mola wao.
(vi)Huhifadhi tupu zao. (vii)Huzichunga amana zao. (viii)Huziangalia ahadi zao.
(ix)Wako Imara katika Ushahidi wao (husimamia ushahidi
vilivyo).



9.Al-Hujuraat (49:15).
(i) Humuamini Allah na Mtume wake ipasavyo kwa kufuata kwa unyenyekevu maamrisho yao yote na kuacha kwa unyenyekevu makatazo yao yote.
(ii)Hupigania dini ya Allah kwa mali zao na nafsi zao.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 197

Post zifazofanana:-

MAMBO YANAYOBATILISHA (HARIBU) SWALA YAKO
Lugha ya Swala Lugha ya swala,kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni Kiarabu. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Darsa za dua
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 04
Soma Zaidi...

Nini maana na Trojan na ni zipi athari zake kwenye kompyuta ama simu
Soma Zaidi...

Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake
Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s. Soma Zaidi...

MAWAKALA WA MARADHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

SWALA YA MTUME (s.a.w)
SWALA YA MTUME Kumswalia Mtume (s. Soma Zaidi...

Nini maana ya najisi, na ni zipi Najisi katika uislamu na aina za najisi
Soma Zaidi...

CHEMSHABONGO NA BONGOCLASS
Soma Zaidi...

nmna ya kufanya istikhara na kuswali swala ya Istikhara
Soma Zaidi...

HIKUMU YA BASMALLAH YAANI KUSOMA BISMILLAH
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

tawhid
Soma Zaidi...