HISTORIA YA MTUME DHUL-KIFL(A.S).

Mtume Dhul-kifl ananasibishwa na Ezekiel anayetajwa ndani ya Biblia. Ni miongoni mwa Mitume waliopata mateso sana mikononi mwa Bani Israil. Hata hivyo hakuacha kufundisha Ujumbe wa Allah. Tunamsoma Dhul-kifl katika aya zifuatazo:

“Na (mtaje) Ismail na Idris na Dhul-kifl – wote walikuwa miongoni mwa wanaosubiri. Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema” (21:85-86).

“Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhul-kifl, na hao wote walikuwa miongoni mwa watu bora” (38:48).

Mtume Dhul-kifl anatajwa kwa wema wake katika kuufuata mwongozo wa Allah(s.w). Na Mwenyezi Mungu anaahidi kuwa marejeo ya watu wema ni mahali pazuri kabisa.

“Huu ni ukumbusho (wa watu wema). Na kwa yakini wamchao Mungu mahali pao pa kurudia patakuwa pazuri kabisa” (38:49).