Je, Nabii Isa(a.s) ni Mtoto wa Mungu?

Mwenyezi Mungu si kiumbe.

Je, Nabii Isa(a.s) ni Mtoto wa Mungu?

Je, Nabii Isa(a.s) ni Mtoto wa Mungu?


Mwenyezi Mungu si kiumbe. Yeye ndiye Muumba wa kila kitu kilicho na kisicho na uhai. Kuzaa ni sifa za viumbe vya Mwenyezi Mungu, hivyo Mungu si baba mzazi wa Yesu wala si baba wa mwanadamu yeyote. Qur,an tukufu inatuamrisha:



Sema: Yeye Mwenyezi Mungu aliye mmoja (tu). Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuhitajiwa na viumbe. Hakuzaa wala hakuzaliwa. Na wala hafanani na yeyote(112:1-4)



Ama katika Biblia, neno Baba limetumika kuonesha sifa ya ulezi wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake, hivyo, Mwenyezi Mungu kuitwa Baba haimaanishi kuwa kamzaa Yesu au binadamu yeyote miongoni mwetu. Na ndiyo maana akasema:



Wala msimwite mtu baba duniani, Maana Baba yenu ni mmoja aliye wa mbinguni, wala msiitwe viongozi;maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo(Mathayo 23:9-10)Na katika maandiko mengine ya Biblia, Yesu amenukuliwa akisema: Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni; Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, hapa duniani kama mbinguni (Mathayo 6:9-10)



Kwa maana hii, Mwenyezi Mungu ni Baba wa watu wote, si baba wa Yesu tu. Ni Baba yetu, ila si kwamba katuzaa, bali ulezi wake wa kutujaalia riziki za kila aina na kutupatia elimu na teknolojia ya kuweza kuzitumia neema na riziki hizo. Hivyo Isa(a.s) si mwana wa Mungu wa kuzaa, bali ni kiumbe wake aliyemuumba kwa neno la β€˜Kuwa’, likawa kama alivyo muumba Adamu.

Bila shaka mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama Adamu; alimuumba kwa udongo, kisha akamwambia β€œKuwa”, akawa.(3:59)



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1533

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    πŸ‘‰6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Mtume kumuoa bi khadija

Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija.

Soma Zaidi...
Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume

Uchaguzi wa β€˜Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na mkataba wa aqabah katika kuandaa ummah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kifo cha Nabii Sulaiman

Pamoja na utukufu na umadhubuti wa ufalme wake Nabii Sulaiman muda wake wa kuishi ulipokwisha aliondoka kama walivyoondoka Mitume,wafalme na wanaadamu wengine.

Soma Zaidi...
Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri

Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji.

Soma Zaidi...