MUDA WA KUCHAJI SIMU YAKO AMA MUDA WA KUCHAJI BETRI YAKO
Wwatu wengi wamekuwa wakijiuliza ni muda gani hasa inapasa kuchaji simu, je nisubiri mpaka chaji iishe kabisa, ama nichaji ikiwa na asilimia ngap?
MUDA WA KUCHAJI SIMU YAKO
Wwatu wengi wamekuwa wakijiuliza ni muda gani hasa inapasa kuchaji simu, je nisubiri mpaka chaji iishe kabisa, ama nichaji ikiwa na asilimia ngap?. maswali kama haya na yanayofanana nitakwenda kuyajibu katika makala hii.
Kikawaida betri inaweza kudumu kuwa hai kati ya miaka 5 mpaka 10. lakini uwezo wa betri hupungua kadri siku sinavyoendelea. Unaweza kudhibiti hali hii kwa kuwa makini na baadhi ya mambo kadhaa. Miongoni mwa mabo hayo ni kuwa makini na muda wa kuchaji.
Wataalamu wa teknolojia wanatueleza kuwa muda mzuri wa kuichaji betri ni pale itakapobakiwa na asilimia kati ya asilimia 50% na 90%. na hakikisha kuwa huichaji mpaka ifikapo 100%. ni vyema kama unataka ifike 100 basi angalau ufanye hivyo mara chache.
Sio vyema sana kuilaza kwenye chaja japo jambo hili halina madhara kwa simu za kisasa kwani zenyewe zina kifaa cha kuifanya isimame kuchaji pindi ikifapo asilimia 100% ya chaji.
Hakikisha betri yako haivi chini ya asilimia 40% na mbaya zaidi isifike asilimia 2% ama 0%. na kama unahitaji kuihifadhi betri yako basi ichaji angalau asilimia 40% kisha uihifadhi.
Kama unataka kutumia simu ikiwa chaji hakikisha unatumia chaja yake ama chaja original ya simu hisika, na epuka kutumia simu yako inapokuwa imoto. Na kama unailaza kwenye chaja hakikisha unaondoa vitu vyote vitakavyo sababisha iwe na moto kama kuiweka juu ya kitu kimoto kama deki.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 web hosting 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Jinsi ya kufanya simu yako iwe fasta
Posti hii inakwenda kukuelekeza njia za kufanya simu yako iwe fasta
Soma Zaidi...KULINDA AKAUNT YAKO YA FACEBOOK DHIDI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO
Watu wengi wanalalamika kuwa akaunti zao za facebook zimehakiwa, yaani zimeshambuliwa na wahalifu wa kimtandano.
Soma Zaidi...Matumizi ya OCR katika simu yako
Somo Hili linakuleteq mafunzo ya OCR katika simu yako
Soma Zaidi...Utajiaje kama simu/kompyuta ina virusi
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta..
Soma Zaidi...