picha

Umuhimu wa kusimamisha uislamu katika jamii

1.

Umuhimu wa kusimamisha uislamu katika jamii

1.4.Maana ya Kusimamisha Uislamu katika jamii.
Ni pale ambapo waislamu katika jamii wataweza kuendesha kila kipengele cha maisha yao ya binafsi na jamii katika siasa, uchumi, utamaduni, n.k kwa kufuata kikamilifu muongozo wa Qur’an na Sunnah.
Rejea Qur’an (3:83), (10:99), (32:13), (61:8) na (64:2).




n b 1.5.Umuhimu wa Jihad katika kusimamisha Uislamu katika jamii.

i.Kusimamisha Uislamu (Jihad) katika jamii ni amri (faradh).
Kama ilivyoamrishwa swala, funga, zakat na hijja, Neno “kutiba” (mmelazimishwa) limetumika katika jihad kama lilivyotumika katika kufunga, kulipa kisasi na faradh zingine pia za kutekeleza Uislamu.
Rejea Qur’an (2:216), (2:183), (2:178,180) na (22:78).



ii.Msamaha na Pepo hupatikana kwa kufanya juhudi (jihad) za maksudi katika kusimamisha Uislamu katika jamii.
Kutekeleza faradh kama swala, funga, zaka na hija na ibada zingine za sunnah za binfsi, itakuwa sio sababu ya msingi ya kupata msamaha na pepo ya Mungu, mpaka jitihada ya dhati katika kupigania Uislamu katika jamii ifanyike.
Rejea Qur’an (4:74), (9:111), (61:10-13), (2:154), (3:169-171), (3:142), (3:157), (2:214) na (9:16).



iii.Mwenyezi Mungu (s.w) ameteremsha chuma (silaha) kuwa nyenzo ya kusimamisha Uislamu katika jamii.
Mitume wametumwa kusimamia haki na uadilifu katika jamii kwa kutumia miongozo ya vitabu vya Allah (s.w) na pia chuma (silaha) kimeteremshwa ili mitume na waumini wakitumie katika kusimamia haki na uadilifu ndani ya jamii.
Rejea Qur’an (57:25).




iv.Kusimamisha Uislamu katika jamii ndio lengo kuu la maisha ya Waumini.
Mwenyezi Mungu (s.w) ametubainishia kuwa chochote tutakachokipenda au tutakachokifanya nje na lengo la kusimamisha Uislamu katika jamii hatakuwa na radhi juu yetu. Rejea Qur’an (9:23-24).



1.6. Kwa nini ni muhimu Kusimamisha Uislamu katika jamii?
Ni muhimu Uislamu kusimama katika jamii ili matunda yafuatayo yapatikane;
i.Waumini wataweza kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah kwa kila kipengele cha maisha ya kila siku binafsi na jamii katika siasa, uchumi, elimu, utamaduni kama wanavyotekeleza swala, funga, hija, n.k.
Rejea Qur’an (51:56), (2:21-22), (7:54), (9:31), (2:85), (2:208), (2:193), (4:75-76), (9:38), (8:39), (22:40) na (47:7).



ii.Kupatikana amani ya kweli na kuondoka hofu na mashaka katika jamii. Hii ni baada ya waumini kuchukua hatamu ya uongozi katika jamii kwa mujibu wa muongozo na sheria za Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (57:25), (2:257) na (5:90-91).



iii.Waumini wataweza kuamrisha mema na kukataza maovu kikamilifu katika jamii pasina kikwazo chochote pindi watakapochukua nafasi ya kuiongoza jamii.
Rejea Qur’an (22:41) na (3:110).



iv.Kuikinga jamii na majanga mbali mbali. Waumini watakapochukua nafasi za kuiongoza jamii ndio itakuwa sababu ya kutoweka maovu ndani jamii ambayo ndio sababu ya kupatikana majanga katika jamii.
Rejea Qur’an (8:25).



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: General Main: Dini File: Download PDF Views 2673

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

DARSA ZA TAWHID

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
fadhila za sura kwenye quran

FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Dua 120

Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe vyote.

Soma Zaidi...
MAANA YA HADITHI SUNNAH

Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila.

Soma Zaidi...
MAANA YA Quran

Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi.

Soma Zaidi...
HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI

Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.

Soma Zaidi...