Uchaguzi wa Ali bin Abu Twalib kuwa Khalifa wa nne
Mkondo wa historia ya Kiislamu juu ya utaratibu wa kuingia kwenye mamlaka umechukua sura mpya, pale alipouliwa Khalifa wa tatu na wapinzani, na kundi hili la wapinzani likamtaka Ali awe ndiye Khalifa wa nne. Kwa hali ilivyokuwa naye akakubali kuchukua nafasi hiyo. Jambo hili lilipelekwa msikitini na wapo waliokubali Ukhalifa wa Ali bila masharti, wapo waliokubali kwa sharti kuwa wahalifu waadhibiwe na wapo waliokataa kumpa mkono wa ahadi ya utii miongoni mwao ni Muhammad bin Muslimah, Usamah bin Zaid, Hassan bin Thabit, Ka'ab bin Malik, Abu Said Khudri, Numan bin Bashir, Zaid bin Thabit, Mughirah bin Shubah na Abdullah bin Salama.27 Wengine waliokataa ni ndugu na jamaa wa ukoo wa Uthman. Baadhi ya waliokataa Ukhalifa wa Ali walihamia Syria. Kwa ujumla uchaguzi wa Ali(r.a) uliwagawa waislamu kwenye makundi manne yafuatayo:
(i) Wafuasi wa Uthman (Uthmanis), ambao walitaka dola iwaadhibu wauwaji. Watu wengi wa msimamo huu walikuwa wakazi wa Syria na Basra. Wasiria walimtaka Muawiyah ndiye awe Khalifa na sio Ali. Lakini Wabasra walitaka awe Talha au Zubeir.
(ii) Marafiki wa Ali (Shian-i-Ali). Watu hawa hawakumuona kuwa Uthman angefaa kuwa Khalifa. Hivyo wakajiita wenyewe Shia-i-Ali (marafiki wa Ali) watu wa mji wa Kufa (Wakufa/Kufans) na Wamisri ndio waliokuwa na msimamo huu. Inaaminika kuwa kundi hili ndilo lililomuua Uthman.
(iii) Mashibah: Watu hawa walikuwa kwenye Jihad wakati Uthman anauliwa. Hawakuwaunga mkono Uthmanis wala Shias.
(iv) Ahli-Sunnah wal Jamaah: Kundi hili lilikuwa lenye maswahaba wengi na lilienea Dola yote ya Kiislamu. Hawa wanasema tunawapenda wote Uthman na Ali. Wote ni Maswahaba waongofu. Kama kuna aliyefanya makosa ni kutokana na ijtihada, yake. Tunafuata Sunnah za Mtume na Sunna za Jamaa waongofu yaani kundi la Maswahaba.28
Utaratibu huu, ingawa kuna baadhi ya wanachuoni wanaoukubali lakini hauhitaji mjadala wowote, ni wazi kuwa hauna nafasi katika Uislamu. Kwa hakika watu wa Madina walikuwa na khofu na kundi hili la wauwaji hivyo kukubali kwao ule Ukhalifa wa Ali kwa mfumo ule yawezekana ni matokeo ya woga tu na siyo hiyari yao. Majibu ya Zubeir na Talha walipoulizwa na mjumbe wa Gavana wa Basra katika msafara wa Bibi Aisha kwa nini wanavunja Ahadi ya utii kwa Khalifa walisema. 'Ba'iyah ilifanywa mbele ya ncha ya upanga na ahadi ya kuwaadhibu wauwaji.29
Inawezekana pia hata kule kukubali kwa Ali kuwa Khalifa kunatokana na woga kwa sababu walipomtaka mara ya kwanza awe Khalifa kabla ya hao wauwaji kumuua Khalifa Uthman alikataa.30 Si hivyo tu lakini alipoona wanamsonga kutaka kumshirikisha katika mzozo wao alihama Madina na kwenda Ahjar sehemu maili chache kutoka Madina.31 Ingawa pia tukio hili linaonekana kumuweka Ali mahali pabaya.
Utaratibu wa kuingia katika uongozi wa dola ulizidi kuharibika alipouwawa Ali na mwanae mkubwa, Hassan akateuliwa kuwa Khalifa wa tano. Lakini Muawiyah alipopata habari hizi aliivamia Iraq. Hassan nae kwa upande wake alimteua Qays kuongoza majeshi ya kupigana na Muawiyah. Kulitokea uvumi kuwa Qays ameuwawa na hali hii ilipelekea majeshi ya Khalifa kumgeukia mwenyewe. Hassan alielewa hali ilivyokuwa mbaya hivyo alisalimu amri kwa Muawiyah, akaacha Ukhalifa kwa makubaliano kuwa atapofariki amuachie nduguye, Hussein ukhalifa. Baada ya makubaliano haya na Muawiyah, Hassan alirudi Madinah lakini aliuliwa kwa sumu aliyolishwa na mmoja wa wake zake kutokana na ushawishi wa Yazid.32 Huu ndio ulikuwa mwisho wa Hassan mjukuu wa Mtume.
Taratibu zote hizi ni za kupora madaraka kama alivyofanya Muawiyah ingawa alishinda kivita, kuwekeana makubaliano na watoto wa Ali, Hassan kuwa atamwaachia madaraka Hussein baada ya kufa kwake, na utaratibu wa kurithishwa, taratibu zote hizi, hazikubaliki katika Uislamu ingawa mfumo huu wa mwisho ndiyo uliyotumika katika utawala wa Banu Umaya, Banu Abbasi na Fatimiya.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa
Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 232
Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitabu cha Afya
👉4 Kitau cha Fiqh
Je Qur-an ilikusanywa na kuandikwa katika msahafu wakati wa uongozi wa Abu-Bakr(r.a)
Je Qur-an ilikusanywa na kuandikwa katika msahafu wakati wa uongozi wa Abu-Bakr(r. Soma Zaidi...
Muhammad hakufundishwa quran na padri Bahira
Soma Zaidi...
MAANA YA HADITHI SUNNAH
Maana ya SunnahKilugha: Neno sunnah katika lugha ya Kiarabu lina maana ya mwenendo au mila. Soma Zaidi...
.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu
3. Soma Zaidi...
UJUMBE WA SIRI KWENYE KITABU CHA AJABU
Soma Zaidi...
Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...
Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...
SIKILIZA QURAN KUTOKA KWA WASOMAJI WA TANZANIA
Soma Zaidi...
Chanzo cha vita vya Ngamia Vita Kati ya Bibi Aisha na Khalifa Ali
Soma Zaidi...
jamii somo la 34
Soma Zaidi...