Kifo cha Khalia Uthman kilivyotokea

Kifo cha Khalia Uthman kilivyotokea

Khalifa Uthman Kufa Shahidi



Ni dhahiri wahaini wa Serikali waliona wakati umefika wa kufanya lile walilokusudia tangu pale walipoweza kumtoa Gavana wa Kufa na kumuweka wanayemtaka bila kuadhibiwa. Wakaibua mbinu ya kutuma watu watatu kwenda Madinah kuwasilisha malalamiko yao. Watatu hao walitoka Misri, Basra na Kufa. Walipofika Madinah baadhi ya maswahaba walimshauri Khalifa kuwa wauwawe lakini kwa msimamo ule ule wa kutotaka kumwaga damu ya Waislamu, Khalifa alikataa na kusema nitawasikiza. Khalifa aliwasikiliza kisha akatoa hutuba ndefu ambayo ndani yake alijibu shutuma zote. Baadhi ya sehemu ya hutuba hiyo ya kihistoria ni kama ifuatavyo:


Ninalaumiwa kwa kuwapenda ndugu zangu. Sio dhambi kwa mtu kumpenda ndugu yake. lakini sijamfanyia mtu udhalimu kwa sababu ya kupenda ndugu. Sijatumia chochote kwa ajili ya ndugu zangu kutoka kwenye mfuko wa Serikali...


Imesemwa kuwa nimewateua vijana wadogo maafisa. nimefanya hivyo kwa kuzingatia mchango wao katika uislamu. Hakuna anayekanusha uaminifu wao na mchango wao katika Uislamu, na Waislamu. Kuteuliwa kwa Usamah na Mtume (s.a.w.) kuwa kamanda wa jeshi ni ushahidi kuwa ujana sio kipingamizi cha kupewa uafisa.


Imedaiwa nimempa gavana wa Misri ngawira yote ya Afrika kaskazini kama zawadi. Ni kweli lakini niliposikia jamii haikupendezwa na jambo hili nimezichukuwa fedha zote kutoka kwa gavana na kuziweka kwenye mfuko wa Serikali (Baitul Mal).


Inadaiwa kuwa nimetenga mbuga za malisho ya Serikali kwa ajili ya wanyama wangu. Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, sitafanya hivyo. Katika mbuga hizo (mashamba hayo) ni wanyama wa Serikali tu (Baitul-Mal) ndio wanaolishwa humo, wote mnafahamu kuwa nilipopewa ukhalifa nilikuwa na wanyama wengi kuliko yeyote Arabia nzima. Leo nina ngamia wawili niliowaacha ili wanisaidie wakati wa Hija. Ingekuwaje, nitenge malisho ya Serikali kwa ajili yangu wakati wanyama wenyewe sina.
Watu wananilaumu kwa kuchoma nakala za Qur'an. Qur'an tukufu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu aliteremshiwa Mtume (s.a.w.). Maswahaba waliokiandika chini ya usimamizi wa Mtume wako hai. Nimepeleka ile nakala ya Qur'an iliyokusanywa na maswahaba.


Inasemwa kuwa nimemrudisha Hakam Madina ambaye alipelekwa uhamishoni na Mtume. ukweli ni kwamba Mtume alimhamisha Hakam kutoka Makka kwenda Taif. Baada ya kumwombea Mtume alimruhusu aishi Madina. Nimetekeleza ruhusa iliyotolewa na Mtume (s.a.w.)....'


(Mwisho wa Hotuba yake akasema). Niambieni kama kuna kitu kisichokuwa cha kweli kati ya niliyosema.....39


Ingawa Khalifa alijibu shutuma zote kwa ufasaha, ukweli na uwazi, wawakilishi wa wapinzani walirudi na kusema uongo kuwa Khalifa amepuuza madai yao.


Ndipo wakaja makundi ya watu elfu, elfu kutoka Misr, Basra na Kufa na kupiga kambi karibu na Madina. Waliotoka Basra walipiga kambi Dhikhasha, waliotoka kufa walikaa 'Awas na waliotoka Misri walikaa Dhi-Murwah. Makundi ya wahaini hawa walishindwa kuingia Madina moja kwa moja kwa sababu walipokuwa wanakaribia Madina, Khalifa alikusanya wakazi wa Madina na kuwahutubia kuwa:


Wananikusudia mimi, karibuni hivi watakumbuka wakati wa ukhalifa wangu na kuujutia, wataona siku moja ni kama mwaka kwa sababu ya vurugu umwagaji damu na uasi utaoenea nchi nzima.40


Wananchi walichukua silaha na kuzuia uvamizi wa mji wao. Hali hii ndiyo iliyolazimisha wahaini kukaa nje ya Madina.


Wahaini hawa walikuwa na agenda moja tu, ya kumwondoa Khalifa madarakani kwa hiyari au kwa nguvu. ndiyo maana walipofika tu Madina kila kikundi kilimkabili waliyemtaka awe Khalifa kwani katika hili walitofautiana. Ibn Sabaa na Wamisri walimtaka Ali. Watu wa Kufa walimtaka Zubair na watu wa Basra walimtaka Talha. Maswahaba wote hawa walikataa na kuwaambia kuwa Mtume (s.a.w.) aliwaambia makundi ya Dhikhasha, 'Awas na Dhi-murwah yamelaaniwa.41


Khalifa aliwatuma maswahaba maarufu akiwemo Ali kusikiliza malalamiko yao. Waliwakilisha matakwa yao pamoja na kutaka Muhammad Ibn Abubakar awe gavana wa Misri badala ya Abu Mussa. Khalifa alikubali bila kuuliza kisha akawaahidi kuwa atatekeleza maombi yao. Ali naye akasisitiza hivyo hivyo. Pamoja na kuwakubalia matakwa yao walivamia msikiti na kumuua Khalifa Uthman akiwa nasoma Qur'an.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 124


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Kujiepusha na kufuata mambo kwa kibubusa
Waislamu wanakatazwa kufanya na kufuata mambo kwa kibubusa (kwa mkumbo) bila ya kuwa na ujuzi unaostahiki. Soma Zaidi...

Quran na sayansi
3; Mchujo wa maji dhaliliKatika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha yakuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalilina pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran?? Soma Zaidi...

Neema Alizotunukiwa Nabii Daudi(a.s)
Soma Zaidi...

DUA 120
Soma Zaidi...

Kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...

Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir
Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu. Soma Zaidi...

Epuka kuwa muoga na yajue madhara ya uwoga
36. Soma Zaidi...

nyakati za swala
3. Soma Zaidi...

Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat at-Tawbah
Mwenyezi Mungu amekuwia radhi (amekusamehe). Soma Zaidi...

NGUZO ZA UISLAMU: SWALA NA SHAHADA NA FAIDA ZAKE
NGUZO ZA UISLAMU. Soma Zaidi...

KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU
Soma Zaidi...

Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 04
Soma Zaidi...