Dalili za HIV na UKIMWI kwenye Ulimi na Mdomo
Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi utaziomna hapa. hizi zinaweza kuwa ndio za kwanza kwa ambaye hajapima HIV

DALILI ZA UKIMWI NA HIV KWENYE ULIMU NA MDOMO
HIV hivi ni virusi vilivyopata umaarufu sana kwa kufahamika kuwa ndio virusi pekee vinavyoweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini yaani UKIMWI. Virusi hivi anaweza kuvipata binadamu yeyote yule. Zipo njia nyingi ambazo unaweza kupata virusi hivi kama kushiriki ngono zembe, kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kijifungua, kushiriki vitu vyenye ncha kali, kupewa damu yenye virusi, na njia nyingine kibao. Dalili za HIV na UKIMWI zinatofautiana kulingana na hatua ya mgonjwa. Lanini kuna wakati Ulimi na Mdomo kuweza kuonyesha dalili hizi wazi wazi.
Dalili za HIV na UKIMWI kupitia mdomoni zinaweza kuwa ni dalili za mwanzoni sana za UKIMWI kwa baadhi ya watu. Ukweli ni kuwa dalili hizi zinaweza kumpata yeyote lakini kuna watu wapo hatarini zaidi kama watoto wachanga, wazee na watu wenye upungufu wa kinga yaani UKIMWI. Dalili hizi tutaziona moja hadi nyingine hapo chini.
Dalili za HIV na UKIMWI kwenye mdomo na ulimi
1.Kukauka kwa mdomo na kuoza kwa meno.
Virusi vya HIV vinaweza kupelekea mdomo kukauka na kukosa mate ya kutosha. Hivyo miongoni mwa kazi za mate ni kulinda meno na mdomo. Hivyo kupelekea meno kuoza. Ni vyema mgonjwa kama anatatizo hili kuonana na daktari aweze kumpa ushauri. Unaweza kutumia dawa maalumu kwa ajili ya kuchochea mate ama kutafuna bigji ambazo hazina sukari.
2.Kupata fangasi wa kwenye mdomo wajulikanao kama candidiasis (thrush).
Fangasi hawa wanaweza kusababisha madoa mekundu kwenye ulimi, ama mdoa meupe kwenye mdomo. Pia wanaweza kusababisha kupasuka kwa kona za mdomo na kutengeneza weupe kwenye kona za mdomo. Pia mdomoni kunaweza kuta buda la nyama lisilokuwa na maumivu. Fangasi hawa wanaweza kuhamia kwenye koo na kusababisha maumivu. Fangasi hawa ni rahisi sana kuondoka baada ya matibabu ila kwa baadhi ya sababu wanaweza kuwa sugu.
3.Vidonda kwenye mdomo na ulimi
Hivi ni vijidonda vijidogo ambavyo vipo duara. Vinaweza kutokea kwenye ulimi na kwenye mashavu kwa ndani. Pia vinaweza kutokea nyuma ya koo. Vidonda hivi vinakuwa na rangi nyekunu pembeni na rangi ya kijivu katikati. Misongo ya mawzo na baadhi ya vyakula vinaweza kuwa ni sababu.
4.Vidonda vya homa.
Kama umeshawahi kushuhudia vidonda ambavyo vinatokana na homa. Vidonda hivi kwa watu wenye UKIMWI vina tabia ya kujirudia mara kwa mara. Dawa za ART huweza kusaidia hali hii kutotokea.
5.Maradhi ya ufinzi ama periodontitis or gingivitis
Haya ni maradhi ya ufizi ambapo ufinzi unakosa nguvu na kushindwa kuzuia meno vyema. Hal hii inaweza kupelekea kung’oka kwa meno. Hali hii inaweza tokea mapema sana miezi 18 baada ya kupata HIV. Ukavu kwenye mdomo, kuvuta sigara kunaweza kufanya hali kuwa mbaya zaidi.
6.Kuota kwa kambakamba ama vinywele vinywele kwenye ulimi na pembeni ya ulimi.
Kitaalamu hivi hujulikana kama Hairy Leukoplakia. Vikambakamba ama vinyweleo nyweleo hivi havina maumivu lakini pia haviwezi kutoka hata kwa kupiga mswaki. Hii inaweza kuwa ni katika dalili za mwanzo zaidi za UKIMWI. Vyenyewe vipo na rangi nyeupe
7.Madoa ya rangi ya dhambarau iliyowiva ama nyekundu kwenye mafinzi, sehemu ya juu ya mdomo na nyuma ya ulimi. Kitaalamu hufahamika kama Kaposi’s Sarcoma (KS Hii inaweza kuwa ni dalili ya kwanza kwa mtu ambaye hajapima HIV. Na kwa ambaye ameshaanza kutumia dawa dalili hizi ni si rahisi kujionyesha.
8.Kuota chunjua kwenye mdomo,na ulimi. Hizi husababishwa na virusi vinavyojulikana kama Human Papillomavirus, HPV. Kikawaida chunjua inaweza kuota popote pale kwenye mwili hasa hasa hutokea mara nyingi kwenye mikono. Watu wenye HIV chunjia hizi huweza kuvamia ulimi na kuhama maeneo mengine kwenye mdomo. Pia baadhi ya virusi wanao;eta hali hii wanaweza kusababisha saratani.
Mwisho nikufahamishe tu kuwa mdomo ni katika sehemu za kwanza kuonyesha dalili za HIV na UKIMWI. Ni vyema kwenda kupima endapo utagundua una moja ya dalili hizo hapo juu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 web hosting 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 ai web app 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Dalili za ugonjwa wa macho.
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa macho, ugonjwa huu kwa kawaida una dalili kuu tano kadri ya maambukizi yanavyoongezeka na madhara yake kwa hiyo tunapaswa kujua dalili hizo Kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za maambukizi ya sikio kwa watoto.
Soma Zaidi...Fahamu Ugonjwa unaosababisha madhara kwenye mapafu
Posti hii inaelezea kuhusiana na Magonjwa yanayosababisha madhara kwenye mapafu na kitaalamu hujulikana Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu
Soma Zaidi...Dalili za kuvimbiwa kwa watoto.
Kuvimbiwa kwa watoto ni shida ya kawaida. Kuvimbiwa kwa watoto mara nyingi huonyeshwa na kinyesi kisicho kawaida au kinyesi ngumu na kavu.
Soma Zaidi...Dalili za kuvunjika kwa nyonga
Kuvunjika kwa nyonga ni jeraha kubwa, na matatizo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha. Hatari ya kupasuka kwa nyonga huongezeka na umri.
Soma Zaidi...