Saratani (cancer)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maradhi ya cancer/saratani

SARATANI (CANCER)

Saratani ni ugonjwa unaotokana na kukuwa kwa seli ndani ya mwili bila ya mpangilio maalumu. Kukuwa huku kunashindwa kuthibitika ndani ya mwili. Seli hizi hukuwa na kusababisha kitu kinachoitwa kitaalamu tumor. Hii ni mkusanyiko wa hizi seli ambazo zimekuwa bila ya mpangilio maalumu ndani ya mwili. Hizi tumor husababisha kutokea kwa malignant tumor na hii ni mkusanyiko mkubwa wa hizi seli ambao huuwa seli nyingine za mwili na tishu. Hutokea wakati mwingine huu mkusanyiko ukawepo ila ukawa hauna madhara kwa seli nyingine, huu utaitwa benign tumor ila zikikuwa zaidi huweza kuathiri tishu za mwili. Hizi tumor zinaweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kuenea sehemu zingine za mwili.

 

Seli za saratani ni hatari zaidi kwani zinaweza kuharibu tishu na viungo vingine vya mwili kama ubongo na maini. Kiti hatari zaidi kwenye seli hizi ni kuwa zinaweza kuhama sehemu moja ya mwili kwenda sehemu nyingine. Kwa mfano saratani ya maini inaweza kuenea kwenye ubongo na kusababisha saratani ya ubongo. Saratani ya matiti na korodani inaweza kuenea kwenye mifupa na kusababisha saratani ya mifupa.

 

Hali hii hufanya seli hizi ziwe hatari zaidi. Mchakato huu wa kuhama sehemu moja kwenda nyingine huitwa kitaalamu metastasisi.

 

Seli ya saratani ya kwanza hutokea pale gene zinapopata hitilafu. Gene ni chembechembe ambazo huhusika katika kutengenezwa kwa selimmpya. Mtu anaweza kurithi gene hizi ambazo zimeharibiwa toka kuzaliwa ama akawa anazo zimeharibiwa kwa sababi zingine. Ila mtu huyu aliyerithi gene ambazo zina hitilafu ni rahisi kwake kupata saratani zaidi kuliko huyu ambaye hajarithi. Kama tulivyoona juu kule kuna mawakala wa kueneza maradhi, hali kama hii kuna mawakala wa kusababisha saratani ambao huitwa carcinogens hawa pia huhusika katika kutia hitilafu kwenye genes. Mifano ya mawakala hawa (carcinogens ) ni ;-

1.Aina flani ya virusi kama vile papilloma virus (HPV)

2.Mionzi kama radio na ulteraviolent (UV) na mionzi mingineyo.

3.Kemikali zinazopatikana kwenye tumbaku kama arsenic, benzene na formaldehyde

4.Asbestos haya ni malighafi zinazotumika kutengezea vifaa vya umeme na vifaa vingine vya nyumba kama vya kuzuia moto.

 

Ni vigumu sana kuepukana na mawakala hawa kwenye maisha, kwani huweza kupatokana kwwenye vyakula vyetu, shuhuli zetukwenye maji na hewa. Ila tutakujaona kwamba unaweza kujiepusha na hatari za saratani kwani karibia mawakala walotajwa hapo juu hueneza saratani ila kwa uchache ila tumbaku ni kwa kiasi kikubwa sana.

 

Unaweza ukagunduwa saratani kwa kutumia vifaa vya kitaalamu kama MRI, x-rays, biospy, na DNA test. Pia unaweza ukajijua mwenyewe kama una tumor kwa kujishika sehemu husika na kuona kama kuna uvimbe wowote usio wa kawaida. Pia ijulikane kuwa zipo tiba za saratani ijapokuwa kuimaliza kabisa mwilini ni kazi mzito ila ukweli ni kuwa karibia aina zote za saratani zinaweza kutibiwa kama mtu atawahi kwa haraka.baadhi ya njia wanazotumia kupambana na saratani ni kama

A)kufanyiwa upasuaji, hufanyika kwa ufasaha zaidi kama saratani haijaenea zaidi

B)Kufanya chemotherapy ni matumizi ya dawa kwa ajili ya kuuwa seli za saratani, ila kwa bahati mbaya njia hii pia huuwa seli nyingine za mwili

C)Radiation therapy ni kutumia mionzi kwa ajili ya kuuwa seli za saratani

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-07     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 840

Post zifazofanana:-

Ifahamu dawa ya kupunguza maumivu
Post hii inahusu dawa ya aspirin katika kupunguza maumivu,ni dawa ambayo upunguz maumivu ya Kawaida, kushusha homa na pia usaidia kwenye magonjwa ya moyo hasa kuzuia stroke kama imetokea mda ndani ya masaa ishilini na manne Soma Zaidi...

Fahamu antibiotics ya asili.
Post hii inahusu zaidi antibiotics ya asili, ni antibiotics inayotumia vitu vya kila siku na ya kawaida na mtu akaweza kupona kabisa na kufanya kazi kama antibiotics ya vidonge vya kawaida. Soma Zaidi...

Safari ya saba ya Sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Faida za kula karoti
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kula karoti Soma Zaidi...

Dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanaume
Posti hii inakwenda kukuletea dalili za fangasi wa sehemu za Siri kwa wanaume Soma Zaidi...

Hiv n kweli majivu hutoa mimb ya siku moja hadi wiki moja
Inashangaza sana, wakati wengine wanahangaika kutafutavijauzito kwa gharama yoyote ile, kuna wengine wanataka kutoa ujauzito kwa gharama yeyote ile. Unadhani njia za kienyeji sa kutoa mimba ni salama? Soma Zaidi...

Dalili za madhara ya ini
Ini Ni kiungo kikubwa Sana mwili na hutumika kuondoa sumu mwili ambayo hujulikana Kama detoxification Soma Zaidi...

Nini maana ya kusimamisha swala?
Je kusimamisha swala kuna maana gani kwenye uislamu? Soma Zaidi...

Mrembo mtoto wa tajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Siri ya wageni wale inafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Sababu za kushukasurat an Nasr
Sura hii ni katika sura za mwisho kushuka, huwendakuwa ndio ya mwisho kabisa. Masahaba waliamini kuwa sura hii imetabiri kifo cha Mtume S.A.W Soma Zaidi...

Nguzo kuu za umama katika umri wa kupata watoto na kulea watoto
Posti hii inahusu zaidi nguzo kuu za umama katika umri wa kujifungua na kulea watoto, ni kipindi ambacho mama anakuwa analea watoto kwa kawaida kadri ya makadirio kipindi hiki uanza kati ya miaka kumi na mitano mpaka arobaini kwa walio wengi na kinaweza k Soma Zaidi...