Imam Abu Hanifah
Imam Abu Hanifah ndiye anayenasibishwa na madh’hab ya Hanafi. Jina lake kamili ni Nu’man bin Thabit Abu Hanifah. Imam Abu Hanifah alizaliwa Kufa, Iraq katika mwaka wa 80 baada ya Hijrah. Yeye ni katika watu wa kipindi cha Tabiin kwani aliwashuhudia maswahaba wa Mtume ikiwa ni pamoja na Khalifa bin Abu Taalib, Anas bin Malik na Sahl bin Sa’d. Alipata elimu katika miji ya Kufa na Basra kisha Makka na Madinah. Miongoni mwa waalimu wake alikuwa Abdallah bin Umar mtoto wa Khalifa Umar bin Khattaab. Pamoja na kujikusanyia elimu nyingi na umaarufu kutokana na elimu na ucha Mungu wake; Imam Abu Hanifah alibakia kuwa mnyenyekevu na mwenye msimamo usiotetereka.
Mwaka 146 A.H Khalifah Mansur alimteua Abu Hanifah awe Kadhi; lakini alikataa akitoa hoja kuwa nafasi hiyo ni nzito kuliko uwezo wake. Mansur alikasirika na kumwambia Imam Abu Hanifah kuwa ni mwongo. Imam Abu Hanifah alimjibu, “kama mimi ni mwongo basi kauli yangu kuwa sifai ni sahihi kwani mwongo hawezi kuchaguliwa kuwa Kadhi”. Mansur alikasirika zaidi na kumtupa gerezani Imam Abu Hanifah.
Hata hivyo, kutokana na vilio vya watu ilibidi Mansur aruhusu Imam Abu Hanifah aendeshe darsa hapo hapo jela. Lakini alivyoona watu wanazidi kufurika jela kuhudhuria darsa, alimpa sumu Abu Hanifah akafa katika mwezi wa Rajab 150 A.H., miaka kumi na nane (18) tangu Abbasids kushika mamlaka.
Jeneza lake liliswaliwa mara sita na kila mara watu zaidi ya hamsini elfu walisimama kumswalia. Na hata baada ya kuzikwa watu toka sehemu mbalimbali duniani walifurika kuja kuswali swala ya jeneza.
Umeionaje Makala hii.. ?
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba.
Soma Zaidi...Historia na sifa ya Mtume Muhammad s.a.w , sehemu ya 14. Hapa utajifunza kuhusu kazi alizozifanya Mtume s.a.w Enzo za ujana wake kabla ya utume.
Soma Zaidi...KUJENGWA UPYA KWA AL-KA’ABAHItambulike kuwa Al-ka’abah ndio mjengo wa kwanza kujengwa duniani.
Soma Zaidi...hii ni historia ya vita vya Muta. Katika makala hii utajifunza sababu ya vita hivi na yaliyojiri katika uwanja wa vita.
Soma Zaidi...MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU).
Soma Zaidi...