Juhudi za Waislamu Katika Kuhuisha Harakati za Kiislamu Zama za Nyerere hadi leo

i. Wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere waislamu walianzisha Taasisi na Jumuiya mbali mbali za Kiislamu kama vile; Baraza Kuu la Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, African Muslim Agency, Al-Haramain, Islamic Foundation, Islamic Propagation Centre (IPC), Munadhwamat Da’awah, n.k.
ii. Taasisi mbali mbali za Kiislamu kati ya miaka ya 1989 hadi 1992 zilianzisha mashule kama vile; Mudio Islamic Seminaries, Ubungo Islamic High School, Kirinjiko Islamic High School, Kunduchi na Ununio Secondary Schools na zinginezo.
iii. Kulianzishwa vyuo vya Ualimu vya Kiislamu kwa ngazi za cheti na stashahada kama vile; Al-Haramain Islamic Teachers’ College - 1987, Ubungo Teachers’ College - 1998, Kirinjiko Teachers’ College - 2004 na vinginevyo vilivyojitokeza baadae.
iv. Mwaka 2005, Taasisi ya Muslim Development Foundation (MDF) ilianzisha Chuo Kikuu Cha Waislamu Morogoro, Muslim University of Morogoro (MUM) kama chuo pekee kikombozi kwa jamii ya waislamu Tanzania.v. Hadi leo hii, Taasisi na shule nyingi za Kiislamu za chekechea, msingi na sekondari pamoja na vyuo zinaendelea kuibuka, nyingi zikiwa na lengo la kutoa elimu Sahihi ya Mwongozo na ya Mazingira kama nyenzo pekee ya kusimamisha Uislamu katika jamii.