HISTORIA YA MTUME SULAIMAN(A.S)
Sulaiman(a.
HISTORIA YA MTUME SULAIMAN(A.S)
Sulaiman(a.s)alikuwa mtoto wa Nabii Daudi(a.s) na pamoja na kuwa Mtume alirithi pia kiti cha ufalme wa baba yake. Ufalme wake ulidumu kati ya mwaka 965 B.C. hadi 926 B.C. Ufalme wake ulienea Palestina ya leo, Transjordan na baadhi ya eneo la Syria. Qur'an inamtaja Sulaiman kuwa mrithi wa Nabii Daudi(a.s) katika aya zifuatazo:
"Na Sulaiman alimrithi Daudi na akasema: Enyi watu! Tumefundishwa (hata kutambua) usemi wa ndege na tumepewa kila kitu, hakika hii ni fadhila iliyo dhahiri" (27:16).
"Na tukampa Daudi (mtoto anayeitwa) Sulaiman, aliyekuwa mtu mwema, na alikuwa mnyenyekevu mno" (38:30).
Nabii Sulaiman(a.s) anatajwa katika historia kama mfalme ambaye haujapata kutokea uflame mkubwa kama wake. Mwenyezi Mungu alimpa uwezo hata wa kumiliki majini. Walimtumikia katika
kazi zake mbali mbali. Ufalme huu unatajwa kuwa Nabii Sulaiman(a.s)aliupata baada ya kumuomba Mola wake ampe ufalme ambao hataupata mwingine yoyote baada yake.
"Akasema: Mola wangu! Nisamehe na unipe ufalme, asiupate yoyote baada yangu. Bila shaka wewe ndiwe Mpaji" (38:35).
Dua hii Nabii Sulaiman(a.s) anaiomba akiwa tayari ni mfalme. Lakini baada ya hapo ndio ufalme wake ukapanuka, kama aya zinazofuatia aya zinavyobainisha:
"Basi tukamtiishia upepo unaokwenda pole pole kwa amri yake, anakotaka kufika. Pia na (Tukamtiishia) mashetani, kila ajengaye na azamiaye (lulu). Na wengine wafungwao minyororoni (wanapokhalifu amri zake)" (38:36-38).
Pamoja na ufalme na mamlaka makubwa kiasi hiki aliyopewa Sulaiman,lakini pia alipewa elimu ya kumtambua Allah(s.w) na kupewa utume. Kwa hiyo alikuwa ni mja mwenye shukrani kwa neema hizo alizofadhilishwa:
Na bila shaka tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu (kubwa kabisa na wakamshukuru Mwenyezi Mungu) wakasema: "Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Aliyetufadhilisha kuliko wengi katika waja wake waliomuamini" (27:15).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π2 Dua za Mitume na Manabii π3 Simulizi za Hadithi Audio π4 Kitabu cha Afya π5 Bongolite - Game zone - Play free game π6 ai web app
Post zinazofanana:
Uchaguzi wa Omar (Umar) kuwa khalifa wa Pili baada ya Mtume
Uchaguzi wa βUmar bin Khattab kuwa Khalifa wa Pili.
Soma Zaidi...Allah(s.w) Amnusuru Ibrahim (a.s) na Hila za Makafiri
Pamoja na kudhihirikiwa na ukweli wa udhaifu wa miungu wa kisanamu, watu wa NabiiIbrahiim(a.
Soma Zaidi...Mtume Muhammad s.a.w analelewa na Babu yako ikiwa na umri wa miaka 6
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 9.
Soma Zaidi...