picha

Kisa cha Malkia wa Sabaa.

Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen.

Kisa cha Malkia wa Sabaa.

Kisa cha Malkia wa Sabaa.


Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen. Watafiti wa mambo ya historia na geografia wanasema Sabaa ilikuwa kiasi cha umbali wa maili hamsini kutoka mji wa Sanaa. Watu wa Sabaa walikuwa wakiabudu Jua na walimfanya mtawala wao kuwa ni mwanamke - malikia.



Pamoja na ushirikina wao, Allah(s.w) aliwaneemesha watu wa Sabaa kwa kila kitu walichohitajia katika maisha yao. Nabii Sulaiman aliwafahamu watu wa Sabaa kupitia kwa ndege Hud-Hudi kama aya zifuatazo zinavyobainisha:



"Na akawakagua ndege (na usimuone kidege Hud-Hud) akasema: "Imekuwaje mbona simuoni Hud-Hudi, au amekuwa miongoni mwa wasiokuwepo (hapa leo)". "Kwa yakini nitamuadhibu adhabu kali au nitamchinja au ataniletea hoja iliyo wazi (ya kumzuilia kuja hapa leo)." "Basi hakukaa sana mara (Hud-Hudi akafika) akasema (kumwambia Nabii Suleiman) Nemegundua usilogundua, na ninakujia hivi kutoka (nchi inayoitwa) Sabaa na (nakuletea) habari yenye yakini"."Hakika nimekuta mwanake anawatawalia; naye amepewa kila kitu na anacho kiti cha enzi kubwa"."Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia (ya kheri), kwa hivyo hawakuongoka" (27:20-24).



Baada ya taarifa hizo Nabii Sulaiman alituma ujumbe kumnasihi malkia aingie katika Uislamu. Awali malkia baada ya kushauriana na mawaziri wake aliona apoteze lengo la Sulaiman kwa kumpa zawadi. Lakini lengo la Mitume ni kufikisha ujumbe wa Allah si kuchuma. Kwa hiyo Nabii Sulaiman alimrejeshea zawadi zake na akaendeleza harakati za kumvuta malkia katika haki mpaka akasilimu. Habari hizi zimebainishwa kwa urefu katika aya Qur’an(
27:27-44).



Jambo tunalotakiwa tulizingatie hapa ni ule msimamo thabiti wa Nabii Sulaiman katika kazi ya kuwalingania watu. Mara nyingi watawala hulewa tamaa ya kujilimbikizia madaraka na mali wakasahau wajibu wao mbele ya Muumba wao. Malkia wa Sabaa alidhani kwa kutumia mali angemtoa Nabii Sulaiman kwenye lengo lake. Lakini haikuwa hivyo.



Hali hiyo si kwa viongozi tu na wakuu wa nchi, bali hata sisi tulio katika harakati za Da'awah tuwe makini tusitolewe kwenye lengo kwa hongo ya mali au wadhifa.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Views 3492

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰3 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰4 ai web app     πŸ‘‰5 web hosting     πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Kuhajiri Waislamu wa Makka Kwenda Madinah

Baada ya mikataba miwili ya β€˜Aqabah na baada ya Waislamu 75 kufika Yathrib salama, Mtume(s.

Soma Zaidi...
Uendeshaji wa dola ya uislamu madinah

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
tarekh 08

KULELEWA NA MAMA YAKE ALIPOFIKA MIAKA MINNEMtume (s.

Soma Zaidi...
Mtume kumuoa bi khadija

Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija.

Soma Zaidi...
Nasaba ya Mtume Muhammad S.A.W na familia yake.

Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 1

Soma Zaidi...