Kuzaliwa kwa Musa(a.s) na kukua kwake na maisha ya ujana wake na kupata Elimu
Musa(a.
Kuzaliwa kwa Musa(a.s) na kukua kwake na maisha ya ujana wake na kupata Elimu
Musa(a.s) alizaliwa wakati bado msako unafanywa na askari wa Firauni kumwua kila mtoto wa kiume wa Kiisrail anayezaliwa. Kwa rehema zake Allah(s.w) mama yake Musa alijifungua bila kutambulika kwa askari wa Firauni. Na ili kumlinda zaidi Allah(s.w) alimteremshia Wahy mama yake Musa.
Ya kwamba mtie sandukuni, kisha litie mtoni, na mto utamtupa ufukoni ili amchukue adui yangu na adui yake (amlee kwa vizuri Naye ni Firaun). Na nimekutilia mapenzi yatokanayo kwangu (ili upendwe na watu wote), na ili ulelewe machoni mwangu.(20:39)
Baada ya kumtupa mtoni, mama yake akamtuma dada yake Musa kufuatilia:
Akamwambia dada yake: “Mfuate”. Basi yeye akamwangalia kwa mbali bila wao kumjua (28:11)
Kitoto Musa kiliokotwa na kufikishwa kwa Firaun. Mkewe Firaun akamrai mumewe kuwa wasimuue bali wamfanye mtoto wao wa kulea.
Na mkewe Firauni akasema (Kumwambia mumewe) “Usimuuwe, atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako; na msimuuwe;huwenda atatunufaisha, au tumpange kuwa mtoto wetu,walisema haya hali ya kuwa hawatambui(kuwa atakuwa adui yao)”(28:9)
Watu wa Firauni walipomwokota Musa bila shaka walitambua kuwa ni mtoto wa Kiisrail na walimpeleka kwa Firauni ili auawe kama watoto wengine Wakiisrail. Lakini mke wa Firauni alivutiwa na uzuri wa mtoto Musa. Ambaye kwa kweli Allah(s.w) alimfanya awe ni mwenye kupendeza machoni kwa watu. Allah(s.w) Ajaalia Musa(a.s) Kunyonyeshwa na Mama Yake Mzazi
Kwa uwezo wake, Mwenyezi Mungu aliharamisha Musa asinyonyeshwe na yeyote yule isipokuwa mama yake. Hivyo, dada yake Musa alijitokeza nyumbani kwa Firauni na kupendekeza:
“.........Basi akasema: Je nikuonesheni watu wa nyumba watakaomlea kwa ajili yenu, na pia watakuwa wema kwake? (28:12)
Dada yake Musa(a.s) alimpendekeza mama yake ambaye Firauni hawakumjua kuwa ndiye mama mzazi wa Nabii Musa(a.s). Ombi hilo lilikubaliwa na Musa(a.s)alirejeshwa kwa mama yake:
Basi tukamrejesha kwa mama yake ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike; na ajue ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, lakini watu wengi hawajui (28:13)
Allah(s.w) Amruzuku Musa(a.s) Elimu
Ili kuweza kutekeleza jukumu la kutetea haki za binadamu na kuwaongoza watu katika njia iliyonyooka, Mwenyezi Mungu akamjaalia Musa elimu ya kutosha na akili yenye upeo mkubwa wa kupembua mambo. Tunafahamishwa kuwa:
Na Musa alipofikia baleghe yake na kustawi, tulimpa akili na elimu, na hivi ndivyo tunavyowalipa watu wema (28:14)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 kitabu cha Simulizi 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
HISTORIA YA BI KHADIJA (HADIJA) MKE WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAAD (S.A.W)
HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)
(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.
Soma Zaidi...Mafunzo yatokanayo na mkataba wa aqabah katika kuandaa ummah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Historia ya kujengwa kwa Alkabah (Maka)
Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a.
Soma Zaidi...