picha

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.

Historia ya Watu wa Mahandaki ya Moto.


Katika Suratul Buruj, kumetajwa kisa cha makafiri waliowatesa wafuasi wa Mitume waliotangulia kabla ya Mtume Muhammad(s.a.w). Makafiri hao walichimba mahandaki na ndani yake wakawasha moto mkubwa kisha wakawa wanawatosa waumini humo mmoja baada ya mwingine. Dhun-Nuwas mmoja



wa waliokuwa wafalme wa Mayahudi; aliingia Najran akiwa na jeshi kubwa ili awalazimishe watu wa Najran wasifuate mafundisho ya Mitume. Watu wa Najran walipokataa kumfuata, alichimba handaki kubwa akawasha moto akawa anamtumbukiza Muumini mmoja baada ya mwingine huku yeye na watu wake wanachekelea. Habari hii inaelezwa katika Suratul-Buruj, kama ifuatavyo:




“(Kuwa) wameangamizwa watu waliowaadhibu Waislamu katika mahandaki. Yenye moto wenye kuni (nyingi). Walipokuwa wamekaa hapo (Waliangamizwa makafiri hao pale wakati walipokuwa) wanatazama yale wanayowafanyia hao Waislamu (walipokuwa wakiwaadhibu). Nao hawajaona baya lolote kwao (Waislamu) ila kumuamini Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda (na) Mwenye kusifiwa. Ambaye ni Mwenye Ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona kila kitu” (85:4-9).



Kisa hiki kimesimuliwa kiwape fundisho na kuwaliwaza waumini wa zama zote; kwamba taabu iwapatayo kutoka kwa makafiri imeanza kuwafikia ndugu zao waliotangulia. Aidha, kutokana na kisa hiki Waislamu wanapata funzo kuwa kubakia na Imani Thabiti na suala la kusimamisha Uislamu katika jamii, kwahitaji juhudi na subira kubwa sana.

Mwenyezi Mungu anawaliwaza Waislamu kuwa makafiri wanaowatesa na kuwaghasi Waislamu hivi leo, atawaadhibu na kuwatesa kweli kweli kama alivyowatesa As-habul- Khudud.




“Hakika wale waliowaadhibu Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, kisha wasitubie basi watapata adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu ya kuungua (barabara)” (85:10). “Hakika kutesa kwa Mola wako ni kukali (sana)” (85:12).



Lakini pamoja na kuliwazwa huko; Waislamu hawatakiwi walale usingizi wasubiri nusura ya Mwenyezi Mungu. Ni wajibu wao wajiandae kwa kila mbinu kupambana na vitimvi vya maadui zao.



“Basi waandalieni (wawekeeni tayari) nguvu mziwezao (silaha), mafarasi yaliyofungwa tayari tayari ili kwazo muogopeshe maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu .................” (8:60).



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1872

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 web hosting    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Makubaliano ya Mkataba wa Al Fudhul

Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 13. Hapa utajifunza historia ya Mkataba wa al fudhul na makubaliano yake.

Soma Zaidi...
Yusufu(a.s) Atupwa afungwa Gerezani

Mkewe Al-Aziz hakumkatia tamaa Yusufu(a.

Soma Zaidi...
Musa(a.s)Kupewa Utume Rasmi

Musa alipotimiza muda, alifunga safari na ahali zake kurejea Misri.

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na maandalizi haya ya ki ilhamu

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Kifo cha Nabii Sulaiman

Pamoja na utukufu na umadhubuti wa ufalme wake Nabii Sulaiman muda wake wa kuishi ulipokwisha aliondoka kama walivyoondoka Mitume,wafalme na wanaadamu wengine.

Soma Zaidi...