Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar

Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar



Zipo tofauti za kimawazo kuhusiana na uchaguzi wa Khalifa wa kwanza, Abubakar(r.a.) mara baada ya kutawafu Mtume (s.a.w.).


Wapo wasemao uchaguzi ule ulifanyika katika mazingira ya kuchanganyikiwa, kwani mkutano haukuwa rasmi. Maelezo ya kundi hili yameegemea kauli zisemazo kuwa Abubakar(r.a.) na Umar(r.a.) walistushwa na taarifa kuwa Ansar walikuwa wamekutana kwenye ukumbi wa mikutano wa Thaqifa Bani Saidah, kumchagua kiongozi anayetokana na wao ambaye


angeshika uongozi wa dola ya Kiislamu baada ya Mtume(s.a.w.). Kwa mujibu wa kauli hizo, Abubakar(r.a.) na Umar(r.a.) walilazimika kwenda kwenye mkutano huo wakiwa na dhamira ya kuzuia usiendelee, hasa ikizingatiwa kuwa Mtume alikuwa bado hajazikwa na hilo ni suala zito lilohitajia muafaka wa Waislamu wote.


Kundi jingine lina mawazo kuwa, pamoja na kuwa mkutano wa Ansar haukuwa rasmi, lakini kuchaguliwa Abubakar(r.a.) kuliwafiki, kwa kuzingatia dokezo za Mtume(s.a.w), ishara zitokanazo na Qur'an na aliyokuja kuyafanya Abubakar(r.a.) wakati wa uongozi wake, ambayo yalidhihirisha usahihi wa chaguo la mkutano wa Thaqifa Bani Saidah.


Wapo wanaosema kuwa kutokuwepo kwa watu wa nyumba ya Mtume (Ahlul-Bayt) katika mkutano ule, kunabatilisha zoezi zima la uchaguzi wa Khalifa wa kwanza. Maelezo ya kundi hili yanatiwa tashdid na usia, unaodaiwa kuachwa na Mtume(s.a.w.) kwa 'Ahlul- Bayt' muda mfupi kabla ya kutawafu kwake; unaosema kwamba haki ya uongozi wa ummah huu baada yake ni ya 'Ahlul-Bayt'. Kwa hivyo Ali(r.a.) ndiye aliyestahiki nafasi hiyo, na warithi baada yake ni wanawe Hassan na Hussein kwa kuwa ni wajukuu wa Mtume(s.a.w.). Kundi hili linadai Ukhalifa wa Abubakar(r.a.), Umar(r.a.) na Uthman(r.a.) ni batili kwa kuwa hao si katika watu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.) na walipewa uongozi katika mikutano isiyo rasmi. Aidha hatua ya kuwafanya Makhalifa ni kudhulumu haki ya Ali(r.a.) akiwa ndugu wa Mtume.


Na kuna wasemao kwamba, kwa kuwa Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu si ya ukoo, kabila au Taifa fulani, na kwa kuwa hakuna aya katika Qur'an inayomwamrisha Mtume(s.a.w.) kurithisha dhima ya uongozi baada yake kwa watu wa nyumbani kwake (Ahlul-Bayt), basi jukumu la uongozi wa ummah limeachwa mikononi mwa waumini wenyewe. Kiongozi atachaguliwa kwa kuzingatia sifa mbali mbali zikiwemo uoni, ucha Mungu, siha n.k.


Sifa zote hizo zimpelekee kuongoza kwa haki na uadilifu. Kwa hiyo
Ukhalifa wa Abubakar, Umar na Uthman si suala la kubishaniwa.





                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 178


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Maandalizi ya Kimafunzo aliyoandaliwa Mtume Muhammad
(i) Suratul- 'Alaq (96:1-5)'Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa 'alaq. Soma Zaidi...

Hitimisho juu ya Historia ya maimam wanne
Soma Zaidi...

Quran si maneno ya shetani
Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa mayatima
Soma Zaidi...

Nini maana ya tabii tabiina
Soma Zaidi...

Suluhu na kupatanisha kati ya mke na mume
Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Furqaan (25:64-76)
Soma Zaidi...

quran tahadhari
TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao. Soma Zaidi...

Ni yupi mtume wa mwisho? na je ni kwa nini Muhammad ndiye mtume wa mwisho?
Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZI MUNGU
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotaja katika surat An-Nisaa (4:60-63, 88, 138-145)
Huwaoni wale wanaodai kwamba wameamini yale yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako? Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUT(A.S) NA WATU WA SODOMA NA GOMORA
Mtume Lut(a. Soma Zaidi...