Nabii Isa(a.s) Azungumza Akiwa Mtoto Mchanga
Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba.
Nabii Isa(a.s) Azungumza Akiwa Mtoto Mchanga
Maryam akamtwaa mwanawe, akaenda naye kwa jamaa zake amembeba. Watu wakastaajabu na kuwaza, imewezekanaje Maryam asiye mzinzi kumpata mtoto bila kuolewa. Na wengine wakauliza:
...............“Ewe Maryam! Hakika umeleta jambo la ajabu: Ewe dada yake Haruni! Baba yako hakuwa mtu mbaya wala mama yako hakuwa hasharati (19:27-28)
Kwa maswali hayo, ikawepo haja ya kumtakasa Maryam kuwa japo hakuolewa, hakumpata mtoto huyo kwa zinaa. Ndipo ikatimia kauli ya Allah(s.w) kuwa Nabii Isa(a.s) atazungumza akiwa kichanga.
Maryam akaashiria kwake (yule mtoto wamuulize yeye). Wakasema:“Tutazungumzaje na aliye bado mtoto kitandani? (19:29)
(Yule mtoto) akasema: “Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu, Amenipa kitabu na Amenifanya Nabii. Amenifanya mbarikiwa popote nilipo. Na ameniusia swala na zaka maadamu ni hai. (19:30-31)
Na ameniusia kumfanyia wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, muovu. Na amani iko juu yangu siku niloyozaliwa, siku nitakayokufa na siku nitakapofufuliwa kuwa hai(19:32-33)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
KIKAO CHA KUMFUKUZA MTUME MUHAMMAD KUTOKA MAKKAH (MAKA), KIKAO ALICHOHUDHURIA IBLISI
KIKAO CHAKALIWA KUJADILI HATMA YA MUHAMMAD KATIKA MJI WA MAKAHiki ni kikao kizito hakijapata kutokea toka muhammad katika ji wa maka.
Soma Zaidi...Maadui wakubwa wa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi
Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri.
Soma Zaidi...Mafunzo yatokanayo na kuanzishwa kwa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...