Maadui wa Uislamu na dola ya kiislamu

Upinzani dhidi ya Dola ya Kiislamu Madinah.
Maadui wakubwa wa Dola ya Kiislamu Madinah.
Kwa kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa Mtume (s.a.w) maadui walioibuka kupambana na Dola ya Kiislamu walikuwa;
oMakafiri wa Kabila la Kiquraish.
oWanafiki.
oMayahudi
oWarumi (Wakristo).
oMakabila mengine ya Kiarabu.Makafiri wa Kiquraish.
- Walivamia mji wa Madinah na kupora mifugo na kuipeleka Makkah.
- Walimwandikia barua kwa kiongozi wa wanafiki Abdullah bin Ubayyi kumtaka wamfukuze Mtume (s.a.w) kutoka mji wa Madinah.
- Kuwatishia vita makabila yaliyokuwa yakiishi kati ya Makkah na Madinah yawe dhidi ya Uislamu na wasijekusilimu.
- Walichoma moto mashamba ya mitende ya waislamu Madinah.
- Walimchoma mkuki Zainabu bint Muhammad (s.a.w) wakati akielekea Madinah.Wanafiki.
- Walikuwa wanatoa nyudhuru za uongo kuepuka jukumu la kupigana jihadi.
- Walimzulia uzinifu mke wa Mtume (s.a.w) Aisha (r.a) kuwa amezini na sahaba Safwan (r.a) wakati wa kurudi msafara wa Banu Mustaliq.
- Walijenga msikiti wao kama kichaka cha kupiga vita Uislamu na kutaka kumuua Mtume (s.a.w).
- Walishirikiana na maadui wengine wa Uislamu ili kuupiga vita Uislamu.
- Walijitenga wanafiki 300 katika vita vya Uhudi na kuwaacha waislamu 700 Waliopambana na maadui wa Kiquraish 3,000 waliojizatiti kivita.
- Walichochea ugomvi baina ya Muhajirina na Answar na kutishia kumfukuza Mtume (s.a.w) Madinah wakiongozwa na Abdullah bin Ubayyi katika msafara wa vita vya Banu Mustaliq.Mayahudi.
- Walishirikiana na wanafiki katika kuwatia wasi wasi waislamu walipobadilishiwa Qibla kutoka Jerusalemu na kuelekea Al-Kaaba, Makkah.
- Walitangaza kuwa Mtume (s.a.w) ni mtume wa uongo.
- Waliifanyia Qur’an stihizai (mzaha).
Rejea Qur’an (2:245), (3:181).- Wamjaribu Mtume (s.a.w) kwa kumuuliza maswali ya kubabaisha yasiyo na majibu ya dhahiri, kama vile:
Usingizi wako ukoje.
Ni vitu gani Israil (Nabii Yaaqub) alijiharamishia mwenyewe.
Ni malaika yupi anakuletea wahayi, n.k.- Kuwavunja moyo na kuwadhalilisha waislamu.
- Walishirikiana na Wanafiki kwa njama za kutaka kumuua Mtume (s.a.w) na kuuhilikisha Uislamu.
- Walivunja na kusaliti mikataba ya amani waliowekeana na Mtume (s.a.w).
- Walichochea fitina baina ya Answar kwa kuwakumbushia ugomvi wao wa zamani baina ya Aus na Khazraj.
Rejea Qur’an (3:100-101).Warumi (Wakristo).
- Gavana, Shurahbil bin Amr Ghassaany wa Dola ya Kirumi alimuua mjumbe wa Mtume (s.a.w), Haarith Bin Umair Al-Az katika mji wa Muttah.
1. Mtume (s.a.w) alituma jeshi la askari 3,000 kupambana na jeshi la Kirumi lenye askari 100,000.

2. Mtume (s.a.w) alichagua makamanda watatu, ambao ni Zaid bin Harith (r.a), Ja’afar bin Abi Twalib (r.a) na Abdullah bin Rawahah (r.a) na kuwaagiza kuwa akiuawa moja anayefuatia achukue nafasi na wakiuawa wote basi wamchague miongoni mwao aongoze jeshi.

3. Makamanda wote 3 waliuawa na hatimaye walimchagua Kamanda Khalid bin Walid (r.a) aliyeoongoza jeshi kishujaa na kupelekea kupata ushindi.

4. Kutokana na ushujaa walioonyesha waislamu katika vita vya Muttah, Warumi walipata woga na kulikimbia jeshi la waislamu katika msafara wa Tabuuk.

5. Kuwashinda Warumi kulipelekea Dola ya Kiislamu kuwa Super Power ya Ulimwengu wakati wa Mtume (s.a.w) na ndio kutimia lengo la kuletwa kwake.
Rejea Qur’an (48:28).Makabila mengine ya Waarabu.
- Mtume (s.a.w) alilishughulikia na kulitia adabu kila kabila la Kiarabu lililojaribu kuleta choko choko dhidi ya Dola ya Kiislamu.

- Makabila ya Taif ya Bani Thaqif na Bani Hawazin yaliyokuwa na nguvu kijeshi, Mtume (s.a.w) aliyasambaratisha katika vita vya Hunain akiwa na askari 12,000, baada ya Fat-h Makkah mwaka wa 8 A.H.

Katika vita vya Hunain, Mwenyezi Mungu (s.w) aliwaacha Waislamu wapate fundisho kwanza, kwa kupata kipigo kutoka kwa maadui.

Mwenyezi Mungu (s.w), aliwaonesha waislamu kuwa, ushindi wao haupatikani kwa wingi na ubora wa silaha zao tu, bali kwa msaada wake.

Baada ya fundisho hilo, waislamu walipata ushindi wa kishindo baada ya Mwenyezi Mungu (s.w) kushushia Malaika.Waislamu walipata ushindi na kuchukua ngawira mbali mbali zikiwemo;
-Ngamia 24,000
-Kondoo 40,000
-Aqyyah (fedha taslim) 4,000/=
-Mateka 6,000“Bila shaka Mwenyezi Mungu amekunusuruni katika mapigano mengi, na siku ya Hunayni (pia); ambapo wingi wenu ulikupandisheni kichwa, lakini haukukufaeni chochote, na ardhi ikawa dhiki juu yenu; ingawa ilikuwa yenye wasaa, kisha mkageuka mkarudi nyuma (mnakimbia). Kisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume Wake na juu ya walioamini. Na akateremsha majeshi (ya Malaika) ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru; na hayo ndiyo malipo ya makafiri.” (9:25-26).