image

Vyakula vya kupunguza presha ya kupanda

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula ambavyo vinaweza kupunguza presha ya kupanda

VYAKULA AMBAVYO HUSAIDIA KUPUNGUZA PRESHA YA KUPANDA AMA HULINDA MWILI DHIDI YA PRESHA YA KUPANDA.

Presha ya kupanda inaweza kupelekea athari kubwa na mbaya sana kwenye afya ya mtu. Presha ya kupanda isipotibiwa ama mtu asipofuata masharti ya kuishi na ugonjwa huu madhara makubwa yanaweza kutokea. Kifo, kupasuka kwa mishipa ya damu, kupalalaizi, kuharibika kwa figo na moyo kushindwa kufanya kazi na kupata shambulio la moyo yote haya yanaweza kuwa ni matokeo ya presha ya kupanda pindi isipotibiwa ama mtu asipofata masharti.:-

 

Unaweza kupamana na presha kwa kufuata mashari kama kufanya mazoezi, kula vyakula salama kwa presha, kupunguza misongo ya mawazo, kupunguza kula chumvi, kupunguza uzito, kupunguza ama kuacha sigara na pombe. Miongoni mwa vyakula salama kwa presha ni kama

1.Mboga za majani ambazo zina madini ya potassium kwa wingi. Madini haya ni mujarabu sana katika kulinda na kuimarisha afya ya moyo. Ulaji wa mboga hizi unaweza kuwa ni njia ya kujilinda na presha ya kupanda. Miongoni mwa mboga hizi ni kama spinachi

2.Maziwa: maziwa ni katika vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi na pia yana mafuta kwa uchache. Hali zote mbili hizi ni muhimu kwa afya ya moyo.

3.Ndizi; ndizi ni katika matunda yenye madini ya potassium kwa wingi. Ulaji wa ndizi unaweza kuwa ni msaada mzuri kwa kulinda mwili dhidi ya presha ya kupamda.

4.Mayai

5.Samaki aina ya salmon na wanaofanana nao.

6.Ulaji wa mbegu za mimea kama maboga na alizeti

7.Kitunduu thaumu: unaweza kutumia vitunguu thaumu kwa kula ama kutafuna, ni vyema kufunga mdomo wakati unapotafuna.

8.Makomamanga; unaweza kula atunda hili kama juisi ama kula kawaida.

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2090


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

VYAKULA HATARI KWA VIDONDA VYA TUMBO
Hivi ni vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo. mwenye vidonda vya tumbo hatakiwi kula vyakula hivi Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula zaituni
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula zaituni Soma Zaidi...

Pilipili kali
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za pilipili kali Soma Zaidi...

Dalili za ukosefu wa madini ya iodini (goiter)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za upungufu wa iodini ambapo kitaalamu hujulikana Kama goiter. Goiter Ni Sababu ya kawaida ya goiter duniani kote ni ukosefu wa iodini katika chakula. Nchini Marekani, ambako utumiaji wa chumvi yenye iodini ni j Soma Zaidi...

Faida za kula Zaituni
Matunda ya zamani, matunda ya asili, Zaituni tunda lipendezalo, zijuwe faida zake leo Soma Zaidi...

KITABU CHA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula maboga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maboga Soma Zaidi...

Matunda yenye vitamini C kwa wingi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu matunda yenye vitamin C kwa wingi Soma Zaidi...

matunda
Soma Zaidi...

Habari ndugu naomba kuuliza eti mtu akipaliwa na asali anakufa?
Post hii inakwenda kukujulisha hatari za kupaliwa na asali ama kitu kingine kama muulizaji alivyouliza. Soma Zaidi...

Fahamu tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari
Post hii inahusu zaidi tiba ya lishe ya ugonjwa wa kisukari ni tiba ambayo utumiwa sana na wagonjwa wa kisukari na walio wengi na wamefanikiwa kupona Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Mahindi
Soma Zaidi...