VYAKULA VYENYE PROTINI KWA WINGI

hivi ndio vyakula vya protini kwa wingi, maziwa, mayai, samaki, dagaa, nyama, maini. Endelea na zaidi

VYAKULA VYENYE PROTINI KWA WINGI



VYAKULA VYENYE PROTINI KWA WINGI



Tunaweza kupata protini kwenye mimea jamii ya mikunde kama kunde na maharagwe. Pia kiasi kikubwa cha protini tunaweza kukipata kwa kula mayai, nyama, samaki, dagaa na maziwa. Pia tunaweza kupata protini kwa kula nafaka kama mchele na nafaka zingine. Ulaji wa mboga za majani unaweza pia kutupatia protini kwa kiasi kidogo. Wadudu kama kukbikukbi, senene na wengineo pia wanaweza kutupatia protini.


Kwa kifupi vyakula vinavyotupatia protini ni pamoja na :-


1.Samaki; samaki ni chanzo kizuri cha protini. Samaki wenye mafuta kama salmon ni vyanzo vyema zaidi vya protini. Ulaji wa samaki umekuwa ni chanzo kizuri cha protini hasa kwa wakazi wa maeneo ya baharini na maeneo ya pwani ama mitoni, mabwawa na maziwa. Tunaposema samaki hapa wanaingia mpaka dagaa, kaa, kaji, kamongo, perege, mikunga, papa na samaki wengine. Pia ulaji wa samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo, kukinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali, chanzo cha madini ya chumvi na fati


2.Mayai; mayai ni katika vyanzo vikubwa vya protini. Karibia watu wengi hujipatia protini kwa kula mayai. Unaweza kula yai likiwa limekaangwa, chemshwa ana la kuchoma. Pia unaweza kula yai bichi kama wafanyavyo baadhi ya watu. Ulaji wowote kati ya niliotaja unaweza kukupatia protini. Ila hakikisha kama umelikaanga ama kulichoma halikauki sana likawa kama chapati iliyokauka, upishi huu unaweza kuathiri virutubisho.


.3. Maziwa; maziwa ni katika vyanzo vikuu vya protini kwa binadamu na wanyama. Maziwa ya mama ni chanzo kipekee kilicho salama zaidi kwa mtoto mchanga kuliko hata ya ng'ombe. Tofauti na kutupatia protini maziwa pia ni chanzo cha vitamini na fati. Maziwa ni katika vyakula vilivyokusanya viinilishe vyote muhimu. Ni vyema kuyachemshha maziwa kabla ya kuyanywa ili kuepuka baaadhi ya matatizo ya kiafya.


4.Nyama; tunaweza kupata protini kwa kiasi kikubwa kwa kula nyama. Nyama ni katika vyanzo vizuri vya protini. Inaweza kuwa nyama nyekundu ama nyama nyeupe. Nyama nyeupe tunaweza kuzipata kwa kula kuku, baadhi ya samaki, kaa. Nyama nyekundu tunaweza kupata kwa kula mbuzi, kondoo na karibia wanyama wengi. Nyama pia ni chanzo kizuri cha fati mwilini. Ulaji wa nyama unaweza kuleta athari za protini kwa muda mchache sana.


5.Mimea aina ya kunde na nafaka; mimea jamii ya kunde hii ni mimea ambayo inatambaa kama kunnde na maharagwe na mimea jamii hii. Mimea hii inatambulika kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Watu wenye kipato cha chini mimea hii ni chanzo chao cha msingi cha kupata protini. Maharagwe yapo katika aina nyingi yapo ya soya na aina mbalimbali. Ulaji wa aina zote hizi unaweza kutupatia protini.


6.Mboga za majani. Kwa kiwango kilicho kidogo tunaweza kupata protini kwa kula mboga za majani. Mboga za majani oekee hazitoshelezi kutupatia kiwango cha protini kinachohitajika. Kwa wale ambao hawali chama (vegetarian) wapo ambao hawali nyama lakini wanakula mayai na maziwa hawa wanaweza kujipati protini kwenye mayai na maziwa. Lakini kwa wale ambao hawali nyama, maziwa wala mayai watahitajika kupata vyamzo vingine mbadala vya protini yaani watumie protini za kutengeneza japo miongoni mwazo zipia mbazo zinatengenezwa kwa wanyama.


7.Vyanzo vingune: tofauti na vyanzo vya protini nilivyotaja hapo juu lakini pia kuna vyanzo vingine kama ulaji wa senene na kumbikumbi na wanaofanana. Kuna baadhi ya jamii zinakula senene hasa jamii zinazopatikana maeneo ya kagera. Kwao senen ni chanzo kizuri sana cha protini. Kumbikumbi nao hupatikana maeneo mengi na jamii nyingi zinatumia chakula hiki.




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1794

Post zifazofanana:-

nikiamka asubuhi huwa nakojoa mkojo mchafu sana halafu najiskia vibaya Sana na mwili wote unaniuma je tatizo litakua ni nin
Soma Zaidi...

WAJUE FANGASI, AINA ZAKE, DALILI ZAKE NA MATIBABU YAKE
Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Soma Zaidi...

Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...

INTRODUCTION TO CHEMISTRY FOR SECONDARY SCHOOL
Learn chemisty for secondary schoo o-level Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za mwanamke katika jamii za Kirumi hapo zamani
(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu. Soma Zaidi...

SIRI
Baada ya kutulia vizuri unaanza kukumbuka umefikaje hapa kwenye misitu. Soma Zaidi...

DARSA ZA QURAN
Soma Zaidi...

'Allah (s.w) humwingiza katika rahma zake amtakaye na kumwacha kupotea amtakaye'
Soma Zaidi...

Masomo ya Afya kwa kiswahili
Makala za afya zilizopata kusomwa zaidi kutoka bongoclass kitengo cha afya Soma Zaidi...

Fahamau protini na kazi zake, vyakula vya protini, na athari za upungufu wake.
unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo Soma Zaidi...

Siku ya Taqwiya na kusimama Arafa
5. Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...