2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w Quran, tawrat, Zabur na injili

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w Quran, tawrat, Zabur na injili

2.

Download Post hii hapa

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w Quran, tawrat, Zabur na injili

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w

2.3.Kuamini Vitabu Vya Mwenyezi Mungu (s.w)
Vitabu vya Mwenyezi Mungu vilivyotajwa ndani ya Qur’an ni;
1.Suhufi – aliteremshiwa Nabii Ibrahim (a.s) na Nabii Musa (a.s).
2.Taurat – aliyoteremshiwa Nabii Musa (a.s)
3.Zaburi – aliyoteremshiwa Nabii Daud (a.s)
4.Injili – aliyoteremshiwa Nabii Isa (a.s) na
5.Qur’an – aliyoteremshiwa Nabii au Mtume Muhammad (s.a.w).



3. Kuhifadhiwa na Kulindwa Vitabu.
Qur’an imebaki katika asili yake kama ilivyoteremsha bila kubadilishwa chochote na wanaadamu ndani yake.
Rejea Qur’an (15:9) na (41:42)

Vitabu vingine vimepotea katika asili yake kwa kupunguzwa, kuongezwa na kupotoshwa asili ya ujumbe wake na mikono ya wanaadamu..



4. Hitoria ya Kushushwa Vitabu.
Historia ya kushushwa Qur’an inajulikana vyema mfano; namna, sehemu, muda/kipindi na sababu ya kuteremshwa kila aya.

Vitabu vingine historia ya kushushwa kwao haijulikani, mfano; muda, nama, sababu au sehemu.




Lengo la kushushwa Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).

Ni kuwa mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu katika kufuata maamrisho na kuacha makatazo yote ya Mwenyezi Mungu (s.w) hapa ulimwenguni.
Rejea Qur’an (2:38-39), (2:185) na (5:44).



Maana ya Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku.
Waumini wa kweli wa vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w) ni wale wanaoendesha kila kipengele cha maisha yao ya kila siku kwa mujibu wa mwongozo uliopo katika vitabu hivyo.



Sababu za kutokubalika Vitabu vilivyotangulia kuwa Mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu zama hizi.
1.Vitabu vilivyotangulia vimeingiliwa na mikono na matashi ya wanaadamu kiasi cha kupoteza au kupotoshwa ujumbe wake wa asili.

2.Lugha ya vitabu vilivyotangulia imetoweka na kusahaulika duniani kiasi kwamba hata kingelikuwapo kimojawapo katika lugha yake asili, ujumbe wake usingelifahamika kwa watu.

3.Vitabu vilivyotangulia vilikuwa ni mwongozo kwa watu maalum na kwa wakati maalum tu, havikuwa mwongozo kwa walimwengu wote na nyakati zote.




Sababu za Qur’an kuwa mwongozo sahihi pekee wa maisha ya mwanaadamu.
1. Qur’an yote ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake, hivyo ni mwongozo wa uhakika.
2. Ujumbe wa Qur’an umeelekezwa kwa walimwengu wote na zama zote zilizobakia hadi siku ya Qiyama.



Maana ya Kuiamini Qur’an katika maisha ya kila siku.
Maana halisi ya kuiamini Qur’an kama Kitabu pekee cha mwongozo sahihi wa maisha ya mwanaadamu (muumini) ni kufanya yafuatayo;
i.Kuwa na yakini pasina shaka yeyote kuwa Qur’an yote ni maneno ya Mwenyezi Mungu (s.w) peke yake.
Rejea Qur’an (2:2).



ii.Kuufahamu vyema ujumbe wa Qur’an na kuuheshimu inavyostahiki kwa kujizatiti katika kujifunza kuisoma na kuijua ipasavyo.
Rejea Qur’an (73:4) na (7:204-205).



iii.Kulifahamu vyema lengo la Qur’an na kuiendea kwa lengo lake tu.
Rejea Qur’an (14:1), (2:185) na (16:64).



iv.Kuitekeleza Qur’an katika kukiendea kila kipengele cha maisha yetu ya kila siku kwa mujibu wa lengo lake tu.
Rejea Qur’an (5:44, 46-47).



                   

Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 3399

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Lengo la swala
Lengo la swala

Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake.

Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran
mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
SHIRK
SHIRK

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...