picha

Dalili za uti kwa wanaume na wanawake

tambuwa chanzo na dalili za UTI na tiba yake, pamoja na njia za kupambana na UTI

Dalili za uti kwa wanaume na wanawake

UGONJWA WA UTI
Ugonjwa wa UTI ni kifupisho cha Urinary Track infections. Haya ni maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo. Mashambulizi haya kwa kiasi kikubwa husababishwa na bakteria aina ya E.Coil. Bakteria hawa huishi kwenye utumbo (gastrointestinal track). Pia UTI inaweza kusababishwa na fangasi na virusi kwa kiasi kidogo sana. UTI inasumbuwa sana watu, inakadiriwa kuwa kati ya kila watu watano mmoja ana UTI. Wanawake wapo hatarini zaidi kupata UTI kuiko wanaume



UTI inaambukizwa vipi?
Maambukizi mengi ya UTI yana tokea choon wakati wa kujisafisha. Bakteria hawa wanatoka kwenye utumbo kuja nje kupitia haja kubwa. Sasa ikitokea mtu amejisafisha vibaya anaweza kuwachukuwa bakteria hawa na kuwapa njia kuingia kwenye njia ya mkojo na kusababisha mashambulizi. Pia wakati wa kushiriki tendo la ndoa (ngono). hii inaweza kusababisha UTI kuhama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Pia kushirikiana vifaa vya ngono, kutumia vifaa vya uzazi wa mpango na njia nyinginezo.



Dalili za UTI
1.Kukojoa mara kwa mara
2.Kuhisi kuunguwa ama umoto wakati wa kukojoa
3.Kutoa mikojo kwa uchache
4.Mkojo kuwa mchafu, kama mawingu ama mwekundu uliopauka
5.Harufu kali ya mkojo
6.Maumivu ya kwenye njonga kwa wanawake
7.Maumivu ya mkundu na puru kwa wanaume.



Dalili za UTI zinaweza pia kuwa tofauti na hizo hapo juu. Dalili hizi hutofautiana kwa kulingana na aina ya UTI. Kama unataka kuzijuwa dalili zaidi za UTI endelea kusoma makala hii mpaka mwisho.



Aina za UTI na dalili zake.
Ugonjwa wa UTI umegawanyika katika makundi mbalimbali. Makundi hayo ni kama:-
1.UTI ya kwenye figo (acute pyelonephritis). UTI hii huathiri figo, na kusababisha dalili kama:-
1.Maumivu ya mgongo kwa juu
2.Homa kali
3.Kuhisi baridi na kutetemeka
4.Kichefuchefu
5.Kutapika.



2.UTI ya kwenye kibofu (cystitis). hii ni aina ya UTI ambayo huathiri kibofu cha mkojo. Dalili zake ni:-
1.Maumivu ya nyonga
2.Maumivu ya tumbo kwa chini ya kitovu ama mvurugiko wa tumbo kwa chini
3.Kukojoa mara kwa mara huku ukiwa na maumivu.
4.Kukojoa damu, ama mkojo wenye rangi nyekundu ya kupauka.



3.UTI ya kwenye mrija wa mkojo (urethritis). mrija wa mkojo kitaalamu unaitwa urethra. Huu ndio mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu na kuuleta nje. Dalili za UTI hii ni kuhisi kuunguwa wakati wa kukojoa.



Dalili za UTI kwa upande wa wanawake.
Kwa upande wa wanawake dalili za UTI zinaweza kuwa zaidi ya tulizotaja hapo juu. Kwa wanawake UTI inaweza kuathiri mfumo mzima wa uzazi kwa mwanmke. Kwa mfano mwanamke anaweza kupata dalili za mimba kumbe ni UTI. Kuvimba kwa matiti, kuuma kwa tumbo, kubadilika hedhi, kukojoa mara kwa mara. Kwa ufupi kwa wanawake uti inaweza kusumbuwa sana kwani inadhaniwa ni maradhi mengine.



Dalili za UTI kwa wanaume.
Kwa wanaume dalili za UTI ni kama ambazo tumetangulia kuzitaja hapo juu. Kwa wanaume hawana dalili maalumu kama wanawake. Hata hivyo maumivu ya kwenye puru na mkundu hutokea kwa wanaume na si kwa wanawake.



Watu hawa wapo hatarini kupatwa na UTI.



1.Kuwa mwanamke. Wanawake wapo hatarini kwa sababu ya maumbile yao. Njia yao ya mkojo ipo karibu sana na njia ya hajakubwa. Hata hivyo njia yao ya mkojo ni fupi kukifikia kibofu kuliko wanaume.
2.Kuwa ni mwenye kushiriki ngoni.
3.Kama unatumia baadhi ya njia za uzazi wa mpango kama spermicidal agent
4.Kama mwanamke hapati tena hedhi, yaani amefikia kikomo cha kupata hedhi
5.Kama una matatizo kwenye mfumo wa mkojo.
6.Kama njia ya mkojo imeziba kwa mfano kama unavijiwe kwenye figo na vikaziba njia ya mkojo.
7.Kama unatumia matibabu ya kuongezea kinga ya mwili nguvu kama vile wenye kisukari
8.Kama unatumia mpira wa kukojolea.



NJIA ZA KUJILINDA NA KUIJIKINGA NA UTI
1.Kunjwa maji mengi sana
2.Nenda ukakojoe punde baada ya kufanya ngono
3.Kwa mwanamke jisafishe kuelekea nyuima na si kutokea nyuma kuelekea mbele
4.Safisha vyema choo baada ya kujisaidia
5.Nenda ukakojpoa punde tu unapohisi unataka kukojoa
6.Vaa nguo za ndani zilizo kavu na zisizo bana.
7.Jisafishe vyema sehemu za siri kabla na baada ya kufanya ngono.





                   



Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 5496

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 ai web app     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Chanzo cha VVU na UKIMWI

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyanzo m ali mbali vinavyohisiwa kuwa chanzo cha UKIMWI

Soma Zaidi...
Dalili za madhara ya figo

Posti hii inahusu dalili za figo.figo husawazisha maji mwilini pamoja na kuchuja mkojo.

Soma Zaidi...
Dalili za presha ya kushuka

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za presha ya kushuka

Soma Zaidi...
Dalili za malaria

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na mdudu kwa kitaalamu anaitwa Anopheles.na anasambazwa na mbu jike pale anapotafuta chakula hasa wakati akiwa na mimba. Mbu hawa hupenda kuishi kwenye mnyasi, madibwi haswa kwenye maji yaliyo simama.

Soma Zaidi...
Namna ya kugundua mtu mwenye kaswende.

Post hii inahusu zaidi njia za kumgundua mgonjwa wa kaswende, njia hizi utumika baada ya kuongea na mgonjwa kuhusu maisha yake hasa kujamiiana na watu mbalimbali.

Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo

Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo, hizi ni njia ambazo zinapaswa kufuatwa ili kutokomeza kabisa maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.

Soma Zaidi...