CHANZO CHA VITA VYA VITA VYA AL-FIJAR NA ATHARI ZAKE

MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU).

CHANZO CHA VITA VYA VITA VYA AL-FIJAR NA ATHARI ZAKE


MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU).
Vita hivi ni vita vilivyotokea kati ya kabila la kiquraysh wakisaidiwa na Kinana kutokea makkah na kabila la Qays 'Aylan kutokea taif. Na vita hivi vilitokea ndani ya miezi mitukufu na vilidumi kwa muda wa miaka mktano. Na mapigano halisi yalidumu kwa muda wa siku tano tu. Vita hivi vimeitwa vita vya uovu kwani vilifanyika ndani ya miezi mitukufu. Vilitokea vita hivi wakati Mtume alipokuwa na miaka kumi na tano. Na alishiriki katika vita hivi. Ijapokuwa Mtume hakupenda kushiriki vita hivi alifanikiwa kutokushiriki ndani ya siku 2 za kwanza lakini siku tatu zilizofata ilibidi ashiriki. Hakuwahi kunyanyua upanga kwa ajili ya kupigana ila alishiriki katika kuokota misahare na kuwapatia wapiganaji.

Inasemekana katika mwezi wa dhul-qada (mfunguo ilikuwa ni ada ya waarabu enzi hizo kufanya sherehe katika sehemu iitwayo Ukaz. Katika sehemu hii ndani ya masiku haya michezo mbalimbali ilifanyika kama kamari, mashindano ya kuchezea panga, kushindana kuimba mashairi, wanawake kucheza na mengineyo mengi. Pia biashara zilikuwa zikifanyika katika eneo hili. Sasa vita hivi vilitokea kwasababu ya sintofahamu iliyotokea kati ya watu wawili wafanyabiashara. Mmoja kutoka kwenye kabila la Quraysh (Makkah) na mwengine kutokea kabila la Qays 'Aylan kutoke taif.

Sababu ni kuwa mtu mmoja kutoka katika kabila la Quraysh alikuwa na mteja, na ikatokea kuwa mfanyabiashara mwingine kutoka kabila la Qays 'Aylan akawa anamfatilia mteja yuleyule. Basi ahapa ndipo pakazuka mgogoro na hatimaye Mtu kutoka kabira la quraysh akamuua yule wa kabila la Qays 'Aylan. Watu kutoka Taif wakaandaa jeshi kuja kulipa kisasi cha ndugu yao alouliwa bila ya sababu. Watu kutoka kabila la Quraysh wakaandaa jeshi nao kwa kulinda heshima ya kabila lao. Bila ya kujali mwezi mtukufu ambao ni haramu kumwaga damu au kupigana, na bila ya kujali sheria zao juu ya mtu aliuliwa kwa makusudi sheria inasemaje. Wakaamuwa kupigana vita kali sana.

Vita vilianza mwanzoni mwa siku na toka vinaanza ushindi ulikuwa ni kwa kabila la Qaysh 'Aylan lakini ilipofika mida ya jioni meza ikabadilika na ushindi ukawa ni wa Quraysh. Harb bin Umayyah (Baba yake mdogo Mtume (s.a.w)) ndiye alokuwa kiongozi wa vita kwa upande wa Mqauraysh na wasaidizi wake. Mwishoni mwa siku ya tano viongozi wa pande zote walikubali kuacha kupigana na wakaamuwa kufanya majadiliano ya amani kumaliza vita na hapa wakawekeana mkabata (maakubaliano) ulofahamika kwa jina la Al-Fudhul.


                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 174

Post zifazofanana:-

kwa nini riba ni haramu?
Soma Zaidi...

SCIENTIFIC PROCESSES IN BIOLOGY
SCIENTIFIC PROCESSES IN BIOLOGYY THE USE OF SENSE ORGANS TO MAKE CORRECT OBSERVATION Sense organ this is an organ of the body that responds to external stimuli by conveying impulses to the sensory nervous system. Soma Zaidi...

Faida za kula Pilipili
Usiogope kuwashwa, kula pilipili ni nzuri kwa afya yako ia virutubisho vingi sana Soma Zaidi...

Taratibu na namna ya kutafuta mchumba na sifa za mchumba
Soma Zaidi...

Dalili za kujifunguwa, na dalili za uchungu wa kujifunguwa
Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran
Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki. Soma Zaidi...

MAANA YA Quran
Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi. Soma Zaidi...

KUAMINI MITUME WA ALLAH (S.W)
Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s. Soma Zaidi...

Msafara wa vita vya Tabuk Dhidi ya Warumi
Ukombozi wa mji wa Makka (Fat-h Makka) mwaka 8 A. Soma Zaidi...

Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.
Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s. Soma Zaidi...

Mafungu ya mirathi katika uislamu
Mafungu ya urithi yaliyotajwa katika haya sita yafutayo:1. Soma Zaidi...

FORM ONE CHEMISTRY
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...