Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume

Uchaguzi wa 'Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.

Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume

Uchaguzi wa 'Umar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.

Mtume(s.a.w.) kumchagua Abubakar kuwa Imam wa msikiti na kutoruhusu mtu mwingine kuswalisha na aliposwalisha mtu mwingine swala ilirudiwa ni dhahiri, kwa maoni yetu, Mtume(s.a.w.) aliashiria kuwa kiongozi awe Abubakar na akawaachia Waislamu waamue kumkubali au kumkataa. Tunaamini kuwa Abubakar alimuelewa hivi Mtume(s.a.w.) ndio maana alipokuwa anakaribia kutawafu aliwaita wajumbe wa Shura na kushauri kuwa yeye anampendekeza Umar awe ndiye Khalifa baada ya kifo chake. Wajumbe wa Shura walipokubali ndipo akamwambia Ali aandike usia huo. Abubakar alifanya hivi kwa jitihadi yake ambayo inakubalika katika Uislamu na hasa akizingatia hali ilivyokuwa mara Mtume alipofariki, Waislamu walipogawanyika makundi matatu yaani ukoo wa mtume, Muhajirin na Answari.

Hivyo alitumia njia hii ambayo ni ya Kiislamu, hakuiburuza Shura na kulikuwa na mjadala kabla ya kukubalika rai hiyo. Wajumbe maarufu wa Shura walikuwa 'Umar, Uthman, Ali,Talha, Abdul Rahman bin Auf, Muadh bin Jabal, Ubay bin Kaab, Zaid bin Thabit na wajumbe wengine mashuhuri kutoka Muhajirin na Ansar. Abubakar alitoa pendekezo lake la kumteua Umar kuwa Khalifa wa pili, wote walikubali ila walieleza wasi wasi wao juu ya ukali wa Umar, hii ndio hoja pekee iliyotolewa na Ali na Talha. Abubakar aliikataa hoja hii kwa kuwafahamisha kuwa Ukhalifa utamfanya asiwe mkali. Kwa kuwa hoja dhidi ya Umar ilikuwa hii tu basi pendekezo likakubalika.

Hatua iliyofuata ambayo imeimarisha uhuru wa kuchagua viongozi ni kuwahutubia waumini katika msikiti wa Mtume, akisaidiwa na jamaa zake, alisimama kwenye mimbari, kwanza alitaka ule usia usomwe mbele ya watu wote waliokuwa msikitini na yeye azungumze nao.9 Usia wenyewe ulikuwa kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahiim. Hili ni tamko linalofanywa na Abubakar bin Abi Qahafu ambaye yuko karibu ya kwenda akhera. Wakati wa kuwa katika hali ya kufa hata kafiri humuamini Mwenyezi Mungu, na hata mfanya madhambi hutubia (hurudi kwenye imani yake) na kafiri humtegemea Mwenyezi Mungu. Nimefanya kila jema kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwa kuboresha dini yake na kwa manufaa ya Waislamu na kwa mimi mwenyewe katika kumteua Umar kuwa Khalifa. Nategemea atakuwa muaminifu na mtekelezaji haki lakini akibadilika na kuwa dhalimu mimi sina lawama kwa kuwa sina elimu ya ghaibu. Kila mmoja anawajibika kwa afanyayo.24


Baada ya usia huu kusomwa, Abubakar alipanda kwenye mimbari huku akisaidiwa na kuuhutubia umma kama ifuatavyo:-

Enyi ndugu zangu, sikumchagua kuwa Khalifa ukoo wangu au ndugu zangu. Nimemteua aliyebora miongoni mwenu mnakubaliana na uteuzi wangu? Wote waliitikia kwa kukubali.11



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 94

Post zifazofanana:-

Haki na wajibu kwa masikini, mafukara na wasio jiweza
Soma Zaidi...

FANGASI SEHEMU ZA SIRI: DALILI ZAKE, CANZO CHAKE NA NJIA ZA KUPAMBANA NAO
Soma Zaidi...

Elimu
Uwanja wa elimu na maarifa Soma Zaidi...

Wanaoongozwa na wasioongozwa na quran
Soma Zaidi...

DONDOO 100 ZA AFYA
Pata dondoo 100 za Afya Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 15
24. Soma Zaidi...

Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.
Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah. Soma Zaidi...

Faida za kula Embe
Embe ni katika matunda atamu na yenye faida kubwa kiafya, soma makala hii hadi mwisho Soma Zaidi...

VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Nini Chanzo
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Njama za Mayahudi Kutaka Kumuua Nabii Isa(a.s)
Njama za kutaka kumuua Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Vyakula vya fati na mafuta na kazi zake
Soma Zaidi...