Fahamu vitamini A na kazi zake, vyakula vya vitamini A na athari za upungufu wake

Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene.

Fahamu vitamini A na kazi zake, vyakula vya vitamini A na athari za upungufu wake

VITAMINI A

Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene. Vitamini A ni moja kati ya vitamini vingi. Vitamini vingine ni viamini b, C, D, E, K. unaweza kupata vitamini A sana kwenye mboga za majani za kijani, maini, mayai, maziwa, karoti na spinach. Katika makala hii tutakwenda kuona mengi kuhusu vitamini A, kazi zake, vyakula vya vitamini A pamoja na athari za upungufu wake mwilini:



Yaliyomo:
1.Maana ya vitamini A
2.Kazi za vitamini A
3.Vyakula vya vitamini A
4.Upungufu wa vitamini A
5.Athari za kuzidi kwa vitamini A



Maana ya vitamini A


Vitamini ni aina ya fat soluble vitamini ambayo ni kampaind ogania (organic compound) inayopatikana katika makundi kama retinol, retinal, retinoic acid na provitamin ambazo ni beta-carotene. Vitamini A ni muhimu katika ukuaji, uboreshwaji wa mfumo wa kinga na kuboresha afya ya macho.



Ugunduzi wa vitamini A umeanza toka miaya ya 1816 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Francois Magendie alipokuwa akimfanyia uchunguzi mbwa mgonjwa. Baada ya hapo tafiti mbalimbali zikafata mwaka 1912, 1913, 1918, 1920 na 1939 na 1947. vitamini A vimepewa jina hili katika tafiti za mwaka 1920.



Kazi za vitamini A


1.Husaidia katika afya ya macho yaani kuona
2.Husaidia katika ukuaji
3.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
4.Husaiia katika ukuaji wa mimba na mtoto aliye tumboni
5.Husaidia katika afya ya mifupa
6.Husaidia katika afya ya ngozi
7.Husaidia katika afya ya meno
8.Husaidia katika utengenezwaji wa uteute mwilini.



Vyakula vya vitamini A


1.Maini
2.Karoti
3.Viazi vitamu
4.Spinachi
5.Maboga
6.Pilipili
7.Maembe
8.Njegere
9.Maziwa
10.Mayai
11.Mboga za majani za rangi ya kijani


Upungufu wa vitamini A


Tafiti zinaonyesha kuwa upungufu wa vitamini A huathiri watoto wanaokadiriwa kufikia 670,000 waliochini ya umri wa miaka mitano kila mwaka. Pia inakadiriwa kuwa watoto katika ya 250,000 na 500,000 wanakuwa vipofu katika nchi zinazoendelea kila mwaka. Tafiti zinathibitisha kuwa chanzo kikuu cha upofu kwa watoto ni upungufu wa vitamini A.



Athari za vitamini A kupitiliza


Endapo mtu atakuwa na vitamini A vingi ndani ya mwili hata vikapitiliza kiwango ambacho mwili unaweza kudhibiti, athari zifuatazo zinaweza kutokea:-
1.Mkusanyiko wa sumu mwilini
2.Kichefuchefu
3.Kuwshwa
4.Kukosa hamu ya kula
5.Kutapika
6.Kuona maluelue
7.Maumivu ya kichwa
8.Kupotea kwa nywele na misuli
9.Maumivu ya tumbo na uchovu



                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 547


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-