Ujuwe mlo sahihi kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo

Post hii itakwenda kuangalia mlo sahihi wa mwenye vidonda vya tumbo. Hata utajifunza ni vyakula vipi hapaswi kula na vipi ana paswa kula.

VYAKULA VYA KUVIEPUKA KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

Vidonda vya tumbo ni nini?

Vidonda vya tumbo ni aina za vidonda ambavyo hutokea kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Vidonda vivi vinaweza kutokea kwenye tumbo ama utumbo. Hata hivyo koo la chakula linaweza kuathirika kupata vidonda, jambo hatuviiti vidonda vya tumbo. Vidonda vya tumbo vinaweza kuleta maumivu makali sana ya tumbo na mara nyingi hutokea wakati mtu ana njaa.

 

Nini husababisha vidonda vya tumbo?

Sababu kuu ya kutokea kwa vidonda vya tumbo ni mashambulizi ya bakteria wanaojulikana kama Helicobacter pylor (H.pylor). bakteria hawa wanaishi kwenye tumbo. Mtu anaweza kuishi na bakteria hawa kwa miaka kwa miaka mingi bila ya kusabbabisha madhara yeyote yale. Lakini si mara zote, bakteria hawa wanaweza kusababisha kuvimba (inflamation) kwenye kuta za tumbo, na kupelekea kutokea kwa michubuko na hatimaye vidonda vya tumbo. Vingine vinavyosababisha vidonda vya tumbo ni kama:-

  1. Misongo ya mawazo
  2. Ongezeko la uzalishwaji wa tindikali tumboni
  3. Matumizi mabaya ya dawa
  4. Saratani ya tumbo

 

Dalili za vidonda vya tumbo

Maumivu ya vidonda vya tumbo ni makali, pia mgonjwa wa vidonda vya tumbo anaweza kupatwa na changamoto nyingine ambazo ni katika dalili za vidonda vya tumbo. Kwa mfano kutapika, kiungulia cha mara kwa mara, tumbo kujaa gesi, maumivu ya kifua, kupungua kwa damu na uzito. Endapo vidonda vya tumbo vitadumu kwa muda mrefu bila ya kupatiwa matibabu afya ya mgonjwa inaweza kuwa mbaya ijapokuwa vidonda vya tumbo havisababishi kifo.

 

Vipi nitatuliza maumivu?

Unaweza kutuliza maumivu ya vidonda vya tumbo kwa kutumia dawa za hospitali. Pia kwa kutumia dawa za kienyeji pia. Lakini unaweza kutuliza maumivu haya kwa kutumia vyakula. Wapo baadhi ya wagonjwa wa vidonda vya tumbo hutumia baadhi ya vyakula kutuliza maumivu. Mfano wa vyakula hivyo ni maziwa. Endelea na makala hii hapo chini utajifunza vyakula hivi vilivyo vizuri kwa vidonda vya tumbo.

 

 

 

Nini husabaabisha maumivu?

Maumivu ya vidonda vya tumbo pia yanaweza kusababishwa na matumizi ya madawa na vyakula ama vinywaji fulani. Pia kukaa kwa njaa kwa muda mrefu kunaweza kuleta maumivu kwa mgonjwa. Hutokea pia misongo ya mawazo ikawa pia ni vichochezi vya maumivu haya. Huenda mgonjwa anatumia hivi bila ya yeye kujua ama anatumia kwa sababu hana namna nyingine ya kufanya. Kwa mfano ijapokuwa maziwa hutuliza maumivu lakini kitaalamu sio mazuri sana kwa mgonjwa. Endelea na makala hii hapo chini utajifunza vyakula hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

 

Vyakula anavyopasa kula mgonjwa wa vidonda vya tumbo.

Ni ngumu sana hapa kuanza kukuorodheshea orodha ya vyakula vyote anavyotakiwa kula mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Hata hivyo kila jamii ina aina ya vyakula vyao ambavyo ni ngumu kujulikana kwa watu wa jamii nyingine. Hapa nitakuletea tu kanuni ambazo utaziangatia pindi unapochaguwa chakula kwa ajili ya kutumiwa na mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Angalia vyakula vyenye sifa hizi:-

  1. Vyakula ambavyo havina gesi
  2. Vyakula ambavyo havina uchachu sana
  3. Vyakula ambavyo havina chumvi nyingi sana
  4. Vyakula ambavyo havina mafuta mengi
  5. Pia vyema ukatumia na vyakula vifuatavyo kwa namna ambayo unaona itafaa kwa upande wako:-

 

  1. kabichi
  2. matunda aina ya maepo
  3. karoti
  4. mboga za majani za kijani
  5. asali
  6. kitunguu thaumu

Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo:

Kama nilivyokueleza hapo juu kuhusu kanuni za kuzishikili unapochaguwa vyakula basi hapa pia utaendelea na kanuni zile zile pindi unapotaka kuepuka vyakula ukiwa kama mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Epuka vyakula hivi:-

  1. vyenye gesi kama maharagwe
  2. vyenye uchachu sana
  3. vyenye pilipili kwa wingi
  4. vyenye mafuta mengi
  5. vyenye chumvi nyingi

Pia punguza matumizi ya vifuatavyo ama wacha kabisa iwezekanapo:-

  1. sigara
  2. pombe
  3. kahawa
  4. maziwa unaweza kupunguza tu matumizi
  5. pilipili kwa wingi

 

Vipi nitajilinda na vidonda vya tumbo?

Ni ngumu sana kwa sababu mpaka leo bado haijajulikana sababu ya kupata bakteria wa vidonda vya tumbo. Hivyo kujikinga na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na mashambulizi ya bakteria ni ngumu. Ila kwa kuwa sababu za kutokea kwa vidonda vya tumbo ni nyingi, unaweza kujikinga na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na sababu nyingine. Njkia hizo ni kama:-

  1. Punguza misongo ya mawazo
  2. Wacha ama punguza kutumia kilevi
  3. Punguza ama wacha kabisa kuvuta sigara
  4. Wacha kutumia dawa kiholela

 

Je vidonda vya tumbo vinaweza kupona kabisa?

Tambuwa kuwa vidonda vya tumbo vinatibika bila ya wasi wowote ule. Unaweza kutibiwa na ukapona kabisa. Hakuna muda maalumu wa kupona lakini haiwezi kumaliza miezi hata sita utapona kabisa. Tukutane makala inayofata ttakapojifunza kuhusu matibabu na dawa za vidonda vya tumbo.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/18/Wednesday - 07:45:53 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2471

Post zifazofanana:-

Dalili za ugonjwa wa ngiri
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo mgonjwa wa ngiri anaweza kuzipata, kwa hiyo baada ya kusoma na kuelewa dalili hizi mgonjwa anapaswa kuwahi hospitali mapema kwa ajili ya kupata matibabu. Soma Zaidi...

Fahamu maambukizi ya kwenye mishipa ya Damu.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa ambao husababisha kuvimba kwa mishipa ya damu katika mwili wako wote. Ambao kitaalamu hujulikana Kama Behcet . Soma Zaidi...

Sababu za ugonjwa wa mkojo kuwa na damu
Posti hii inaelezea sababu zinazosababisha mkojo kuwa na damu. Soma Zaidi...

Matumizi ya OCR katika simu yako
Somo Hili linakuleteq mafunzo ya OCR katika simu yako Soma Zaidi...

hathari zitokanazo na uvutaji wa sigara ,pombe na madawa ya kulevya na mbinu za kujikinga nayo
Posti hii inahusu zaidi utumiaji wa pombe na sigara pamoja na madawa katika jamii. Soma Zaidi...

Sababu za mimba kutoka
Post hii inahusu zaidi sababu za mimba kutoka, hili ni tatizo ambalo linawakumba wanawake wengi ambapo mimba utoka kabla ya kumfikisha mda wake, kwa kawaida Ili kawaida mimba nyingi utoka zikiwa na miezi chini ya Saba au wengine wanaweza kusema kwamba mim Soma Zaidi...

Huduma kwa mama mwenye kifafa cha mimba.
Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wajawazito wanaweza kuzipata wakiwa na Dalli au tayari wana kifafa cha mimba. Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu mapacha wanaofanana
Post hii inahusu zaidi watoto mapacha wanaofanana,ni watoto wanaozaliwa wakiwa wanaofanana kwa sura na hata group la damu huwa ni Moja. Soma Zaidi...

Zijuwe faida za kiafya za kula nanasi
Je umeshawahi kula nanasi kwa wingi. Soma Zaidi...

Yajue magonjwa ya kurithi.
Posti hii inahusu zaidi Magonjwa vya kurithi ambayo mara nyingi utokea kwenye jamii ni magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwenye familia na wanafamilia walio wengi wakaweza kupata ugonjwa huo Magonjwa yenyewe ni kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Habari nasumbuliwa na tumbo upande wakilia adi nikikojoa mkojo wa mwisho uwa wa kahawia tiba take nini?
Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo typhod, vidonda vya tumbo na shida nyingine kwenye mfumo wa chakula. Soma Zaidi...

Mafunzo ya HTML level 1 somo la 3 (HTML basic level FOR BEGINNERS)
Hili ni somo la Tatu katika mfululizo wetu wa mafunzo ya HTML kwa basic level kwa wanaoanza kujifunza. Hapa tutakwenda kujifunza tag za html ambazo huwa zinatumika katika uandishi. Soma Zaidi...