picha

Tufanyeje ili kuepuka kuaribika kwa figo?

Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia kuaribika kwa figo, hizi ni njia zinazotumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuaribika kwa figo na hasa wale ambao hawajapata tatizo hili wazitumie ili tuone kama tutaweza kupunguza tatizo hili.

Fanya hivi ili kuilinda figo yako:

1. kula vyakula vyenye kuupa mwili wako afya. Vyakula hivi ni kama samaki, matunda, mbogmboga na kuepuka vyakula visivyo boresha afya kama vyenye mafuta mengi, chumvi nyingi ama vyenye sukari nyingi.

 

2. fanya mazoezi kwa mara kwa mara. Kufanya mazoezi sio tu kuwa kunaboresha afya ya figo bali kunaboresha afya ya viungo vingine kama moyo, misuli na mifumo mingine ya mwili. Pia mazoezi hufanya mwili kuwa imara.

 

3. hakikisha una uzito wa kawaida. Uzito kuzidi tofauti na kawaida kunaweza kusababisha shida nyingi za kiafya kama hatari ya kuweza kupata kisukari, pia huhatarisha afya ya moyo na figo. hakikisha uzito wako unaendana na urefu wako. Ongea na daktari kujuwa kama uzito wako umeendana na urefu wako.

 

4. Pata usingizi wa kutosha. Mwili unahitaji usingizi kwa ajili ya mambo mengi, usingizi husaidia mwili kutibu majeraha kwa ufanisi, kuboresha mfumo wa kinga na kufanya mwili ku starehe (relax). Mtu akikosa ukisngizi anaweza kuwa katika hatari ya kupata maradhi mbalimbali ikiwepo maradhi ya figo.

 

Njia nyingine za kulinda figo:

1. Wacha kuvuta sigara

2. Punguza kunywa pombe

3. Punguza misongo ya mawazo

4. Hakiisha sukari ya mwili ipo katika hali ya kawaida.

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views 1390

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉4 Dua za Mitume na Manabii     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 web hosting    

Post zinazofanana:

Ugonjwa wa kisonono, sababu zake nanjia za kujilinda.

Kisonono husababishwa na bakteria. Bakteria ya kisonono mara nyingi hupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine wakati wa kujamiiana, ikiwa ni pamoja na kujamiiana kwa mdomo, mkundu au uke.

Soma Zaidi...
Dalili za mtu aliyekula chakula chenye sumu

Post hii inahusu zaidi mtu aliyekula chakula chenye sumu, chakula chenye sumu ni chakula ambacho kikitumiwa na mtu yeyote kinaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu hata kifo.

Soma Zaidi...
Maumivu ya tumbo chini ya kifua, upande wa kulia na chini ya kitomvu.

Afya ya tumbo ni ishara tosha ya umadhibuti wa afya ya mtu. Maradhi mengi wanayouguwa watu chanzo kile mti anachokula. Yapo maradhi sugu kama saratani ambayo husababishwa pia na vyakula. Post hii itakwenda kujibu swalo la muulizaji kuhusu maumivu ya tumbo

Soma Zaidi...
Dalili za Ugonjwa wa mapafu.

posti hii inahusu dalili za ugonjwa wa mapafu.ambapo kitaalamu hujulikana Kama Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu yako. Majimaji mengi kw

Soma Zaidi...
Dalili za Ugonjwa wa ini

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa inni, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye ugonjwa wa inni, Dalili zenyewe ni kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa surua kwa watoto.

Surua ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na homa na upele mwekundu, unaotokea utotoni. Wakati mtu aliye na virusi akikohoa au kupiga chafya, matone yaliyoambukizwa huenea angani na kutua kwenye sehemu zilizo karibu. Mtoto anaweza kupata virusi kwa ku

Soma Zaidi...