Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam

Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam.

Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam

Zakaria(a.s) Akabidhiwa Ulezi wa Maryam


Baada ya kupigwa kura juu ya nani awe mlezi wa Maryam, Nabii Zakaria akachaguliwa kuwa mlezi wa Maryam. Allah(s.w) akaikubali ile nadhiri na dua ya mama yake Maryam.



Basi Mola wake akampokea (mtoto) kwa mapokezi mema na akamkuza kwa makuzi mema, na akamfanya Zakaria awe mlezi wake. Kila mara Zakaria alipoingia chumbani(kwa Maryam) alikuta vyakula pamoja naye. Akauliza: β€œEwe Maryam! Unapatawapi hivi? Akajibu: β€œHivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila kutarajia(3:37)



Aya hizi zinatuonesha kuwa Maryam alikuwa katika malezi mema na uangalizi wa karibu toka kwa Nabii Zakaria(a.s) kiasi cha kuepusha mazingira ya ufuska yasimfikie.Allah(s.w) aliweka maandalizi haya mapema ili atakapoleta muujiza wake kwa Maryam kuzaa mtoto bila ya kuwa na mume isionekane kuwa alikuwa mzinifu, bali iwe ni dalili ya kuwepo Allah(s.w) mwenye nguvu na uwezo wa kila kitu.



Kutokana na mazingira hayo na hifadhi ya Allah(s.w) Maryam akakua vyema na kupata hadhi ya kuwa mwanamke bora kuliko wanawake wote:

β€œNa (kumbuka) Malaika waliposema: β€œEwe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuchagua na kukutakasa na kukutukuza kuliko wanawake wa ulimwengu (wote).(3:42)



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1856

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰2 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰3 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    πŸ‘‰6 Dua za Mitume na Manabii   

Post zinazofanana:

Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri

Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji.

Soma Zaidi...
Je waislamu walishindwa vita vya Uhudi?

Katika vita vya Uhudi waislamu walikufa wengi kulinganisha na makafiri. Lakini makafiri walikimbia uwanja wa vita baada ya kuzidiwa. Je ni nanibalishindwa vita vya Uhudi kati ya waislamu na makafiri?

Soma Zaidi...
Sababu ya uislamu kuwa ndiyo dini sahihi pekee

Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Shukurani za Nabii Ibrahiim(a.s) kwa Allah(s.w)

Kwa neema hii ya kuruzukiwa watoto wawili - Ismail na Is- haqa(a.

Soma Zaidi...
Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga

Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga.

Soma Zaidi...