picha

Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba

Mtume (s.

Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba

Mkataba wa 'Aqabah na vipiengele vyake na mafunzo tunayoyapata katika mkataba wa aqaba

Mtume (s.a.w) alivyoandaa Ummah wa Kiislamu Makkah.
- Mtume (s.a.w) alitumia kila aina ya fursa iliyopatikana katika kuufikisha
ujumbe Uislamu kwa watu wengine.



- Mtume (s.a.w) alifikisha ujumbe wa Uislamu kwa watu na makabila mbali
mbali kwa siri na dhahiri kutokana na uadui wa Maquraish dhidi yake.



- Mtume (s.a.w) alitumia mikataba kwa kuandaa ummah wa kiislamu kutoka
sehemu mbali mbali hasa mji wa Madinah (Yathrib) kama ifuatavyo;




Mikataba ya ‘Aqabah.
- Hii ilikuwa ni baina ya Mtume (s.a.w) na watu wanaotoka nje ya mji wa
Makkah hasa waliokuja kuhiji msimu wa Hija.



- Mtume (s.a.w) alikutana na kikosi cha kwanza kabisa cha watu sita (6)
kutoka Madinah (Yathrib) wa kabila la Khazraj, baada ya kuwafikishia
ujumbe wa Uislamu, walisilimu na wakaahidi kuufikisha kwao Madina.



- Mwaka uliofuata, 621 A.D, kikundi kingine cha waislamu 12 (2 Aus na
10 Khazraj) walikutana na Mtume (s.a.w) kwa siri eneo la ‘Jaratul
‘Aqabah’ na kuweka mkataba wa kwanza wa ‘Aqaba na kukubaliana
yafuatatayo;


i.Hawataabudu chochote isipokuwa Allah (s.w) pekee.
ii.Hawataiba wala hawatapokonya misafara ya biashara njiani.
iii.Hawatazini.
iv.Hawatawaua watoto wao tena.
v.Hawatasema uongo wala hawatawasingizia wengine uovu.


vi.Hawatamuasi Mtume kwa kila atakalowaamrisha na watakuwa waaminifu kwake kwa hali yeyote iwayo.

- Mtume (s.a.w) aliwapa mwalimu wa kuwafundisha Uislamu, ‘Mus’ab bin
Umair.
- Mwaka uliofuata, 622 A.D.walimjia Mtume (s.a.w) waislamu 75
(wanawake 2) wakiongozwa na mwalimu wao, ‘Mus’ab na kufunga
Mkataba wa pili wa ‘Aqabah sehemu ile ile kwa kukubaliana kuwa;



oMtume na Waislamu wote wa Makka wahamie Madinah (Yathrib) na wao watawapokea na kuwahifadhi dhidi ya maadui wao.

- Mtume (s.a.w) aliwachagulia viongozi 12 (9 Khazraj na 3 Aus) na watu
watakaokuwa chini ya kila kiongozi, na wanaume wote walimpa Mtume
(s.a.w) mkono wa bai’at kwa maana ya utii wao kwake.



- Baada ya kikundi hicho kurejea na kufika Madinah salama, ndipo Mtume
(s.a.w) aliwatangazia waislamu wote wa Makkah kuhamia Madinah.



- Na takriban baada ya miezi miwili hivi, Waislamu wote wenye uwezo wa
kuhama walishahamia Yathrib (Madinah) kwenda kujiimarisha zaidi.



Mafunzo yatokanayo na Mikataba ya ‘Aqabah katika kuandaa ummah.
i.Waislamu hawana budi kupanga mikakati na mambo yao kwa siri ili kutojulikana na maadui wa Uislamu na waislamu.



ii.Waislamu hawanabudi kutotangaza mikakati yao kwa maadui kabla ya kuitekeleza ili kuepukana na njama ya kukwamishwa.



iii.Waislamu hawanabudi kuwa na mipango na mikakati (long and short term strategies) ya muda mrefu na mfupi katika kuandaa Ummah.



iv.Uongozi bora na makini ni jambo la msingi sana la mwanzo katika kuusimamisha na kuuendeleza Uislamu katika jamii.



v.Waislamu wanaharakati wanapoazimia jambo lolote katika kuusimamisha na kuuendeleza Uislamu, hawana budi kujifunga nalo na kupeana kiapo cha utekelezaji.



vi.Waislamu hawana budi kutumia kila aina ya fursa itakayojitokeza katika kuusimamisha na kuuendeleza Uislamu katika jamii.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views 3456

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

tarekh

MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU).

Soma Zaidi...
Nabii Isa(a.s) Azungumza Akiwa Mtoto Mchanga

Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba.

Soma Zaidi...
Nasaba ya Mtume Muhammad S.A.W na familia yake.

Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 1

Soma Zaidi...
Kwanini mwanadamu hawezi kuunda dini sahihi

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...