Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s)
(i) Allah(s.
Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s) Kutokana na Historia ya Nabii Yunusi(a.s) tunajifunza yafuatayo:
(i) Allah(s.w) ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu, hivyo waumini wamuelekee Allah kumuomba msamaha hata kama wamefanya kosa kubwa kiasi gani.
(ii) Toba inayokubaliwa pamoja na sharti nyingine ni ile inayoletwa kabla ya muda wa hukumu ya adhabu ya Allah (s.w) au kabla ya kufikwa na mauti:
Hawana toba wale ambao hufanya maovu mpaka mauti yamemhudhuria mmoja wao, (hapo) akasema: “Hakika mimi sasa natubu.” Wala (hawana toba) wale ambao wanakufa katika hali ya ukafiri. Hao tumewaandalia adhabu iumizayo. (4:18)
(iii) Katika kazi ya Da’awah (kulingania Uislamu) tusiwakatie tamaa watu bali tuendelee nao kwa kubadilisha mbinu mpaka mwisho wa uhai wetu au mpaka Allah(s.w) apitishe hukumu yake. Tumuige Nabii Nuhu(a.s) kwa subira (alilingania kwa miaka 950) na tusirudie kosa la kukosa subira la Nabii Yunus(a.s).
(iv) Matendo mema na ucha-Mungu, huwa ni sababu ya dua na toba ya mja kuwa kabuli mbele ya Allah(s.w).
“Basi isingelikuwa ya kwamba yeye (Yunus) alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanamuabudu (Allah(s.w) vilivyo) bila shaka angalikaa tumboni mwaka (huyo samaki) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe)”. (37:143-144)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 web hosting 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Nasaba ya Mtume Muhammad S.A.W na familia yake.
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 1
Soma Zaidi...tarekh 4
KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBOTukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Adam(a.s)
(i) Utukufu wa mtu katika Uislamu hautokani na nasaba, rangi,kabila,utajiri ila uwajibikaji kwa Allah(s.
Soma Zaidi...Ukasha bin Mihsan ni Sahaba aliyechangamkia Fursa
Katika somo hili utakwnda kujifunz anamna nambavyo Sahaba Ukasha alivyochangamkia fursa katika mambo ya heri
Soma Zaidi...