Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa
Kama unapata maumivu wakati wa tendo la ndoa, suluhisho lako lipo kwenye makala hii

MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA NA BAADA
Hii ni hali inayowapata wanawake kwa kiasi kikubwa wakati wanaposhiriki tendo la ndoa. Maumivu haya pia yanaweza kumpata mwanaume ila kwa uchache sana. Hali hii kitaalamu inafahamika kama dyspareunia.
Maumivu haya yanaweza kutokea wakati wa uume unapoingia kwa mara ya kwanza, ama wakati wote wa kuingia na kutoka ama baada ya kumaliza tendo la ndoa. Maumivu ya wakati wa tendo la ndoa yanaweza kutokea kwenye uke, ama uume ama kwenye tumbo kwa kwa wanawake. Makala hii itakwenda kukuorodheshea sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Sababu za maumivu wakati wa tendo la ndoa
1.Uke kuwa mkavu kutokana na maandalizi mabovu kabla ya kuingiza uume. Pia inaweza kuwa ni kutokana na kukosa hamu ya kushiriki tendo.
2.Kuwepo kwa majeraha kwenye uume ama uke. Majeraha haya yanaweza kuwa ni kukeketwa ana ya namna nyingine.
3.Kuwepo kwa uvimbe ama ukawa na matatizo ya ngozi katika sehemu za siri. Haya yote yanaweza kusababisha maumivu wakati wa kuingia kwa uume.
4.Maumbile ya uke. Wakati mwingine jinsi uke ulivyo inaweza kuwa ni tatizo. Kuwa uke mwingine unatabia ya kubana misui yake. Hali hii inaweza kupelekea maumivu wakai wa kupenya kwa uume.
5.Matatizo ya kimaumbile, kwa mfano kuwa na ukilema kwenye uke, ama kuwa na nyama ama ngozi ambayo inaweza kuzuia kupenya kwa uume.
6.Kuwepo kwa maradhi katka mfumo wa uzazi wa kike. Matatizo haya ya kiafya yanaweza kuwa kwenye ovari, ama kukawa na uvimbe ndani ya kizazi ama kukawa na shida katika mirija ya uretas.
7.Kufanyiwa baadhi ya matibabu katika maeneo ya siri. Kwa mfano baadhi ya matibabu ya saratani katika sehemu za siri, matibabu haya yanaweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa
8.Matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawaso. Wakati mwingine uoga, kuwa na msongo wa mawazo ama kukumbuka maumivu uliyoyappata siku zanyuma, hali hizi zinaweza kupelekea maumivu wakati mwingine.
9.Staili iliyotumika wakati wa kufanya sex. Wakati mwingine mikao ya kufanya tendo la ndoa inaweza kuwa ni sababu ya maumivu. Ni vyema kutumia mikao iliyo rahisi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 web hosting 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 ai web app 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Sababu za kupasuka kwa mfuko wa kizazi
Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.
Soma Zaidi...Kuwepo kwa maziwa wakati wa ujauzito.
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.
Soma Zaidi...Unaweza kuhisi chochote ktk tumbo ukiwa na wiki mbili? Na je ukibonyeza tumbo utahisi chochote ukiwa ns wiki
Ni mida gani njamzito ananza kuhisi kuwa tumboni anebeba mtoto.
Soma Zaidi...Nguzo kuu za umama katika umri wa kupata watoto na kulea watoto
Posti hii inahusu zaidi nguzo kuu za umama katika umri wa kujifungua na kulea watoto, ni kipindi ambacho mama anakuwa analea watoto kwa kawaida kadri ya makadirio kipindi hiki uanza kati ya miaka kumi na mitano mpaka arobaini kwa walio wengi na kinaweza k
Soma Zaidi...Mbinu za kuwakinga watoto na saratani.
Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo tunaweza kuzitumia ili kuwakinga watoto dhidi ya saratani, kama tulivyotangulia kusema kwamba saratani ya watoto mara nyingi Usababishwa na akina Mama hasa kwa sababu ya mtindo wa maisha wakati wa ujauzito kwa hiyo tun
Soma Zaidi...Mambo ya kuzingatia iwapo mimba imetoka.
Post hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia iwapo mimba imetoka mambo haya yanaweza yakawahusu akina Mama wenyewe, familia na jamii kwa ujumla.
Soma Zaidi...