Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah
Baada ya mikataba miwili ya ‘Aqabah na baada ya Waislamu 75 kufika Yathrib salama, Mtume(s.
Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah
Baada ya mikataba miwili ya ‘Aqabah na baada ya Waislamu
75 kufika Yathrib salama, Mtume(s.a.w) aliwaita Waislamu na kuwapa habari njema, akawaambia:
“Allah(s.w) keshakupeni mahala pazuri pa amani pa kukaa na kuendesha Dini yenu bila ya kuteswa na yeyote. Mahali penyewe ni Yathrib. Nimekwisha pata habari kuwa ndugu zenu wako tayari kukupokeeni kwa hali na mali. Basi kila aliyetayari aondoke leo asingoje kesho, kwani ndugu zenu huko wamesimama mikono wazi, wanangoja kukupokeeni.”17?
Mtume(s.a.w) alitoa amri ya kuhama mnamo April, 622 A.D. mwaka wa 13 B.U na Waislamu katika makundi makundi walianza kuhama kwa siri kuelekea Yathrib. Ili maadui wasije ng’amua kuhama kwao, Waislamu walisafiri usiku na mchana walijipumzisha mafichoni. Walihama na mali ile tu iliyokuwa nyepesi kuchukulika. Vitu vyao vingine vyote waliviacha Makka ikiwa ni pamoja na nyumba zao, vikachukuliwa na jamaa zao waliobakia katika ukafiri. Ni ‘Uthman bin Affan peke yake aliyeweza kuchukua mali yake yote. Mali ya ‘Uthman isiyochukulika ilinunuliwa na jamaa zake kwa fedha taslimu.
Baada ya miezi miwili hivi, takriban Waislamu wote walikwisha hamia Yathrib. Waislamu wachache, akiwemo Abubakar na ‘Ali bin Abu Talib, walibakia Makka na Mtume(s.a.w) ili kufanikisha maandalizi ya kuhama kwake pale atakapopewa ruhusa ya kuhama na Mola wake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 web hosting 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 ai web app 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Mbinu za Mtume Salih(a.s) Katika Kulingania Uislamu
Kama Mitume waliotangulia, Nabii Salih(a.
Soma Zaidi...Mbinu na njia walizotumia maadui wa uislamu dhidi ya waislamu na dola ya kiislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...