Uendeshaji na Kupanuka kwa Dola ya Kiislamu Kipindi cha Makhalifa Waongofu

a) Wajibu wa Khalifa kama kiongozi wa Dola

i. Kujenga maisha ya binaadamu katika misingi ya Ucha – Mungu na matendo mema.
Rejea Qur’an (57:25)

ii. Kutumia uchumi wa Dola katika kukuza na kuendeleza maadili ya raia wake.
iii. Kuamrisha mema na kukataza mabaya katika jamii kupitia njia zifuatazo;

- Kuteua Makadhi wacha – Mungu na waadilifu kwa kusimamia sheria.

- Kuteua Madai’yah (walimu) wa kufundisha mambo muhimu ya dini na maisha kwa ujumla.
- Khutba za Ijumaa na Sikukuu za Eid zilitumika kuelimisha waumini.

- Kuteua tume (jopo) la watu kwa ajili ya kufuatilia tabia na mienendo ya watu na kutoa adhabu.


iv. Kulinda mipaka ya Dola kwa gharama yeyote, kwa vita au diplomasia.

v. Kuteua viongozi wa ngazi mbali mbali kwa kushirikiana na Shura yake ya watu maalum.
vi. Khalifa ndiye mkuu wa majeshi na ndiye amir – jeshi anayeamua vita ipiganwe au isipiganwe kwa kushirikiana na watu wa shura.
vii. Khalifa pia ndiye mwanasheria mkuu wa Dola ya Kiislamu, anayesikiliza kesi na kutoa hukumu.
b) Mgawanyo wa viongozi wengine waandamizi wa Dola na Majukumu

- Vyombo vikuu vya utendaji katika kuendesha Dola ni pamoja na;

1. Kamati kuu ya utendaji

2. Shura ya waumini (watu) wote

3. Tume ya kufuatilia malalamiko ya raia.- Dola iligawanywa katika majimbo na wilaya na kuwa na viongozi wafuatao;

1 Walii – Gavana,

2 Amil – mkusanyaji wa mapato ya Dola

3 Kadhi – jaji kwa ajili ya kusimamia sheria na kutoa hukumu.c) Vyanzo vya Mapato na Uchumi wa Dola ya Kiislamu

Zifuatazo ni miongoni mwa vyanzo vya uchumi wa Dola ya Kiislamu:

i. Zaka na Sadaka ndio ilikuwa njia kuu ya kukusanya mapato ya serikali

(Dola) ya Kiislamu iliyowahusu waislamu wote wenye uwezo.ii. Jizya – Ni kodi waliokuwa wanalipa wasiokuwa waislamu wanaume tu wenye uwezo wa kuwa askari kwa ajili ya ulinzi wa Dola.


iii. Al-Kharaj – Ni kodi waliolipa wasiokuwa waislamu, walio na mashamba katika Dola ya Kiislamu.


iv. Al-fay – Ni mapato yanayotokana na mashamba ya Serikali (Dola) ya

Kiislamu Madinah.v. Al-Ghanimah (Ngawira) – Ni mapato yanayotokana na mali ilitekwa katika vita, iliyolipwa 1/5 ya mali yote ilyotekwa.


vi. Ushr – Ni kodi (ushuru) iliyotolewa na waislamu wenye ardhi katika Serikali (Dola) ya Kiislamu kwa kiwango cha 10% kwa maji ya asili (mvua) na 5% kwa maji ya kumwagilia.


vii. Zaraib – Ilikuwa ni kodi zilizotozwa na serikali (Dola) ya Kiislamu kwa muda kwa ajili ya maslahi ya nchi.
d) Ulinzi na usalama wa Dola ya Kiislamu wakati wa Makhalifa

- Wakati wa Ukhalifa ulinzi na usalama uliimarishwa kwa kiwango kikubwa.

- Kinyume na wakati wa Mtume (s.a.w) hapakuwa na jeshi maalum la ulinzi na usalama wa Dola, bali kila muislamu mwanamume alikuwa askari.
- Wakati wa Makhalifa pamoja na kila muislamu kuwa askari lakini kulikuwa na jeshi maalum kwa ajili ya ulinzi wa Dola na raia.
- Kulikuwa na askari wa farasi, wa miguu na la wanamaji lililoanza wakati wa

Ukhalifa wa Uthman (r.a).

- Kuliimarishwa zaidi kwa Idara ya ulinzi na usalama ukilinganisha na wakati wa Mtume (s.a.w).