Nabii Yunus(a.
Nabii Yunus(a.s) ni miongoni mwa Mitume wa Allah(s.w) waliotajwa katika Qur-an. Yunus(a.s) ametajwa katika Qur-an kwa majina matatu:
(i) “Yunus” (37:139) Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.
(ii) “Dhun-Nun”
Na (Mtaje) Dhun-Nun (Yunusi) alipoondoka hali amechukiwa, na akadhani ya kwamba hatutamdhikisha. Basi (alipozongwa) aliita katika giza (akasema): Hakuna aabudiwaye isipokuwa Wewe, Mtakatifu “Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu (nafsi zao).” (21:87)
(iii) “Sahibul-Hut” (Mmezwa na Chewa)
Basi subiri kwa hukumu ya Mola wako, wala usiwe kama mmezwa na Chewa (Yunusi). (Kumbuka) alipolingana, (alipomwita Mwenyezi Mungu), na hali ya kuwa amezongwa (barabara).(68:48)
Majina ya “Dhun-Nun” na “Sahibul-Hut” yana maana ya “Mwenye kumezwa na samaki (chewa).” Nabii Yunus (a.s) ameitwa majina hayo mawili kutokana na historia ya maisha yake ya Da’awah iliyompelekea mpaka akamezwa na samaki mkubwa (chewa) kisha akatapikwa ufukoni akiwa hai kwa uwezo wa Allah(s.w).
Umeionaje Makala hii.. ?
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W, sehemu ya 7
Soma Zaidi...HISTORIA YA BI KHADIJABi Khadija jinalake halisi ni Khadija bint Khuwald bin Asab baba yake alikuwa ni mfanya biashara.
Soma Zaidi...“Na wasomee khabari za watoto wawili wa Adam kwa kweli, walipotoa sadaka, ikakubaliwa ya mmoja wao na ya mwingine haikukubaliwa Akasema (yule asiyekubaliwa sadaka yake): “Nitakuua”.
Soma Zaidi...Sura na historia ya Mtume Muhammad s.sa. w, sehemu ya 5. Hapa utajifunza kuhusu kuzaliwa kwa Mtume.
Soma Zaidi...MKATABA WA AL-FUDHULBaada ya vita hivi viongozi wa pande mbili hizi waliamuwa wakae chini na wakubaliane kuweka kanun i na utaratibu utakaozuia kutotokea uonevu kama huuu tena.
Soma Zaidi...