vyakula vya kuongeza damu, dalili zake na sababu za upungufu wa damu
Zijuwe sababu za upungufu wa damu, dalili za upungufu wa damu na kazi za damu mwilini,n avyakula vya kuongeza damu

Upungufu wa damu, dalili zake na vyakula vya kuongeza damu
VYAKULA VYA KUONGEZA DAMU
Damu ni tishu iliyo katika kimiminika. Katika miili yetu damu ina kazi ya kusafirisha viinilishe na hewa ya oksijeni na kuondoa hewa chafu ya kabonidaiyoksaidi mwilini. Pia urekebishwaji wa joto na usafirishwaji wa homoni ndani ya mwili hutegemea damu. Kwa ufupi damu in akazi nyingi. Upungufu wowote wa damu mwilini unaweza kuleta athari nyingi mbaya za kiafya mwilini. Makala hii inakwenda kukueleza njia ya kuongeza damu kwa haraka.
Kazi za damu mwilini
1.Kusafirisha viinilishe kutoka katika mfumo wa mmengโenyo wa chakula kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
2.Kusafirisha hewa ya oksijeni kutokakwenye mapafu kwenda maeneo mengine ya mwli.
3.Kusafirisha hewa ya kabonikaiyoksaidi kutoka kwenye seli na kpeleka kwenye mapafu kwa ajili ya kutolewa nje
4.Kudhibiti joto la mwili kwa kulipooza inapohitajika na kuliongeza inapohitajika
5.Kusafirisha homoni kwenda maeneo mbalimbali ya mwili.
Vyakula vya kuongeza damu mwilini
1.Nyama nyekundu kama nyama ya ngโombe, mbuzi. Kondoo
2.Maini
3.Nyama ya figo
4.Mboga za rangi ya kijani kama mchicha na apinachi
5.Maharagwe
6.Kunde
7.Mayai
8.Nafaka nyinginezo
9.Njegere
10.Koeosho na karanga
11.Samaki
12.Nyama ya ndege
13.Karoti
14.Matikiti
15.Zabibu
16.Viazi vitamu
17.Matunda yenye uchachu kama machungwa, ndimu na limao.
18.Polipili nyekundu
Dalili za kupungua kwa damu mwilini
1.Uchovu wa hali ya juu
2.Udhaifu wa mwili
3.Ngozi kuwa na rangi ya njano au mauko
4.Kupumua kwa shida
5.Mapigo ya moyo kutokuwa ya kawaida
6.Kizunguzungu na kichwa kuhisi chepesi
7.Maumivu ya kifua
8.Miguu na mikono kuwa ya ubaridi
9.Maumivu ya kichwa
Sababu za upungufu wa damu mwilini
1.Upungufu wa madini ya chuma mwilini
2.Upungufu wa vitamini A na B-12 mwilini
3.Maradhi kama HIV, UKIMWI, saratani, mardhi ya figo haya huweza kuleta upungufu wa damu
4.Mfumo wa kinga mwilini kuuwa na kuharibu seli hai nyekundu (autoimmune)
5.Uharibifu wa seli hai nyekundu kufanyika kwa haraka kuliko utengenezwaji.
6.Kuwa na maradhi ya sickle cell
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 ai web app ๐2 Kitau cha Fiqh ๐3 Bongolite - Game zone - Play free game ๐4 Dua za Mitume na Manabii ๐5 kitabu cha Simulizi ๐6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Zijue Faida ya kula tunda la tango.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida za kula tango japokuwa watu wengi hulipuuzia Ila Lina Faida kubwa Sana mwilini.
Soma Zaidi...Faida za kiafya za tangawizi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kutumia tangawizi
Soma Zaidi...Vyakula bora kwa ajili ya afya ya macho.
โMacho ni moja ya viungo muhimu zaidi vinavyokuunganisha na ulimwengu, lakini mara nyingi tunayasahau hadi pale tunapoanza kupata changamoto za kuona. Kama ilivyo viungo vingine, macho yanahitaji virutubisho maalum ili yasibadilike ubora kadiri umri unavyosonga mbele. Makala haya yanakupa orodha ya vyakula bora unayoweza kuingiza kwenye sahani yako leo ili kuimarisha uwezo wako wa kuona
Soma Zaidi...Fahamu vitamini A na kazi zake, vyakula vya vitamini A na athari za upungufu wake
Vitamini A ni katika vitamini fat soluble vitamin akama vile retinol, retinal, retinoic acid na beta-carotene.
Soma Zaidi...