Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Vitamini E ni moja kati aya vitamini ambavyo vinapatikana kwenye vyakula, matunda na mboga. Pia unaweza kuvipata kwa njia ya vidonge kutoka kwenye maduka ya madawa. Kama vilivyo vitamini A, B, C, D na K vitamini E navyo endapo vitapungua mwilini kutakuwepo na madhara kiafya. Ijapokuwa upungufu wa vitamini hivi ni aghalabu sana kutokea. Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake.
YALIYOMO:
Maana ya Vitamini E
Mnamo mwaka 1922 wanasayansi wawili kwa majina ya Herbert Mclean Evans na mwenzie Katharine Scott Bishop waligundua vitamini E. baada ya ugunduzi wa vitamini E tafiti mbalimbali ziilifanywa katika kuonyesha ni zipi kazi za vitaini E mwilini. Kwa mfano Mwaka 1946 wanasayansi walikuwa wakifanya tafiti juu ya nadharia inayodai kuwa vtamini E husaidia dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu (coronary heart diseases). mwaka 1949 tafiti zilifanywa kuhusu nadharia ya kuwa vitamini E huweza kusaidia watoto njiti kuwakinga na maradhi kadhaa.
Kazi za vitamini E mwilini
Vitamini E katika miili yetu zina kazi kuu zifuatazo:
Vitamini E bi antioxidant, ndani ya miili yetu husaidia katika kuzuia athari za kemikali mbaya zifiharibu miiliyetu.
Husaidia katika utengenezwaji wa utando wa seli,na kulinda seli dhidi ya uharibifu wa kemikali.
Husaidia katika ukuaji mzuri wa misuli.
Husaidia katika utengenezwaji wa utando maeneo mbalimbali ya mwili kama kwenye neva, mapafu, na maeneo mengine
Upungufu wa vitamini E
Upungufu wa vitamini E hutokea nadra sana lakini tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E vikipungua mwilini vinaweza kusababisha matatizo kwenye mfumo wa fahamu., ukuaji mzuri wa misuli na udhaifu wa misuli. Pia upungufu wa vitamini E unaweza kuathiri macho na hivyo kupelekea mtu kutoona vizuri.
Vyakula vya vitamini E
Tafiti mbalimbali kuhusu vitamini E
Tafiti hizi zilifanya lakini zinahitaji kuendelea zaidi maana bado majibu ya uhakika hayajapatikana juu ya matokeo ya tafiti hizo. Ijapokuwa maneno ni kama hivyo lakini ukweli ni kuwa vitamini E vina faida katika afya zetu:-
1. Mwaka 2017 tafiti zilifanya na kuonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kupunguza udhaifu wa misuli wakati wa kuzeheka
2. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kulinda mtu dhidi ya maradhi ya ubongo kama kusahausahau na kuchanganyikiwa.
3. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E mwilini husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya figo, kibofu, mapafu na korodani.
4. Husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu
5. Husaidia kwa wajawazito
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2877
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Kitabu cha Afya
Faida za kula Palachichi
Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako Soma Zaidi...
Faida za kula ndizi
Somo hiki linakwenda kukueleza faida za kiafya za kula ndizi Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula kungumanga
Soma Zaidi...
Vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo, na vyakula salama kwa vidonda vya tumbo
Makala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Soma Zaidi...
Lishe salama kwa mjamzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu lishe salama kwa mjamzito Soma Zaidi...
Majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi
Posti hii inahusu zaidi kazi ya majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi, pamoja na kutibu saratani mbalimbali na upambana na fangasi na bakteria kama tutakavyoona. Soma Zaidi...
VYAKULA HATARI KWA VIDONDA VYA TUMBO
Hivi ni vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo. mwenye vidonda vya tumbo hatakiwi kula vyakula hivi Soma Zaidi...
Faida za uyoga mwekundu
Posti hii inahusu zaidi faida kuhusu uyoga mwekundu ni uyoga unaopatikana katika sehemu mbalimbali na pia kuna waliofanikiwa kupandikiza na kuweza kuvuna ila uyoga huu una siri mbalimbali kama tutakavyoona. Soma Zaidi...
Asili ya Madini ya shaba
Posti hii inahusu zaidi asili ya madini ya Shaba, ni sehemu ambapo madini ya Shaba yanaweza kupatikana ni katika mimea na wanyama Soma Zaidi...
Vyakula gani ambavyo sitakiwi kula kama nina pressure ya kupanda
Post hii itakufundisha kwa ufupi vyakula vya kuviepuka kama una presha ya kupanda. Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula Pera
Soma Zaidi...
Karanga (groundnuts)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula karanga Soma Zaidi...