Vyakula vya madini kwa wingi, na kazi za madini mwilini

Utajifunza vyakula vyenye madini kwa wingi, kazi za madini mwilini na athari za upungufu wake

Vyakula vya madini kwa wingi, na kazi za madini mwilini

VYAKULA VYA MADINI KWA WINGI
Madini ni katika virutubisho ambavyo huhitajika katika kuhakikisha kuwa mwili unabakia kati aafya njema.mwili unahitaji madini kwa ajili ya kuimarisha afya ya moyo, mishia, misuli na maeneo mengine ya mwili. Madini tunaweza kuyapata kutoka kwenye vyakula tunavyokula kama mboga za majani, nyama, matunda na nafaka zingine. Je ungependa kujuwa vyakula hivyo ama vyanzo vya madini? Na je ungependa kujuwa ni zipi hasa kazi za madini katika miili yetu?. makala hii ni kwa ajili yako, hapa utakwenda kujifunza mengi kuhusu somo hili.



Kabla ya kuona vyakula hivyo kwanza ningepata kukujuza kazi kuu za virutubisho vya madini kwenye miili yetu. Madini yamegawanyika katika aina kuu mbili kuna ambayo yanahitajika kwa wingi katika miili yetu na kuna ambayo yanahitajika kwa kiasi kidogo. Kwa ujumla madini yana kazi kuu zifuatazo:-



KAZI ZA MADINI MWILINI
1. Madini hutumika kwa ajili ya kudhibiti kiwango cha majimaji kwenye mwili kama madini ya sodium au chumvi


2. Huhitajika madini kwa ajili ya utengenezwaji wa asidi mbalimbali kama asidi ya hydrocloric kama madini ya chloride na phpsphprus


3. Husaidia katika kudhibiti kiwangi cha uzalishaji wa tindikali mwilini kama tindikali ya hydrocloric kama madini ya chloride


4. Husaidia katika usafirishwaji wa taarifa kutoka sehemu moja ya mwili kwenda sehemu nyingine kama madini ya sodium na potassium


5. Husaidia katika ujongeaji wa mishipa kama madini ya sodium na cailcium


6. Madini huhitajika kwa ajili ya kuimarisha afya ya mifupa, misuli, mishipa, meno na moyo kama madini ya calcium na magnesium


7. Huhitajika madini kwa ajili ya kuganda kwa damu maeneo yenye majeraha kama madini ya calcium na phosphorus


8. Huhitajika madini kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa kinga mwilini kama madini ya calcium


9. Huhitajika katika utengenezwaji wa hemoglobin chembechembe nyekundu za damu kama madini ya chuma


10. Huhitajika katika kutengeneza protini na genetics material, huhitajika katika utengenezwaji wa manii na ni muhimu katika mfumo wa uzalishaji kwa mfano madini ya zinc



VYAKULA VYENYE MADINI KWA WINGI
Kwa kuwa umesha jifunza kazi za madini zilizotajwa hapo juu, basi tambuwa kuwa kuna aina nyingi za madini ambazo baadhi yake zimetajwa hapo juu. Madini haya unaweza kuyapata kwenye mchanganyiko wa vyakula vingi. Lakini kuna vyakula ambavyo madini huwa ni mengi kuliko vyakula vingine. Hapa chini ninakuletea vyakula ambavyo vina madini kwa wingi ambavyo ni:-



1. Kwenye mbegu kama mbegu za maboga. Mbegu za maboga zina madini mengi sana. Unaweza kula mbegu za maboga kwa kutafuna, kutumia unga wake kama kiungo cha mboga ama kukaanga na kula kama bisi. Mbegu za maboga na m,begu nyingine zenye mfano wake kama mbegu za matango zina madini kama magnesium, zinc, manganese, copper, selenium, na madini ya phosphorus.



2. Kwenye samaki hasa samaki wenye magamba magumu kama kobe (shellfish) jamii ya tondo. Kama umeshawahi kula tondo, utakuwa unaelewa nini klimaamnishwa.kama hutambui nitakujuza. Angalia mfano wa konokono, basi samaki wenye kufanana na konokono wanatembea na majumba yao, ukimshituwa anaingia ndani. Samaki hawa ndio wanaozungumziwa hapa. Samaki hawa wana madini kama selenium, zinc, copper na chuma



3. Mboga za majani jamii ya kabichi. Mboga hizi zina madini kama magnesium, potassium, manganese na calcium



4. Kwenye nyama hasa nyama za viungo maalumu kama maini na figo. Nyama hizi zina madini kama selenium, zinc, madini ya chuma, na phosphorus.



5. Mayai ni moja kati ya vyakula vyema virutubisho vingi sana. Katika mayai kuna madini ya chuma kwa wingi sana, phosphorus, zinc na selenium.



6. Maharagwe, maharage ya na madini kama cailcium, magnesium, madini ya chuma, phosphorus,potassium, madini ya shaba na zinc.



7. Palachichi, tunda hili lina madini kama magnesium, potasium, manganese na madini ya shaba.



8. Maziwa yana madini kama cailcium, potassium, phosphorus, zinc na selenium.



9. Viazi mbatat vina madii kama potassium, magnesium, manganese, calcium, madini ya chuma na madini ya shaba.



10. Pia madini kama potassium, manganese, shamba na magnesium tunaweza kuyapata kwenye matunda kama, ndizi, fenesi, machungwa, pasheni, nanasi na mapera.



ORODHA YA MADINI NA CHANZO CHAKE NA FAIDA ZAKE.
Kwa ufupi ninakuletea orodha ya madini mablimbali na vyakula ambavyo hupatikana. Pia utajifunza kazi za kila aina ya dini ndani ya miili yetu.

1. Madini ya sodium (table salt) Madini haya unaweza kuyapata kwenye spinach, maharage,punje za maboga n.k.



2.Madini ya chuma. Haya hupatikana kwenye maini, nyama, maharage, na mboga za majani. Madini haya ni muhimu kwa utengenezwaji wa hemoglobin yaani chembechembe nyekundu za damu.


3.Madini ya kashiam(calcium). Haya hupatikana kwenye maziwa,maini, mboga za majani na cheese. Madini haya husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno, misuli na utengenezwaji wa neva. Husaidia piaa kuwezesha kuganda kwa damu kwenye majeraha. Husaidia katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa kuzifanya enzymes kuwa active.



4. Madini ya phosphorus, haya hupatikana kwenye nyama, maziwa, samaki, na mayai. Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.



5. Madini ya Potashiam (potassium) Hupatikana kwenye ndizi, machungwa,nyama na kaa. husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini.



6.Madini yakopa ( copper) Haya hupatikana kwenye nyama, samaki, na maini.husaidia katika mifupa na utengenezwaji wa hemoglobin (chembechembe nyekundu za damu).



7.Madini yamanganese Madini haya hupatikana kwenye figo,maini, chai na kahawa. Husaidia katika utengenezwaji wa mifupa, na katika mmeng'enyo wa chakula kwa kufanya enzymes ziwe active.



8.Madini ya iodine Madini haya hupatikana kwenye chumvi na vyakula vya baharini kama samaki. Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid.






                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 717

Post zifazofanana:-

Sifa za wanafiki zilizotaja katika surat An-Nisaa (4:60-63, 88, 138-145)
Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako? Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG'ATWA NA NYOKA
Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu. Soma Zaidi...

Ijuwe Dua ya Ayyuub(a.s)
Nabii Ayyuub(a. Soma Zaidi...

KUAMINI MALAIKA
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

SABABU ZA KUKOSA HAMU YA TENDO LANDOA
Hii ni hali inayompata mtu kukosa hamu kabisa ya kushiriki kitendo chochote kinachohusiana na kufanya tendo landoa au bunyeto. Soma Zaidi...

Sababu za kuharibika kwa ujauzito na dalili zake
Dalili za kuharibika kwa ujauzito na dalili za kuharibika kwa ujauzo Soma Zaidi...

KISUKARI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Kutuma sms ndefu
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Ndoa ya mke zaidi ya mmoja katika uislamu na taratibu zake, faida zake na namna ya kuitekeleza
- Je, Ukeweza, (ndoa ya mke zaidi ya mmoja) humdhalilisha mwanamke? Soma Zaidi...

Sifa za uchumi wa kiislamu na njia halali za uchumi na umiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...

Hadithi aliyoisimulia Kijakazi kwa sultan
Soma Zaidi...

Kisa cha Israa na Miraji na kufaradhishwa swala tano
Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B. Soma Zaidi...